Katibu Mkuu Yakubu aeleza mipango ya Serikali kujenga miundombinu ya michezo nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
740
479
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Serikali imepanga kujenga viwanja viwili vya michezo nchini katika mkoa wa Arusha na Dodoma ili vitumike katika michuano ya Kombe la Afrika mwaka 2027 vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 kila mmoja.

Bw. Yakubu alisema hayo Julai 24, jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa China uliomtembelea ofisi ndogo jijini humo ambapo amesisitiza kuwa kuna fursda ya ushirikiano katika kujenga miundombinu ya michezo katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali imejipanga kuboresha na kukarabati viwanja saba vya Uhuru, Uwanja wa Benjamin Mkapa vya Dar es Salaam, Uwanja wa Sheikh Abeid Arusha, Uwanja wa Sokoine Mbeya, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Mkwakwani Tanga.

Amesema pias Serikali inajenga pia Viwanja vya wananchi kupumzikia katika jiji la Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Arena mbili katika mikoa hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CREC Bw. He Yeting kutoka nchini China amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la kuboresha miundombinu ya michezo hapa nchini kuilingana na mahitaji ya wakati huu.View attachment 2698147View attachment 2698148View attachment 2698149View attachment 2698150View attachment 2698151View attachment 2698152View attachment 2698153
IMG-20230724-WA0165.jpg
 
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Serikali imepanga kujenga viwanja viwili vya michezo nchini katika mkoa wa Arusha na Dodoma ili vitumike katika michuano ya Kombe la Afrika mwaka 2027 vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 kila mmoja.

Bw. Yakubu alisema hayo Julai 24, jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa China
Serekali inakarabati viwanja vya CCM?
 
Back
Top Bottom