TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,581
6,675
Imethibitishwa Abass Kandoro hatunaye tena. Source inasema alihamishiwa Hospitali ya Muhimbili mapema leo baada ya hali yake kubadilika katika Hospitali Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Kandoro amewahi kuwa katika nafasi ya ukuu wa Mkoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza Singida na Mbeya.

Abbas Kandoro.JPG


PMO_0585-768x512.jpg
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipomtembelea Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

********************** UPDATES I Aprili 28, 2018 ************************
Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu jamaa na marafiki wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro.

Mkandoro.jpeg

----
Kandoro Manyema.jpg
Mwili wa Abas Kandoro ukiingizwa kwenye msikiti wa Manyema kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea nyumbani kwake Mbweni utakapoagwa na kusafirishwa kuelekea kijiji cha Ihemi mkoani Iringa kwa mazishi yatakayofanyika hapo Kesho.
 
Back
Top Bottom