Tanzania yatoa msaada wa tani 300 Somalia

Calnde

JF-Expert Member
Oct 7, 2008
1,373
277

kufuatia njaa iliyokithiri somalia (haijawahi kutokea ndani ya miaka 60) Tanzania imeahidi kuisaidia Somalia tani 300 za mahindi. Huu ni moyo wa utoaji

na hakika likiwa limefanyika kwa moyo basi Mungu ataibariki Tanzania mara dufu.

Lakini kuna jambo moja tuu linanishangaza, hivi ni kweli Tanzania inawapenda watu wake? Leo bungeni nimewasikia wabunge kama watatu

wanalalamika majimboni kwao kuna njaa kali na chakula walichoahidiwa (iwe cha bure/au cha gharama nafuu/gharama halisi) hakijapelekwa zaidi ya

miezi miwili sasa. Huu ndo mwendelezo tabia ya kujali watu wa nje kuliko wazawa? Sipingi kusaidiwa kwa somalia, maana hakika tunapaswa kufanya

hivyo lakini maneno matakatifu yanasema mtu asiyewajali watu wa nyumbani mwake ameikana imani, ni mbaya kuliko asiye amini! Nawasilisha
 
Kwa ile hali iliyopo Somalia, naunga mkono hoja. Nafikiri tuna reserve ya kutosha ya chakula. Si vibaya tuwasaidie hawa wenzetu. Kwa kweli hali yao ni mbaya sana.
 
Nami nakubaliana nawe mkuu. lazima tuwasupport. But tunasubiri na hapa kwetu hali iwe hivyo ili tutoe hiyo reserve?
 
Hawa watu wanahali mbaya sana. Tuwasaidie kwa misaada na maombi ili tuweze kupata baraka toka kwa Mola.
 
Ndio maana nasema JK ni Rais makini.. zilizobaki chuki binasfi tu
 
Hata nchi wahisani wanavyotoa misaada haina maana wananchi wao wanajitosheleza kwa kila kiti. Kutoa siyo utajiri ni moyo. Hata kama sisi tuna njaa hatujafikia ile ya somalia. Naunga mkono hoja.
 
We can mobilize our internal resources, Tanzania watu wana pesa nyingi, halali na haramu! We can help them, ila tusisubiri wa kwetu wafikie hapo ili na

sie tukaombe msaada South Africa or else where! We must act now!
 
Hata nchi wahisani wanavyotoa misaada haina maana wananchi wao wanajitosheleza kwa kila kiti. Kutoa siyo utajiri ni moyo. Hata kama sisi tuna njaa hatujafikia ile ya somalia. Naunga mkono hoja.

Unaunga mkono hoja ipi boss?
 
Najua mnaongea tu coz hamjawaona watanzania wenzenu wenye njaa,kwasababu nyie mnaishi maisha mazuri kuliko wa tanzania walioko vijijini
 
Ndio maana nasema JK ni Rais makini.. zilizobaki chuki binasfi tu
Kama umakini wa raisi unatokana na msaada anaotoa kwa majirani wakati nchini kwake kuna njaa, basi hata mimi nina sifa ya kuwa rais. Maana nina huruma ile mbaya. Huwa nipo tayari nikose, lakini nimsaidie mwenzangu ambaye yupo kwenye shinda.
 
Najua mnaongea tu coz hamjawaona watanzania wenzenu wenye njaa,kwasababu nyie mnaishi maisha mazuri kuliko wa tanzania walioko vijijini

Muda si mrefu nilikuwa mikoa ya kusini, lindi/mtwara. Asikudanganye mtu watu ni maskini mno. Njaa ipo pengine haijafikia Somalia but hali ni mbaya.

Wazee hawana hata nguo za kuvaa, wanalala kwenye virago. Maji yanapatikana kwa shida mno, machafu na kwa gharama ya sh 500 kwa lita 20.

Huwezi amini wenzetu wanakula panya (not as custom but because of hardship), mbwa, ngombe wanaokufa kwa magonjwa nk. The only source of

income ni korosho, once in a year! Im not amplifying anything here, im presenting what my own eyes have seen!
 
Hivi Raisi wao naye alikuja kutembeza bakuri? Duh. Nilikiri sisi ni waombaji tu, kumbe tunatoaga.
 
Kama umakini wa raisi unatokana na msaada anaotoa kwa majirani wakati nchini kwake kuna njaa, basi hata mimi nina sifa ya kuwa rais. Maana nina huruma ile mbaya. Huwa nipo tayari nikose, lakini nimsaidie mwenzangu ambaye yupo kwenye shinda.

Basi kwa maana hiyo tuna maraisi wazuri wengi Tanzania!
 
Kama wana moyo wa kusaidia kwa nini wanashindwa kufuta tax holidays za matajiri ambayo yanaendelea kujineemesha na umasikini wa Watanzania? Wananchi wamebaki kuwa watumwa kwenye nchi yao.
 
Tutoe msaada wa chakula Somalia,lakini pia tuwatumie watanzania wanaohitaji,pengine tofauti kati ya Tanzania na Somalia ni kiwango cha njaa(tz wanaweza kupata panya) na idadi ya waathirika

Mtu moja mwenye njaa kati ya walioshiba ana thamani sawa na wengi wenye njaa katkati ya wenye njaa
 
Tutoe msaada wa chakula Somalia,lakini pia tuwatumie watanzania wanaohitaji,pengine tofauti kati ya Tanzania na Somalia ni kiwango cha njaa(tz wanaweza kupata panya)na idadi ya waathirika

Mtu moja mwenye njaa kati ya walioshiba ana thamani sawa na wengi wenye njaa katkati ya wenye njaa
 
Back
Top Bottom