TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

TANZIA: Mufti Issa Shaaban Bin Simba afariki Dunia

Wakuu kuna taarifa kuwa mufti wa Tanzania amefariki katika hospitali ya TMJ. Mwenye taarifa kamili atujuze.
 
13822_1067191123309955_96896253477347580_n.jpg


Muda mfupi uliopita nimepata taarifa kuwa kiongozi mkuu wa waislamu nchini Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia.

Hakika ni majonzi na pigo kubwa kwa Waislam na watanzania kwa ujumla.
Amezaliwa Shaaban na ameondoka ndani ya mwezi wa Shaaban,
Innalilah wainailah Rajiun.

Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti na amjaalie pepo ya kheri na kumsamehe madhambi yake.
The Grand Muft of Tanzania has passed away.

Chanzo: Abdul Mohamed

 
Kwa Mungu tumetoka na kwake tutarejea.

Pumzika kwa Amani Mufti.
 
RIP Mufti wetu. Misimamo yako yenye kujali utu, utaifa, umoja, na mshikamano wa kitaifa kwa hakika ni alama njema uliyotuachia. Upumzike kwa amani Sheikh. Maziko sijui ni saa ngapi na wapi nikamzike kiongozi huyu muadilifu.
 
RIP MUFTI WETU,
Poleni sana Watanzania wote, Mungu awape faraja ya kweli.
 
Muda mfupi uliopita nimepata taarifa kuwa Kiongozi Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia.

Hakika ni majonzi na pigo kubwa kwa Waislam na watanzania kwa ujumla. Amezaliwa Shaaban na ameondoka ndani ya mwezi wa Shaaban,Innalilah wainailah Rajiun.

Mwenyezi mungu ampe kauli thabiti na amjaalie pepo ya kheri na kumsamehe madhambi yake.

The Grand Muft of Tanzania has passed away.

Wote njia moja kila mtu na muda wake. Ila mkuu kulikuwa kuna haja gani kutumia kiingereza hapo chini?
 
RIP mufti Simba, poleni waislamu , poleni familia.
 
TANZIA: Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba afariki dunia leo Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, BAKWATA yathibitisha.
 
Back
Top Bottom