Tanzania yatoa msaada wa tani 300 Somalia

Igunga kuna njaa inatishia kuuwa Watanzania, sasa kama Matonya nae siku anasaidia omba omba wenzake basi kweli uchumi wetu unapaa!
 
Wakati wa ziara ya Rais wa Somalia iliyomalizika hivi karibuni hapa nchini, Rais wa Tanzania ameahidi kutoa tani 300 za mahindi kama msaada wa chakula kwa Somalia.

Katika mazingira tuliyonayo sasa hapa nchini, huku mikoa kadhaa ikikabiliwa na ukosefu wa chakula na hivyo tishio la njaa kwa nchi yetu; iweje leo tuanze kugawa chakula kidogo tulicho nacho?

Tulishasikia mara kadhaa kuwa kuna upungufu mkubwa wa chakula katika maeneo kadhaa hapa nchini, hali iliyolazimisha serikali kusitisha uuzwaji wa chakula nje ya mipaka ya Tanzania, na vile vile Serikali kutoa chakula kwenye maghala ya hifadhi ya chakula ya taifa ili kiingie sokoni kupunguza uhaba huo. Inakuwaje leo chakula hicho hicho cha dharula tunakitumia kugawa nje ya nchi?

Unawezaje kutoa damu kwa mgonjwa anayehitaji lita 2 za damu ili apone hali wewe mwenyewe unahitaji lita moja ya damu ili upone?
Siku zote, Wema usizidi uwezo.
 

kikweteutabiri.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete​
Mwandishi Wetu
SERIKALI imetangaza kuwa itatoa msaada wa tani 300 za mahindi, ili kuwasaidia watu 3.5 milioni wa Somalia kupunguza makali ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilieleza kuwa Tanzania pia imeahidi kutoa misaada mingine kwa nchi hiyo kwa kadri uwezo wa nchi unavyoruhusu .

Mchango wa Tanzania umetangazwa wakati wa mazungumzo rasmi kati ya Serikali ya Tanzania na ile ya Jamhuri ya Somalia, na wakati wa futari ambayo Rais Jakaya Kikwete, alimwandalia mgeni wake Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini.

“Tunasikitika sana kuona matatizo makubwa ya ukosefu mkubwa wa chakula yanayoikabili nchi yako. Kama unavyojua Tanzania ni nchi maskini na uwezo wetu siyo mkubwa. Lakini tuna methali hapa isemayo kutoa ni moyo siyo utajiri. Kwa hiyo kwa moyo huo wa mtu maskini, tumeamua kutoa mchango wetu mdogo wa tani 300 za mahindi ambazo ni sawa na magunia 3,000 ili kusaidia ndugu zetu wa Somalia kukabiliana na hali ya njaa kubwa,” Rais Kikwete alimwambia Rais Sheikh Ahmed.

Aliongeza Rais Kikwete: “Tunajua kuwa mahitaji yenu ni makubwa zaidi kuliko hiki kidogo tulichotoa. Lakini sasa ndiyo kwanza tumeingia katika msimu wa mavuno. Tutaangalia huko mbele kama tunaweza kuwachangia zaidi ndugu wetu wa Somalia.”

“Tunazungumza pia na marafiki zetu ili tuwashawishi kuona kama nao wanaweza kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Somalia ya kuhakikisha inapata chakula cha kutosha ili kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi.”

Wakati wa futari ambayo Rais Kikwete alimwandalia Rais huyo wa Somalia katika Mwezi Mtukufu huu wa Ramadhani, Rais Kikwete alitoa mwito kwa kampuni zinazotengeza maji nchini kusaidia kuchangia upatikanaji wa maji kwa wananchi hao wa Somalia. Somalia inahitaji mamilioni ya lita za maji ili kukabiliana na ukosefu mkubwa wa chakula na maji.

“Tutazungumza na kampuni zinazotengeneza maji hapa nchini kama nazo zinaweza kuchangia kupambana na janga hili kubwa linalowakabili wananchi wa Somalia,” Rais Kikwete alimwambia Rais wa Somalia katika shughuli ya futari.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi nchini, mawaziri, makatibu wakuu na maofisa waandamizi wa Serikali na mawaziri wakuu wa zamani, Mzee Salim Ahmed Salim na Mzee Joseph Warioba.

Katika mazungumzo hayo rasmi, Tanzania na Somalia, zimezungumza masuala mengi ambako nchi hizo zinaweza kushirikiana kuisaidia Somalia baada ya ujumbe wa nchi hiyo kuelezea maeneo ambako Tanzania inaweza kuisaidia Somalia kama katika mapambano ya pamoja dhidi ya ugaidi katika Bahari ya Hindi na kusaidia kufundisha wataalamu wa fani mbalimbali.

Rais Kikwete pia alimpongeza Rais wa Somalia na ujumbe wake wa mafanikio ya kijeshi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha El-Shabaab ambacho kimefukuzwa katika maeneo mengi ya Mji Mkuu wa Mogadishu ambacho kimekuwa kinayashikilia kwa muda mrefu.

Rais pia alimpongeza Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed kwa mafanikio yake mengine ya kuleta utulivu zaidi ndani ya Serikali yake na kuongeza muda wa utumishi wa Serikali na Bunge kama moja ya njia ya kuleta maelewano ndani ya Serikali, na kati ya Serikali na Bunge la nchi hiyo.

Rais Ahmed ambayo aliwasili nchini juzi na asubuhi, aliondoka nchini jana baada ya kuwa kukutana na kuzungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kilimanjanro Hyatt Regency mjini Dar es Salaam.


Chanzo: Tanzania kusaidia tani 300 za mahindi Somalia
 
Tanzania pledges 300 tonnes of maize for Somalia famine. Africans for Africa - lets maintain the momentum!

http://www.timeslive.co.za/africa/2011/08/10/tanzania-donates-food-for-somalia
 
Hii sasa ni kumpenda jirani yako zaidi ya nafsi yako! Jamani mbona kuna watz kibao hawana chakula na kila siku media zinatangaza na serikali imelala tu! Jamani huyo waziri wa chakula anafikiri kwa kutumia nini?
 
kiyasi wapewe,msaada wengien mashemeji zetu wengine mawifi wengine ndioooo kama vile kwenye ccm wapo wengine wanamiliki miradi basi ilimradi mambo juu ya mambo,istoshe pia wapewe manake kwakeli hali yao wanastahil kusaidiwa .
 
Tanzania kutoa tani 300 za chakula kusaidia SOMALIA wakati wananchi wake wa MANYONI MASHARIKI wanakula PUMBA, JE hii nikujiosha mbele ya mataifa mengine ili kuonekana Tuna huruma? Chakushangaza mheshimiwa wa JIMBO HILI hajawahi kulizungumzia, naomben mtoe mawazo yenu tunaenda wapi na serikali hii?.
 
Back
Top Bottom