MUKAMASIMBA
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 1,655
- 362
acha uongo dunia nzima inalaani vitendo vya hili kundi kuua,kubaka,kupora mali za wa congomani,kupora madini na maliasili,kama wanasimamia haki ni kwa nini wakina ntaganda wako icc!!!na kuna wengine kibao wanatafutwa!!!!
mokala 1989 unanichosha mdogo wangu....kwani mtu kwenda anakotaka shida ipo wapi?hata kama ni ------ au msukuma anahaki ya kuhamia nchi yoyote atakayo...balali (R.I.P)si alikuwa(kama kweli alikufa) mmarekani unajua hilo?usiseme hivo brain drain iliyopo huko bongo pekee inatisha achana na watu wanaohama nchi....wewe siyo mahaka kutuhumu Gen James Kabarebe......watutsi ni watu....Tuache ubaguzi
Mkuu Jasusi zoezi la wahamiaji haramu lilifanyika huko nyuma mwaka 2002 kama sijakosea. Mbona hakukuwa na malalamiko haya? Pili, mbona raia wa nchi nyingine hawalalamika kama Wanyarwanda.Nguruvi3,
Sisi si watoto wadogo. Kikwete aliposema wakimbizi haramu akiwa mkoa wa Kagera kila mtu mwenye akili alijua wanaolengwa ni akina nani. Hata kama Waganda 50 wamekumbwa katika msako huo walioathirika zaidi ni Wanyarwanda, hata wale ambao wameishi Tanzania zaidi ya miaka sitini. Sijaona popote pale zoezi la kuwakamata na kuwafukuza Wachina ambao wana madanguro yao Dar-es-Salaam likiendelea, au Wahindi na wapakistan ambao wanaitana na kupeana ajira katika viwanda wanavyoongoza, au wasomali ambao nasikia wamejaa na kununua mashamba Rufiji. Sijaona. Mpaka nitakapoona hivyo, na muda unazidi kwenda, nitaendelea kuamini kuwa Kikwete alilenga Wanyarwanda kwa sababu za kisasi chake tu kwa Kagame.
kwa wanao-administer.......Wakuuu twende mbele turudi nyuma.......sheria ni sheria tumejiwekea na zingine kuziridhia sisi wenyewe......naona hapa kuna wandugu wanaanza kuzungumza as if hatukutakiwa kuwa na mipaka na as if....kuwa na sheria ni waste of time!!.....really!!.......I'm really shocked!.....hizi ndoto sijui zinatokea wapi.......kama sheria zetu zina kasoro hilo ni jambo jingine...lakini sheria zimewekwa ili ZITULINDE kwa kila hali......thats all!Mkuu,
.....Kuna tofauti kati ya kuwa na sheria na jinsi hizo sheria zinavyokuwa administered. ............
Hivi, wewe kwa akili zako timamu unaweza kulaani kabila zima au jumuiya nzima kwa vitendo vya wachache? Kwa sababu Ntaganda yuko ICC basi Watusi wote au wanyarwanda wote wenye asili ya kitutsi ni guilty? Mkimaliza kuwahukumu Wanyarwanda mtageukia akina nani tena? Kwa sababu dhambi ya ubaguzi wa kikabila ni kama kula nyama ya mtu.
kama hilo kundi ni la kutetea watu ni kwa nini kila mtu anakana kuhusika nalo si rwanda,si uganda!!!ni kwanini taasisi za haki za binadamu wanalituhumu kwa mauaji ya kimbari!!!! Ni kwanini jumuiya ya kimataifa inawatafuta viongozi wake!!!!!Tatizo watu kamanyie sio watafiti ilimjue ukweli,hao wanao andika hizo article za kuwafanya M23 Kua wauaji ni hao watu wasiopenda watusi na akina ntaganda kwenda ICC nivisa vya kabila tu akishirikiana na hao wafaransa ili waonejinsi watakavyo waondoa watusi congo,jaribu kufanya utafiti wa kina.
What are we becoming as a people? Mtu anafukuzwa tu kwa kutizama urefu wa pua yake na wembamba? Kikwete is a national disgrace.
Hawa wamekuja baada ya mwaka 1996. Mwaka 1996 wanyarwanda warirudishwa rwanda na burundi. Nakumbuka enzi hizo walikua wana amuru kuimba hata ubeti mmoja wa wimbo wa taifa ama wa tanzania tanzania. Hawa waliopo sahizi ni wajuzi juzi tu, na nifikiri si kweli wanatumia hiyo creteria ya urefu kwani hakuna watanzania warefu? wanaorudishwa ni wahamiaji kweli kweli, sema kuna mapungufu kwa wale walio olewa na kuolewa, lakini majority ni wahamiaji haramu.
Na je umesikia katika walalamishi kwamba yeye ni msukuma, ama mhaya ama mkwele? Tanzania hatuna kabila la wahutu ama watusi. Hivyo yoyote ambaye hajaolewa ama kuoa mtanzania na hana karatasi ni mhamiaji haramu.
Birth certificate, zilikua hazitolewi mahospitalini mtu alipokua anazaliwa kwa sehemu kubwa sana ya Tanzania na tena huko ngara,karangwe na b,mulo zilikuwa hazitolewi kabisa na ilikua haiwezekani kuipata labda kama unataka kujiunga na jeshi,polisi ama chuo. Sasa hao wenye nazo wamezipata lini waweke copy kwenye mtandao. Eti kisingizio zimechukuliwa, wote wamenyang'anywa hata wale waliopitia porini na ng'ombe zao?
Naisubiri hiyo next step.step by step .... hao ni next....tunaanza na majambazi na wapora ardhi wa mikoa ya kagera na kigoma kwanza!
habari hii hapa http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/16173-kiama-cha-jeuri-ya-wahamiaji-haramu
mkoa unatarajia idadi ya watu 52,000. Kwa maana hiyo kulikuwa na sensa iliyokuwa inaendelea chini chini kuwabaini.
Kagera, kigoma na geita : Wahamiaji 1851 wamenaswa wakiwa na magobori 6 na short gun moja
kigoma : 885, magobori 2 na shortgun 1
geita : Wahamiaji 246, gobori 3 na sare za jwtz na kibuyu cha maji.
Kagera : Wahamiaji 750, gobori 52, shortgun 10
wahamiaji na majambazi wametakiwa kusalaimisha silaha zao.
Nchimbi amesema wahamiaji waondoke na ngo'ombe wao bila kunyang'anywa
kanali masawe anasema waliotenganishwa na familia warejee ili kupewa kibali cha muda wakisubiri uraia.
My take
hawa watu wanaosemwa ni masikini wamkeja kusalimisha maisha, hivi wanabeba magobori na short gun za nini?
Mkoa wa kagera tu zimekamatwa short gun 10 ambazo ni ka platoon ka jeshi la msituni.
Kwa hesabu ya haraka hadi sasa zimekamatwa silaha kwa idadi hii
short gun =11
magobori = 64
unaweza kwenda nwilaya nzima ya muheza usipate idadi hiyo ya silaha. Hawa wenzetu ambao si rai wamekuja na silaha nyingi za nini? Hivi hapa kuna huruma ya nini jamani. Fikiria silaha hizo zimetoa roho watanzania wangapi na kwanini tuone ni halali wenye nchi kunyofolewa roho zao na wahamaji haramu.
Idadi ya 52,000 inahitaji kituo cha afya kwa mujibu wa takwimu za kitabibu tanzania. Wtahitaji waganga na manesi, watahitaji shule zaidi ya 20, watahitaji huduma za afya. Kumbuka hawa hawajulikani kama wapo katika idadi ya wananchi. Hii maana yake ni kutumia resource zetu kuwaumiza raia wetu wanaolipa kodi kwa mujibu wa katiba ya jmt kwa hisani ya wahalifu wasiofuata sheria. Hivi hili linahitaji mjadala zaidi.
Wakati wakitumia resource zetu wao wanajitapa kwao wana maendeleo. Kwamba tanzania ni shamba la bibi la kulea watu wa mataifa mengine. Jamani hili hatulioni?
Hivi huyu anayesema ametenganishwa na mkewe na watoto, short gun aliitumia wapi na kwa kibali gani. Ni raia gani wa tanzania anayemiliki short gun. Hili hatulioni kama tatizo tunataka kuwafurahisha wahalifu wakubwa.
Mtu gani anayetafuta hifadhi akiwa na short gun, huyu alikuja mwaka gani? Maaana mwaka 1959 hazikuwepo tanzania na kama zilikuwepo zilikuwa 'strong room'. Tunaambiwa walikuja mwaka 1959 nasi tunaitikia bila chembe ya fikra. Silaha za nini wanabeba hawa kama si kujiandaa na vita?
Watu hawajui kuwa goma ilianza hivi hivi wkafikia malaki sasa wanataka kujitenga. Drc inalipa gharama kwa ujinga tunaotaka kuutetea au kuulea. Hawa ni wahalifu wakubwa halafu tunawapa huruma, please give me a break!
binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja! Hiyo ni dhana ya tanu, na imejengwa katika msingi wa umajumui, pan africanism. Tokea ilipotokea jenerali ulimwengu, pamoja na jamaa wengine kadhaa, kutangazwa kuwa si raia, na wakaondoloewa hadhi zote walizokuwa nazo wakati ule, niliona kwamba tanzania imechukua mwelekeo wa hatari. Kwamba kuna idadi kubwa tu ya watu ambao uraia wao una mashaka, lakini hawasumbuliwi kwa sababu? - ni wenzetu! Hoja kubwa iliyotumika hapo ni msimamo wa jenerali ulimwengu, au tuseme uhusiano wake na system. Alipoanza kuandika mambo yanayokosoa system, tayari akawa kanyea kambi. Lakini tunaweza kujiuliza, hiyo criticism yake ilikuwa na maslahi kwa taifa? Ni kweli alikuwa anawanyima raha watu binafsi - lakini si taifa. Suala la uraia tokea hapo limekuwa likitumiwa kama fimbo ya kuwapiga watu fulani wanaoonekana "kuleta shida". Na haishangazi katika mazingira tuliyonayo, ya kutamalaki kwa ufisadi, wizi, rushwa, ulafi (greed), unyanyasaji na uonevu, basi kuendesha zoezi kama hili la "kusaka wahamiaji haramu" lazima watu watatia ajenda zao za ulaji na wizi. Suala hili ni nyeti, linahitaji umakini, kuzingatia sheria inasemaje, haki za binadamu, lakini juu ya yote ukweli kwamba sisi ni waafrika, tumegawanywa tu kwa sababu za mahitaji ya wakoloni. Hatulazimiki kujigawa kufuata ukoloni ulivyotugawa. Tuanzishe taratibu zetu. Kama ni ujambazi, ushugulikiwe kama ujambazi kwa taratibu za kudumu, siyo operesheni kama hizi zinazoendana na uporaji, wizi, unyanyasaji, na kuonesha jinsi tulivyofilisika kifikra na kifalsafa
Wamepoteza credibility kwa kuwa wamekuwa infiltrated. serikali ya Rwanda ina fungu maalum (special fund) kwa ajili ya PR na propaganda. Fungu hili linatumika kulipa international PR agencies ku-engineer habari, interviews na mengineyo ili kuipotray Rwanda in the positive light.Gazeti la The East Africa limepoteza credibility kwasababu ya kutofanya uandishi wa kisomi bali kushabikia tu. Jk hakusema Wanyarwanda, alisema wahamiaji haramu. Ilikuwa ni juu ya mhariri kujitridhisha na madai ya msemaji au kuyaweka sawa na si kushabikia.
Tumeona makala nyingi zinatoka Kigali na zile za Nairobi ni kuongeza chumvi.
Nalipenda gazeti hili lakini limepoteza credibility sana.
Acheni roho mbaya hiyo,mnachotaka nikupora mali zao tu,fikiri hawa munaofukuza nikixazi cha wakimbizi walio ingia tz 1959 nawengi wa wazazi wao wameisha kufa wamezaliwa tz hawajui rwanda na wala hawana ardhi ya kuishi rwanda kwani baada ya kufukuzwa rwanda ardhi zao zilichukuliwa na wahutu,wewe kumfukuza nikama kukufukuza wewe mwenyewe uende nchi ambayo huijui,fikiria hali hiyo,wanasema kabla hujatendea mtu kitu kibaya anza kwanza ujiweke mahala pake.
Habari hii hapa http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/16173-kiama-cha-jeuri-ya-wahamiaji-haramu
Mkoa unatarajia idadi ya watu 52,000. Kwa maana hiyo kulikuwa na sensa iliyokuwa inaendelea chini chini kuwabaini.
Kagera, kigoma na Geita : wahamiaji 1851 wamenaswa wakiwa na magobori 6 na Short gun moja
Kigoma : 885, magobori 2 na Shortgun 1
Geita : wahamiaji 246, gobori 3 na sare za JWTZ na kibuyu cha maji.
Kagera : wahamiaji 750, gobori 52, shortgun 10
Wahamiaji na majambazi wametakiwa kusalaimisha silaha zao.
Nchimbi amesema wahamiaji waondoke na ngo'ombe wao bila kunyang'anywa
Kanali masawe anasema waliotenganishwa na familia warejee ili kupewa kibali cha muda wakisubiri uraia.
My take
Hawa watu wanaosemwa ni masikini wamkeja kusalimisha maisha, hivi wanabeba magobori na short gun za nini?
Mkoa wa Kagera tu zimekamatwa short gun 10 ambazo ni ka platoon ka jeshi la msituni.
Kwa hesabu ya haraka hadi sasa zimekamatwa silaha kwa idadi hii
Short gun =11
magobori = 64
Unaweza kwenda nwilaya nzima ya Muheza usipate idadi hiyo ya silaha. hawa wenzetu ambao si rai wamekuja na silaha nyingi za nini? Hivi hapa kuna huruma ya nini jamani. Fikiria silaha hizo zimetoa roho Watanzania wangapi na kwanini tuone ni halali Wenye nchi kunyofolewa roho zao na wahamaji haramu.
Idadi ya 52,000 inahitaji kituo cha afya kwa mujibu wa takwimu za kitabibu Tanzania. Wtahitaji waganga na manesi, watahitaji shule zaidi ya 20, watahitaji huduma za afya. Kumbuka hawa hawajulikani kama wapo katika idadi ya wananchi. Hii maana yake ni kutumia resource zetu kuwaumiza raia wetu wanaolipa kodi kwa mujibu wa katiba ya JMT kwa hisani ya wahalifu wasiofuata sheria. Hivi hili linahitaji mjadala zaidi.
Wakati wakitumia resource zetu wao wanajitapa kwao wana maendeleo. Kwamba Tanzania ni shamba la bibi la kulea watu wa mataifa mengine. Jamani hili hatulioni?
Hivi huyu anayesema ametenganishwa na mkewe na watoto, short gun aliitumia wapi na kwa kibali gani. Ni raia gani wa Tanzania anayemiliki short gun. Hili hatulioni kama tatizo tunataka kuwafurahisha wahalifu wakubwa.
Mtu gani anayetafuta hifadhi akiwa na short gun, huyu alikuja mwaka gani? maaana mwaka 1959 hazikuwepo Tanzania na kama zilikuwepo zilikuwa 'strong room'. Tunaambiwa walikuja mwaka 1959 nasi tunaitikia bila chembe ya fikra. Silaha za nini wanabeba hawa kama si kujiandaa na vita?
Watu hawajui kuwa Goma ilianza hivi hivi wkafikia malaki sasa wanataka kujitenga. DRC inalipa gharama kwa ujinga tunaotaka kuutetea au kuulea. Hawa ni wahalifu wakubwa halafu tunawapa huruma, please give me a break!