TANZIA: Kamanda James Kombe afariki dunia

TANZIA: Kamanda James Kombe afariki dunia

Zizuu

Senior Member
Joined
Apr 17, 2013
Posts
136
Reaction score
28
Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kifo hicho Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Advera Senso alisema, Kombe alifariki Oktoba 22 mwaka huu na taratibu za mazishi zinaendelea.

Aidha Senso alisema Marehemu Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.

Baadhi ya vyeo alivyopitia na miaka ya kupata vyeo hivyo katika mabano ni pamoja na Sagenti wa Polisi (1973) Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977), Mkaguzi wa Polisi (1984), Mrakibu Msaidizi (1986), Mrakibu wa Polisi(1991), Mrakibu Mwandamizi (1995), Kamishna Msaidizi wa Polisi (1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu mwaka 2010.

Baadhi ya nafasi alizowahi kuzitumikia katika Jeshi la Polisi ni pamoja na kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika wilaya za Dodoma, Tarime, Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) katika mikoa ya Lindi, Arusha, Kigoma pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza ghasia Tanzania na hadi anastaafu alikuwa mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania.
 
Mbona wanakufa wazalendo wengi vijijini na haitangazwi?Huyu nae ni wa kawaida tu kwani kila nafsi itaonja mauti.Aliwaibia sana watanganyika kwa kula na kupokea rushwa.
 
Ooooooooop,what news is this?mimi nilijua Kamuhanda kumbe Kamanda Kombe,R.I.P kamanda.
 
Mbona wanakufa wazalendo wengi vijijini na haitangazwi?Huyu nae ni wa kawaida tu kwani kila nafsi itaonja mauti.Aliwaibia sana watanganyika kwa kula na kupokea rushwa.
 
Alikuwa anaingia field kabisa........hapa ni pale junction ya Kenyatta.....hu ho haaa (kung-fu)

images
 
RIP Rtd Kombe be blessed along the journey (Ex boss wa Lukosi).
 
Aliekua kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania kamanda Kombe amefariki dunia.

Source: radio uhuru
Natumaini amepata nafasi ya kutubu dhambi maana mpaka hapo aliwaonea wengi-usiulize makofi polisi and the like!!!!!!
RIP
 
ni yule aliyewahi kuwa RPC Arusha?kama ni yeye alisaidia sana kupunguza ujambazi arusha,Rip bwana komandoo.
 
Mmmmh... nilidhani yule Kombe mwenye kesi ya mauaji!


Yule mu uaji wa wale wafanyabiashara wa morogoro ni Abdalla Zombe sio Kombe.

Hata hivyo mi ningefurahi sana kama ningesikia ni Kamhanda, alipo muua Mwangosi akapandishwa cheo.
This is only in Tanzania.

Waziri Celina Kombani naye yupo kimya wakati wale wafanyabiashara wa Madini wa morogoro
walikuwa wanamfadhili kila uuchaguzi tena kwa asilimia kubwa sana. Huyu naye hana shukrani kabisa.
 
Kila mwanadamu ni mdhambi, usimhukumu mtu usije ukahakumiwa, kila dhambi inasamehewa na Mungu kama utaitubu na kuiacha, dhambi isiyosamehewa ni kumkufuru roho mtakatifu...
TUSIMHUKUMU, MUNGU NDIYE ATAMHUKUMU.. R.i.p kamanda kombe... Mungu akurehemu.
 
Back
Top Bottom