TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

  1. Kila mwanadam aliye zaliwa na mwanamke anasiku chache za kuishi duniani nazo zimejatabu na mateso pumzika kwa amani mama yetu kipenzi 😭😭😭😭
 
Leo sijui ni kwanini nimetokea Kukumbuka sana Maneno ya Wahenga hasa huu Msemo usemao Malipo ni hapa hapa Duniani.
 
Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe ameeleza kushtushwa kwake na kifo cha mbunge mwenzao mama Getrude Rwakatare.

Akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Mbowe amemtaja mama Rwakatare kama mtu makini aliyekubalika katika huduma zote alizoshiriki ikiwemo Bungeni, Kanisani na katika sekta ya watoa huduma ya elimu.

KUB Mbowe ametuma salamu za pole kwa Chama Cha Mapinduzi, Kanisa la Mikocheni Assemblies of God na kwa familia ya mama Rwakatare.

RIP mama Rwakatare

Source: Ayo TV

Maendeleo hayana vyama!
 
R.I.P Mama wewe Mbele sisi Nyuma.

my take:
naomba mtu mmoja JF anaedhani , kujiona na kujidai kuwa yeye ni Genius sana ana akili kuliko sote humu na sote tunajua yeye ni mwandishi mzuri basi na ajitolee haraka kuanza kuandika kitabu kwa side effects za Covid19 nchini (economic, social, political, like culture, health, crime, employment, sports, deaths, BP, conflicts, psychological issues, hunger, corruption, prostitution, sanitation, lack of clothing, stress,depression, unwanted pregnancies, HIV Aids, Malnutrition, Education Standards drop , Gender Discrimination, Mimba za utotoni, Domestic Violence manake hivi sasa watoto na baba na mama wote wanagombea Remote Control ni vita ya tatu ya dunia : tv moja!

Mtoto mdogo = Katuni na Mazombi, Baba = TBC na Al Jazeera , Binti na Mama = Sultani, Ruby Ring na Kara Sevda na MTV India! Brazamen = Hollywood Movies, Mtv halisi Music and Boxing!! kazi ipo na hii Corona!!

tutasikia na kuona mengi namuomba Mungu atuondolee Covid19 nchini Tanzania, Amen

wapi Pascal?
Nimecheka hiyo ya kugombania remote, ndio ukweli kila mtu anataka aangalie kinachomuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu siwezi sahau Ni pale nilipoona Mchungaji Rwakatale anashangilia kwa nguvu na kugonga dawati bungeni kufurahia kauli ya Mh. Bulembo kwamba "Zitto Kabwe auawe eti ni msaliti!!!" Siasa hizi Ni Kama pombe, Kuna wanaokunywa akili zikachangamka zaidi positively, Ila Kuna wanaokunywa wanapoteza akili kabisa" Mtumishi gani anafurahia kauli ya mtu kuuawa hata Kama amekosa??! Nilitegemea aombe angalau dakika 3 kwa Speaker ili amuombee Zitto kwa mungu ambadilishe. RIP Rev. Dr. Getrude Rwakatale. Sote wa Mungu na njia Ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakuwa maiti utapewa sifa zote nzuri hata kama sifa zingine hustahili kupewa utapewa ila Mungu ndio atakayejua hatima ya maisha yetu baada ya kifo. Mungu akutendee kulingana na matendo yako uliyotenda hapa dunia. R.I.P mama Lwakatare

DUMU KUBWA
 
Naona umepanick mkuu

Upepo wa kisuri suri na ukufunike jioni ya leo
Baba Swalehe unaongea nini aisee, unawaza kinyumenyume mkuu! watu wakienda kulia wewe kushoto! kwani ulikuwa ukimchukia Mama? kakufanyaje? sio kwamba tuna ya kujifunza katika maisha yake hasa kukuza elimu kwa shule zake bora sana? au ni yale makofi alipiga bungeni ile si ni mob psychology tu wenzio wakipiga makofi nawewe unapiga au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom