ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 4,452
- 5,669
Tanzania tuko zaidi ya watu milioni 45, ukubwa wa nchi yetu ni km² 945, 087 (laki 9), Taiwani wako milioni 23, ukubwa nchi ya Taiwani km² 36,179 (elfu 36), Mkoa wa Arusha una km² 37 000 (elfu 37)!
Tanzania yetu inazalisha umeme < 1 500 Megawatt wakati Taiwani inazalisha 48 480 MW.
Fikiria hiyo tofauti sisi MW 1500 vs Taiwani MW 48 000, halafu sisi tunakimbizana na vimegawatt 2000 na bado kuna watu wanataka kutushika mashati kwamba tusijenge hata hizo 2000 tusizalishe kwa sababu ya Wanyama, nasema mwambie huyo Muzungu wako aje kuchukuwa hawa Wanyama awapelelke kwao hatuwahitaji tunataka Umeme, ...
Kwanini tusiwaajiri hawa watu wanaongoza hizi nchi tuwalipe vizuri sana, tuwape eneo fulani kama ukubwa wa Singapore tuone wanafanyaje baada ya miaka miwili, mitano tulinganishe na viongozi wetu wazawa.
Kiukweli uwezo wetu wa kufikiri na kufanya vitu vya maana kuweka mazingira sahihi ya nchi kuinuka na kusimama ni mdogo sana. Watu wetu hata ukiwapa miaka 50 hamna chochote cha maana wanachoweza kufanya wako zaidi kisiasa, ubinafsi, ukabila, udini na kwamba mimi ndio mkubwa.
Kiukweli hii nchi ukimpa Msingapore, Emir wa Dubai, Mwingereza inainuka baada ya miaka mitano tu na miaka kumi itasimama imara.
Uchawi upo kwenye mazingira. Mazingira ndio kila kitu. Mazingira, Mazingira, Mazingira.