TANZIA Lee "Scratch" Perry, mtayarishaji nguli wa Reggae, afariki dunia akiwa na miaka 85

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Perry.jpg


Pigo lingine laufika muziki wa Reggae. Mwimbaji na mtayarishaji nguli wa muziki wa Reggae, Lee "Scratch" Perry, ameondoka akiwa na miaka 85.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness, Lee, ambaye jina lake halisi ni Rainford Hugh Perry, aliaga dunia tarehe 29 Agosti, 2021 katika hospitali huko Lucea, Jamaica.

Lee "Scratch" Perry ni nani?
Perry alizaliwa tarehe 20 Machi 1936 huko Kendal, Jamaica, katika parokia ya Hanover, akiwa mtoto wa tatu katika familia. Mama yake, ambaye alikuwa na asili ya Kiyoruba, alishikilia kwa karibu mila za Kiafrika.

Akiwa bado kijana, Perry aliamua kuwa maisha ya kufanya kazi ngumu za shamba hayakuwa yake. Kuhusu hili aliwahi kunukuliwa akisema: "Hakukuwa na kitu cha kufanya isipokuwa kazi za shamba, kwa hivyo nilianza kucheza dominoes na nikajifunza kusoma akili za wengine."

Perry Alianza safari yake ya muziki mwaka 1950 na baadaye kufanya kazi katika studio kadhaa za kurekodi kama vile Studio One iliyomilikiwa na Clement Coxsone Dodd, pamoja na Amalgamated Records ya Joe Gibbs. Mwaka 1973 Perry alianzisha Black Ark studio nyumbani kwake na kufanya kazi na wasanii wakiwemo Bob Marley and The Wailers, The Beastie Boys na The Clash.

Baadhi ya nyimbo maarufu zilizopikwa kwa mikono ya Perry ni kama vile Small Axe, Duppy Conqueror za The Wailers, War Ina Babylon (Max Romeo), Curly Locks na Beat Down Babylon (Junior Byles) na Police And Thieves, hit kubwa sana iliyofanywa na Junior Murvin.

Perry 1.jpg

Perry alikuwa mwanzilishi wa muziki wa dub katika miaka ya 1970 na alitengeneza rekodi zaidi ya 1,000 zaidi ya miaka 60. Perry alifahamika pia kwa majina kama vile "Upsetter" na "Mad Scientist."

Tofauti na muziki, Perry alifahamika pia kwa mtindo wake wa uvaaji wa kipekee na haiba (personality) yake ambayo wengi wamekuwa wakimuona kama mtu aliyechanganyikiwa. Mara nyingi alionekana akiwa kapaka nywele zake rangi, akiwa kavaa pete nyingi na nguo zenye rangi nyingi za kung’aa, huku akipenda kuzungumza kwa vina na kwa mtindo ambao huenda usimuelewe tafsiri yake usipotuliza akili.

Mnamo mwaka 2003, Perry kupitia albamu yake ya Jamaican E.T, alishinda Tuzo ya Grammy kipengele cha Albamu Bora ya Reggae.

Clothes.jpg

Wakati sifa na umaarufu wake ukikua, Lee alipata shida (inayosemekana ya kiakili) na akateketeza studio yake ya The Black Ark. Baada ya hapo, alihamia Uingereza na kisha Marekani na baadaye kuishia Uswizi, ambapo aliendelea kufanya muziki kwa kasi kubwa.

Kifo cha Perry ni pigo lingine kwa mwaka huu baada ya Msanii wa reggae Bunny Wailer, mmoja wa waanzilishi wa The Wailers aliyefariki akiwa na umri wa miaka 73 pamoja na Ewart Beckford, maarufu kama U Roy aliyefariki Februari mwaka huu akiwa na miaka 78.


Sehemu hii ya documentary inayoitwa Beats of the Heart (1977) Lee Scratch Perry anaonekana katika studio yake ya The Black Ark katika session ya kurekodi akiwa na The Heptones, The Congos na Junior Murvin.
Perry alikuwa na mizuka sana, mcheki tu na utaelewa. Sessions nyingi za studio alizofanya ambazo nimebahatika kuziona, alikuwa amevaa bukta na vest, nadhani ni kwakuwa alikaa muda mwingi kupika hits ndani ya studio katika nchi yenye joto kali.

Kwa muda ambao nimekuwa interested na Reggae, nimepata kujifunza mengi sana kuhusu muziki huu. Perry ni mmoja wa ma-genius ambao hawatofutika katika historia ya Jamaica na ulimwengu.

Pumzika kwa amani, Mr. Scratch.
 
Hakuna kitakachosalia chini ya Jua,Apumzike kwa Amani Lee perry.
 
Daaah RIP lee, we gonna miss uu, ni kazi sana kumwelewa huyu ndugu. Ila alikua regend wa Reggae
 
Beats of the Heart (1977) Hii documentary ni nzuri sana ndani yake kuna nyimbo za reggae za zamani nzuri sana.
 
Back
Top Bottom