TANZIA: Mchoraji wa katuni za Sokomoko afariki dunia

TANZIA: Mchoraji wa katuni za Sokomoko afariki dunia

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Mchora katuni maarufu ya SOKOMOKO Thaddei Thomas Marealle, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Kairuki, taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa kaka ake William G Marealle Mikocheni jijini Dar es Salaam

641418775.jpg

​
=====

Marehemu alijipatia umaarufu kupitia Katuni za Sokomoko zilizokuwa zikichapishwa kupitia gazeti la Sani lililojipatia umaarufu sana miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000

Kupitia gazeti hilo zilikuwepo katuni nyingine maarufu kama vile Kifimbo, Kipepe, Harakati a Pimbi, Ndumila kuwili, Lodi lofa, Madenge, Sukununu za babu Sani, Bush Star na Born Town.
 
Nyuma Yako; Mbele Yetu
Tangulia tu mzee wetu
Mzee wa vigaragosi tupu
Mzazi wa Sokomoko mlevi
Umetuachia simamzi kuu
Burudani tutaikosa walahi
Visa na mikasa ya mlevi
Mlevi mbwa awazaye ulevi
Iwe asubuhi au mchana
Tangulia mkuu wetu mwema
Mungu akupe pumzisho jema
Amina Amen Na Iwe Hivyo
 
Hili jina Sokomoko linanikumbusha msichana mmoja tulisoma nae primary akiitwa Flora Gikalo..akaambiwa ataje list ya mawaziri wakuu Wa nchi hii...kufika kwa Sokoine akakwama..akaropoka Sokomoko...aisee hilo jina tumemuita mpaka tuko tunabalehe..sijui yuko wapi!?

RIP sokomoko!
 
Back
Top Bottom