TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Pole kwa wafiwa, hakika tutamkumbuka kwa uadilifu wake na kupigania haki za wanyonge, msema kweli asiye pindisha wala kupotosha.Mungu ailaze roho yake peponi.
 
Wadi wasi wako nini mkuu, mimi mkono unenda kinywani bila tatizo.
Hayo mengine lala nayo

Mimi sina wasi wasi wewe ndio unatakiwa kuwa na wasi wasi kwani huko unakojitapa kuwa una pesa nyingi ni kutokana na 10% za contract ya mabehewa mliyowapa wahindi; sasa ngoja wale walioko mahabusu wapande mahakamani na kuwataja ndio mtakapoona uchungu wa wizi!!!
 
Mhe. Kandoro sinto kusahau kamwe. Ulijua uongozi ni nini. Ulitenda haki na kuheshimu watu wote. Ulizingatia haki. Ukubagua mtu kwa itikadi ya chama au dini. Ulikuwa na mapenzi mema kwa nchi yako ya Tanzania. Nakumbuka mara nyingi ulinambia na kuongelea uzalendo kupungua Tanzania.Si vibaya nikatamka hili wakati wa uchaguzi 2010, kulipotokea sintofahamu ya kutangaza matokeo ulikuwa muwazi kumtaka msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo na ulimwambia na kumshauri wazi Rais kuwa Wenje atangazwe japo Masha alikuwa chaguo la Mkuu. Penye haki ulipenda haki itendeke. Lakini ulitumia busara na hekima hasa katika maamuzi magumu. Nakukumbuka ulivyokuwa Mwanza. Yule mzee alie zurumiwa nyumba yake na yule mpemba. Mzee alie kuwa kipofu. Mwenyekiti wa Baraza akaamua anavyoona inafaa baada ya kupewa rushwa na yule mpemba. Nilipokupa taarifa ulichukua maamuzi haraka. Lakini baada ya miaka ulipohamishwa nami kuondoka nimepata taarifa yule mzee kipofu ulomtetea alipewa kesi ya uongo na kufungwa na mali yake kuzurumiwa tena. Inaniuma sipo Tanzania, najua ungekuwepo ungemsaidia. Nasikia anateseka gerezani! Mhe. Kandoro, umetangulia wanyonge hawato kusahau. Nakumbuka mengi ambayo uliyafanya na hata uliponambia huko radhi kujiuzuru ukuu wa mkoa kama kikundi fulani cha watumishi kilichokuwa kimejiimarisha kula sahani moja na wakubwa wengine na kuzurumu haki ya wananchi wataendelea kukumbatiwa na wakubwa. Nashukuru Waziri Mkuu na Rais walikusikia. Na kuchukua ushauri wako. Nakumbuka ulivyowakatalia wale wafanya biashara wanaojiita wazee wa jiji walipo kuja kwako na zawadi ya mamilioni ya fedha. Uligoma kuzipokea na kuwakemea. Mhe. Kandoro ni mengi watu wengine hawayajui ila tuliokuwa karibu yako tunajua. Hukua kiongozi fisadi, ulipinga rushwa na udharimu. na kuheshimu misingi ya utu, haki na sheria.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahala pema. Mhe. Kandoro nitakumiss, huku niliko natamani niruke nije walau nikupe heshima za mwisho lakini kutokana na majukumu sinto fika. Pumzika kwa amani. Umeitimisha utumishi wako ulotukuka. Amen!
 
Nimepata khabar kuwa amezikwa leo huko Ihemi-Ifunda-Iringa....na kuwa watu wengi WAMEMSINDIKIZA katika nyumba yake ya milele..
 
Back
Top Bottom