Tanzania yapaa kijeshi Duniani

Tanzania yapaa kijeshi Duniani

Hakuna nchi isiyokuwa na SWAT isipokuwa inategemeana na terminology inayotumika ktk nchi. Huo ni mkusanyiko wa wataalam wa polisi wenye mafunzo ya kijeshi na silaha. Na inaweza pia kuundwa na watalaam mbalimbali kutoka ktk vyombo vya ulinzi na usalama.

Nimekusoma,
Bado kwa tz ukizungatia silaha tunazotumia ni duni (ak47) ukilinganisha na vikosi vya nchi jiran kama kenya wanavikosi maalumu kama vile vilivyoenda westgate na kuokoa watu kabla ya jeshi la kenya kuingilia na kuharibu.

Vikosi ndo mfano wa swat wako trained , well equiped with combat gears , bullet proof, doors explosives.
Wamepata mafunzo israel na usa.

Hao wataalamu unaowasema ww ni wale wa maofisin tu na wanasubiri matamasha tu.
 
Tatizo watanzani tumezoea kusikia vitu Negative tu na hii ni dalili ya kutokujiamini na kudharau taifa letu...kama unadharau taifa lako ambalo ndio utambulisho wako nje ya mipaka unazani kauna mtu atakuheshimu wewe...!ndio mana hata kanchi kama Rwanda nako kanajitutumua mbele yetu kwasababu wanajua raia waliowengi watanzania hawajui thamani yao na wanajizaru...TUBADILIKE JAMANI

Its true kunamaeneo mengi hayapo sawa but some times let us proud our self to beTanzanian.
''UKITAKA KUSHUKURU ANGALIA WALIOCHINI NA UKITAKA KUOMBA ANGALIA WALIO JUU''
 
Jamani ongeeni yote,haters pondeni lakini Tanzania ni nzuri kijeshi Afrika na hata kidunia. Msioamini na mpo Dar naomba piteni pale Sabasaba banda la JWTZ mkapewe taarifa nyingi za jeshi letu. Mtapewa pia taarifa za hizo SPECIAL FORCES. Humu wengi mtaleta u shabiki na hata data hamna!

Sindo hapo mkuu mtu anabisha ukimwambia atetee hoja yake hawezi anajifanya anajuaa mambo yakijeshi kumbe kayajulia kwa msaada wa movie zakijajusi kama 24!!
 
Tofauti na wengi wanavyojua,tanzania imeanza kutajwa na mitandao mbalimbali kati ya vikosi 35 bora zaidi duniani kwa vifaa bora,mafunzo sahihi na uwezo wa kupigana kwenye mazingira yoyote,dunia imeshangazwa na ufanisi wa JWTZ Kongo kwani chini ya kapeti Rwanda haikukubali kirahisi m23 kushindwa,na ni nchi pekee kutoka Africa huku Asia ikitoa nchi kadhaa,sasa Tanzania inawekwa level moja na seal ya USA,special force ya Israel na wakali wengine.

=============
I know we are good, but are we that good?
Halafu hata China hawamo?
I doubt the report!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Majeshi Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa majeshi bora duniani.

Chini ya kichwa cha habari “35 Most Badass Elite Fighting Units from Around the World” mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa.

Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi wa kila kikundi.

Vikosi vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji la Marekani, SAS cha Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni zisizoweza kuingiliwa na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya Ireland.

Vingine ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha JTF2 cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS, Majeshi Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian Joint Response Unit cha Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando Marine, Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces Special Command na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.

Vingine ni Kikosi cha US Army Special Forces Sniper with Remington Modular Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum ya Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi cha KSK cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi Maalum ya Israel – Shayetet 13, Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz, Majeshi Maalum ya Austria – Jagdkommando, Majeshi Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya Peru.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
3 Julai, 2014


Huyo mwandishi Micky Wren ndiyo nani? Mbona niki google jina lake hata picha mtandaoni hana?
 
Huyo mwandishi Micky Wren ndiyo nani? Mbona niki google jina lake hata picha mtandaoni hana?

Wameitunga wahuni tu.. Huyo mwandishi ana dem wa kitz ndio maana kaivhomek tz.,egypt? South africa, yani izo spesho forces zinazidi za sauz na misri? Msituchefue hapa huyo mwandishi katumia vigezo gani
 
sf27.jpg


Kwa upande wa vifaa nadhani bado tuko nyuma ukilinganisha na hayo majeshi mengine
 
Wewe andika kibantu! Unakanganya maneno ka umekunywa taptap!

Nyie ndo vibaka mnaoletewa mabomu ya magendo mkawauzia watu ka nyanya.
Matokeo yake mtu akigombana na mkewe tu anamtupia.

Huko Arusha naskia mna wateja wengi sana.
Siku tukimtia mkononi huyo shemeji yako afande matonyonso atanyea mkononi.

Njaa yenu inaumiza wengi sana.

Wewe weka comment yako hapa. Hujaelewa,kujoa ukalale. Hunijui kuniongelea mimi.


The king.
 
hujasikiliza vizuri kama kweli wamesema hivyo wamekudanganya ukitaka kupata ukweli ingia google hata katika nchi bora 10 zenye jeshi zuri africa haimo mkuu.

Tatizo hujaelewa, wamesema sio jeshi bora bali kikosi maalumu chenye kufanya kazi kiufanisi. Hivyo katika jeshi zima Kuna vikosi kazi maalumu kwa shughuli maalum...
 
Mijadala ya namna hii imekuwa maarifu saana hapa JF. Sio vizuri kushabikia vita; tunamzidi nani anatuzidi nani si mijadala mizuri. Sisi tujitahidi kulinda nchi yetu dhidi ya maadui wa nje na wa ndani.
 
Unajiita Mussolin, hata genesis ya jina lako hujui, hii ni kejeli au dhambi? Kwa sababu babu yako hakuwepo ndo unakejeli wa tz wanaokufanya ulale. Miaka ijayo hata km si mtoto wako lazima mmoja wa ukoo wako atakuwemo usihofu.

punguza viroba
 
Matege,kwann huamin?mpaka wakutie bakora useme wako vizur?historia inalibeba jeshi letu

napata shida kwa sababu wanajeshi kutoka Tanzania ndo wanaongoza kwa kuuwawa huko nje.. ubora wetu uko wapi..??
 
Back
Top Bottom