Tanzania yaonya kusambaratika EAC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yaonya kusambaratika EAC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 18, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,790
  Likes Received: 83,167
  Trophy Points: 280
  Tanzania yaonya kusambaratika EAC
  Mwandishi Wetu, Zanzibar
  Daily News; Wednesday,December 17, 2008 @21:15

  Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iko hatarini kusambaratika kama ilivyotokea mwaka 1977, ikiwa baadhi ya nchi wanachama zitaendekeza unafiki na ubinafsi katika Jumuiya hiyo, Tanzania imeonya.

  “Hatuwezi kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ubinafsi, unafiki tukiendekeza mambo hayo na lile la ukabila, Jumuiya itavunjika kwani mambo hayo hayajengi, tutaibomoa EAC,” ameonya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk. Diodorus Kamala.

  Alikuwa akifungua mkutano wa siku moja hapa jana ulioandaliwa na wananchi wa Wilaya ya Mjini Unguja kuhusu mchakato wa kuwa na soko la pamoja. Alisema tatizo la ujanja ujanja na ubinafsi linaloonekana kuweka mizizi katika jumuiya hiyo, litaipeleka pabaya ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa kulikomesha.

  Alisema Tanzania imejitolea kutoa elimu ya bure kwa nchi nyingine za EAC namna ya kupiga vita ukabila. Alisema tangu kuundwa kwa jumuiya hiyo, kero nyingi zimeongezeka ikiwamo vikwazo vya kibiashara vikiwasumbua wananchi kwani bado kuna vikwazo visivyo kuwa vya kodi vinawekwa na baadhi ya mataifa wanachama.

  “Ukiniuliza tumefaidika nini nitakujibu kuwa badala ya mategemeo ya kupungua na kuondoka kabisa, ndio kwanza vikwazo vimeongezeka,” alisema na kuzitaka nchi hizo kuacha unafiki na ujanja ujanja kwani hakusaidii kuimarisha EAC.

  Alisema mtindo wa baadhi ya nchi za EAC kukataa bidhaa fulani kuingia katika nchi nyingine ni mambo yatakayosababisha kuyumba na kulegalega kwa jumuiya hiyo ambayo imeundwa tena baada ya ile ya zamani kuvunjika mwaka 1977.

  Alitoa mfano wa nyama ya Tanzania inayopelekwa na wafanyabiashara kutoka Simbawanga kuwekewa vikwazo Kenya; maziwa yanayozalishwa mkoani Mara pamoja na magari ya mizigo kukataliwa kufanya kazi katika nchi mojawapo (hakuitaja), ni mambo ambayo hayaonyeshi nia njema katika ushirikiano huo ambao awali ulivunjika kwa mambo ya kutokuaminiana mwaka 1977.

  Alisema kutokana na kutokuwapo kwa dhamira njema na ubinafsi wa nchi wanachama wamediriki hata kudai nafasi za ajira kama za uhudumu, udereva na ulinzi kwa zile taasisi za jumuiya zinazokuwapo katika nchi mojawapo, jambo alilosema ni kinyume cha mkataba wa kuanzishwa kwa EAC.

  Alikanusha na kuwakemea wanaodai Tanzania inachelewesha Soko la Pamoja, na kusisitiza kuwa msimamo wa nchi utaendelea kubaki ule ule katika mambo matatu; ardhi kubakia mikononi mwa Watanzania; matumizi ya pasi za kusafiria yabakie kama yalivyo pamoja na kupinga kuwapo kwa ukazi wa kudumu.
   
 2. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Keep it up Dk. Diodorus Kamala!!!!!!!!!!!!
   
 3. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2008
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Dk. Diodorus Kamala, Ni vema umetoa onyo hili, lakini kwa mtazamo wangu, ingefaa uwasemee wahusika huko huko waliko usoni mwao ili wajue sisi hatutaki mchezo maana tayari tumekwisha athirika na jumuia hii iliyovunjika mwaka 1977. Mpaka sasa wastaafu wetu bado wanapigwa virungu na kuswekwa kwenye kalandikas kwa kudai mafao yao. Ya nini kuhalakisha kujiunga wakati bado hatujayatatua matatizo yaliyopita, Bado hatujajua umuhimu wa kujiunga tofauti tu na kwamba wa Musoma na Tarime watapata free entry wakti wakipitia huko kukwepa adha ya usafiri kwa kanda ya kati?

  Kamala, wafanya kazi nzuri lakini usiwe mnafiki, nenda kawasee wahusika nyumbani kwao...
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Lakini vitu vingine sisi wa tanzania tunapenda kuwalaumu wenzetu wakati tatizo ni letu , tunawekeza sana kwenye siasa na urasimu badala ya kuwekeza kwenye vitu vya msingi, matokeo yake tutaendelea kuwa wanyonge kiuchumi, ambayo baadae itatu sababisha tuwe wanyonge kisiasa kama ilivyo tokea kwa urusi. Na pia linganisha na China walio amua kufanya economic reform, wakati urusi walianza na Political reform.
  Mfano ni kuuza kiwanda cha maziwa cha Northern creamers kwa mtu asiye na uwezo au mwenye kutaka faida ya haraka then tunawalaumu wakenya kwa kutufanya collection point. Viwanda vya Sukari kupewa watu kwa urafiki au ukaribu na viongozi wakati in reality hawa wezi kazi, hiyo ardi tuna ingangania ni vizuri , lakini serekali iwasaidie wananchi waweze kuzalisha vya kutosha na ku-add value on that land, kwa mfano serekali kuwa na sheria kali kuhusu kuhodhi na matumizi ya hiyo ardhi, kuwapa nyenzo kama ni hayo matrekta madogo au plua, kuwekeza katika malambo kusaidia kilimo, feeder roads na umeme huko vijijini, sio watu wanapoteza 90% ya muda wa uzalishaji kutafuta kuni na maji. relwe tuna mpa rafiki yetu ili faida yote tuipate sisi wakati quality ni poor, kwa hiyo utaona vitu vingi tuchukulia vinakuja bila kuji bidisha na kuwa wabunifu, kwa maneno mengine tatizo ni serekali yetu au viongozi wetu
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...nilifikiri hii federation ilishakufa kabla haijaanza,kila mtu anafikiria yeye ni muhimu kuliko mwenzake na bila yeye hakuna federation,ife tuu tuendelee kuchapana kodi kisawasawa!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,790
  Likes Received: 83,167
  Trophy Points: 280
  Koba, tumewashtukia hawa majamaa wanajifanya kutaka federation kumbe nia yao kubwa ni kunyakua ardhi yetu!! Waache waende zao wasije kutuletea matatizo yao ya kikabila nchini mwetu. Tayari tuna matatizo yetu makubwa yanayosababishwa na mafisadi.
   
 7. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hii sasa imekuwa ni issue between Tanzania na Kenya.
   
 8. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  mtu inabidi ajiulize wakati mwingine, kwa nini kelele nyingi dhidi ya Tz zinapigwa na Kenya tu? yeye ni polisi wa EAC? Je hakuna mahali pa kupeleka malalamiko yao?

  Juzi Rwanda imesema inabidi iwaulize watu wake kama wanataka federation, Kenya imelalamika kuwa hakuna umuhimu, kwa kuwa hawakusema hili kabla ya kuingia EAC, why lakini?

  Kenya kwa muda mrefu ilikuwa inachochea wafanyabiashara Tanzania waibane serikali irudi COMESA toka SADC, baada ya kuona mbinu zote zinashindwa sasa wanalazimisha kila kitu kikubaliwe na Tz katika EAC...nadhani ni kama vile baadhi ya waKenya wanaiona Tz kama extension ya nchi yao sasa.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nilisema tangu mwanzo Kenya ina ajenda ya siri na EAC,nia na madhumuni ya kutaka shirikisho haraka haraka ni ardhi na kutaka kuendelea kuifanya Tanzania soko la bidhaa zao.Tanzania sasa tunazalisha bidhaa za plastic,mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine nyingi ambazo siku za nyuma tulikuwa tukiagiza kutoka Kenya,mwaka 2010 Tanzania itakuwa na kiwanda kikubwa A. Mashariki cha kusindika matunda hii maana yake ni kufa kwa kiwanda cha kusindika matunda huko Kenya kwasababu wanategemea kupata matunda ghafi kutoka Tanzania.

  Ajenda ya kutaka free movement na ukaazi wa kudumu nao pia unalenga kunyakua ajira na kuendelea kutumia vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania kama mbuga ya wanyama ya Serengeti,mlima Kilimanjaro,Ngorongoro kuwa ni vyao .Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya utalii kwasababu ya kuwa na vivutio vingi kuliko nchi yoyote ya afrika mashariki.Kenya ina mbuga chache sana tena zina msongamano mkubwa {25 per km}ukilinganisha na Tanzania.Wakenya walikuwa wanawadanganya watalii kwa muda mrefu sana kwamba Kilimanjaro uko Kenya,uongo wao umeshagundulika sasa wanakuja kwa mlongo wa shirikisho !!!!!!!!!!!!!!!!!.

  Mheshimiwa D Kamala tuko nyuma yako,waambie hii si ile Tanzania ya mwaka 1977.
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mimi nashangaa sana Koba, sioni umuhimu wa kuwa na Jumuiya ambayo haina faida yake, ukiangalia kwa makini other EAC members wao wanaitamani Tanzania ili kujineemesha tu.

  Ni heri kujitoa mapema tukabaki na SADC na kama yenyewe hailipi tubaki kivyetu-vyetu. Kwani kujiunga ni lazima? Tatizo letu ni kuigaiga tu- fulani wameungana basi nasi tuungane. Kama huu Muungano wtu wa Tanganayika na Zanzibar tu haujakaa sawa hadi sasa pamaoja na miaka yake 40 tena Wazanzibari wengi ni wahamiaji toka Bara (Juzi nimeskia ripota wa TBC kutoka Pemba akiongea kiswahili cha Kipemba lakini jina lake Masanja!) lakin matatizo bado lukuki ya nini kujepeleka kwenye matatizo ya Wakenya, Waganda, Warundi na Wanyarwanda?
   
 11. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  HONGERA DR.Diodorus Kamala.

  Watanzania Tusimame imara.

  Waache hao Mau Mau na Mungiki watape tape
   
 12. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kwani ni lazima hatutaki kwa sababu watanzania tumeamka. Kilichowafanya wao kuuvunja 77 nini na hata sisi tushindwe sasa. Tena sisi ni wajanja tangu zamani why tu-invest halafu tuje gombana? Hatutaki tena hasara. We keenly foresee economic burden potentials kama hii bloody EAC. Keep it up Tanzanians!

  Hell them Kenyans for yelling at our land that GOd gave us.

  There is a saying that goes "You can not eat all your cake and have it" Kenyans want to prove this saying wrong. Ahahaaaaaaa!
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Tamko la waziri Kamala juu ya EAC ni zuri, lakini tamko hilo ilibidi ilibidi litolewe kwa wahusika moja kwa moja kuliko kutoa tamko hilo mahali pengine kama alivyofanya.

  Kenya ina agenda ya Siri ya kutaka kutufanya msukule ndani ya EAC.

  Kama inawezekana mazungumzo yaendelee muungano uanze 2025-2030.
  Wakati huo hata mimi naweza kuwa mtu mzima pengine waziri au waziri mkuu wa nchi.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kabla ya kuja uongozi wa Dr. Kamala inawezekana kuna mtu aliwaahidi mengi sana hawa wenzetu wa Kenya. Akatusainisha mikataba ya mahotelini bila kujali maslahi ya nchi. Saini zozote zilizowahi kupigwa na huyo mtu kwa niaba ya Jamhuri katika historia ya utumishi wake zingepitiwa upya.

  Nani aliyetufikisha hapa, aliyewaahidi Wakenya ardhi na ajira kabla ya uongozi wa Dr. Kamala ?
   
 15. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli Kuhani
  Hata mimi nimewaza sana, maana inaonekana kama hawa jamaa wamenyang'anywa tonge mdomoni ili hali sie tunaamini hata tonge hatukuwashikisha. Aliyepita alikuwa Mwapachu siyo? Aliwaahidi nini hawa? We need to peruz ze dokuments! Wamekuja na kasi kubwa sana ya matusi na kejeli kuhusu referendamu yetu ya kukataa shirikisho wakati hata wao hawajafanya tulilofanya.
  Tusije tukawa tunapambana kumbe, mheshimiwa aliyepita alikuwa analala kwenye vikao,wao wakafikiri anasema NDIYO
   
 16. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Actually, Mwalimu Zawadi, Bakari Mwapachu hajawaji kupita pale, wala mdogo mtu, Juma, ambae ndie Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwa sasa. Waliopita pale ni mafisadi washutumiwa wawili maarufu, Dr. Msabaha, na your usual suspect the illustrious Mr. V.G. Cent.

  Kwa hiyo Dr. Kamala pale right now all he's been doing all along is really to clean up the mess there. Kina V.G. Cent watakuwa walisha toa toa ahadi nyingi sana kwa Wakenya pale.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi hayo ambayo tunang'ang'ania yana faida gani kwa mtanzania?

  i) Hiyo ardhi ambayo tunadai ni ya kwetu, mara ngapi wananchi wamenyang'anywa na kupewa wawekezaji uchwara (kwa long-term lease) kwa dhana kuwa ardhi ni mali ya umma? Mara ngapi wananchi maeneo yao yamegawiwa kwa wenye nazo, na hao wakalipwa bei ya mafenesi yaliyomo wakati wajanja wa ardhi wanavuta mamilioni?

  ii) Matumizi haya ya pasi si yanawafaidia jamaa wa immigration zaidi ya wananchi wa kawaida? Tangu lini mtu mwenye nazo amaeshindwa kupata pasi ya Tanzania? Nchi zote zenye ushirikiano wa karibu zinalegeza masharti ya matumizi ya pasi. Hii ni kweli kuanzia Nafta hadi E.U. Leo tunataka tubakie na ukiritimba wa pasi halafu tunasema tunataka ushirikiano zaidi?

  iii) Nchi nyingi tu zina mpango wa ukazi wa kudumu. Watanzania wengi tu wamefaidika na hiyo. Ni wangapi walio marekani wamebeba Green Card? Wangapi wako ulaya kama permanent resident? tunaona shida gani kumruhusu mganda, mrundi au mkenya kuja kuishi kwetu ili mradi havunji sheria? Mbona na sisi wengi tu wako Nairobi, Mombasa, Jinja na kwengineko?

  iv) Tulikuwa kwenye Comesa ambamo hivyo vipengele vyote vya biashara viliondolewa au kulegezwa. Usafirishaji wa mizigo ulirahisishwa na mengineyo. Pamoja na faida zote hizi, tukajitoa kwa mbinde tukithamini zaidi ushirikiano wetu na nchi za kusini kwetu. Ushirikiano uliokuwa zaidi wa kisiasa na si wa kiuchumi! Tulibembelezwa tubaki, hatukuta kusikia. Sasa leo tunalalamikia nini?

  Hapana, kwenye hili sisi ni kikwazo. Hatuwezi kusema sisi kwenye hizi ishu hatugeuki halafu tukajidai ati tunataka maelewano! Bora tuwaambie wenzetu kuwa huo Muungano wanaoutaka sisi hatuna mpango nao. Tutafute njia mbadala ya kushirikiana nao bila kuwa sehemu ya huo ushirika. Lakini tutakaoumia ni sisi na si wao kama tunavyojidanganya!

  Mtoto akililia wembe, mpe. Kama ilivyokuwa Comesa, hivyo hivyo itakuwa kwenye EAC. Ingawa safari hii ni wenzetu watachoka kutuvumilia na kutuacha sisi tukumbatie visivyo na faida.

  Amandla.....
   
 18. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Fundi,

  hivi kweli kama unaona hayana faida kwa Mtanzania, kwa kufuata vigezo ulivyoainisha hapo juu, ndiyo ziwe sababu za kukubali protocal ya EAC kama ilivyo sasa?

  Hiyo idadi ya Watanzania unaosema wanaishi huko unakotaja, je ni wangapi na wanamiliki ardhi kwa kiwango gani? Hujui hata sasa kuna wageni kibao wanaishi hapa kama Watanzania wanavyoishi kwao, bila kujali kuwa kuna protocal au hakuna?

  Ni watanzania wangapi wataenda kumiliki ardhi Kenya? Ipo kiasi gani kule?
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  1. Kama hizi ndiyo sababu pekee tunazozitoa kupinga hii protocal basi kwa mtazamo wangu hazitoshi. Kwa hiyo tukubali hiyo protocal.

  2. Kama mtu una uhalali wa kuishi mahali kwa nini ukatazwe kumiliki ardhi? Mbona humu humu kwenye jamvi tunataja viongozi wetu ( Balali, Mgonja etc etc) kwa mfano wanaomiliki nyumba marekani wakati wao wanaishi Tanzania?

  3. Hao wageni kibao unaowataja wanaishi kwa wasiwasi na kujificha. Ikiweko hiyo protocal itaondoa uoga huo na kuwaruhusu wao nao waishi kama wanavyoishi raia wa nchi husika. Mbona hatujiulizi ni watanzania wangapi wanaoishi katika nchi jirani?

  4. Kama wanauwezo wakununua hiyo ardhi kwa bei ambayo wenye nayo wanataka, hamna kitakachowazuia watanzania kumiliki ardhi Kenya, Uganda, Rwanda au Burundi. Kama wanataka. Na vile vile kwa hao tunaowaita wageni wakitaka kumiliki ardhi Tanzania nao ni lazima wafuate sheria. Wanunue kwa mwenye ardhi kwa bei anayoitaka n.k. Mbona pamoja na hii chimera ya kumiliki ardhi waswahili wote wameuza ardhi yao Kariakoo na Ilala? Ninachopinga ni kile kilichotokea maeneo ya Msasani, ambapo wavuvi waliokuwa wanakaa maeneo hayo waliondolewa, wakalipwa fidia kiduchu, viwanja vikakatwa na wajanja wakaviuza kwa mamilioni. Si heri wale wavuvi wangekuwa wanavimiliki na hivyo kuwapa haki ya wao wenyewe kuwauzia wanaovitaka? Sasa leo viwanja vyenye thamani ya mamia ya mamilioni, mtu analipa pango ya vilaki! Si heri ingejulikana kuwa ile ardhi ni asset yake na angelipa kodi based kwenye value ya ile ardhi?

  5. Hili suala ni kama lile la dual citizenship. Tunatanguliza emotion badala ya kuangalia hali halisi.

  Kweli leo baada ya miaka zaidi ya arobaini ya uhuru wetu hatuoni aibu kusema tunawahofia masikini wenzetu wakenya? Hivi karibuni tutawaongeza warundi, waganda na watu wa msumbiji kwenye orodha hiyo! Huu uoga wetu ndiyo unaotubakiza hapa tulipo.

  Ni hayo, tuu.

  Amandla.....
   
 20. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Fundi, Awethu!

  Sasa, unadhani kwa nini federation haiwezi kuwa federation hadi ardhi ya Tanzania ipatikane? Si Wakenya tu wanaoonekana kwenye hii issue, ni other members as well, lakini wanatajwa sana kwa kuwa wao pia ndiyo sasa wanajiona kama polisi wa EAC. wao wana specific ambitions ambazo lazima zipatikane Tanzania, pengine kuliko mataifa mengine...ndiyo maana sasa vita ni kama ya Tz na Kenya tu.

  Kama wajanja ndiyo waliowadhulumu ardhi watu wa msasani, sasa iweje tuamue tu, kuitoa kwa wengine badala ya kuondoa udhaifu uliopo ili watu wafaidike na ardhi yao?

  Kumbuka pia kwamba sheria za umilikaji ardhi katika nchi hizi zinatofauti sana. Kwa hela mbuzi niliyonayo, na kwa kabila langu, siwezi kununua ardhi Kenya hata siku moja. Lakini nitaweza kununua huko kwetu, hata kama ni kweli kuna wakati nitaingiwa na tamaa au kughiribiwa na wajanja, lakini hiyo itakuwa udhaifu wangu, si mfumo, unaonaje?
   
Loading...