Tanzania yaonya kusambaratika EAC

EAC hiki ni kini macho kwani hawa wakenya wanataka watufanye sio ngazi, kwa maoni yangu mie naona haina haja kabisa ya kuendelea na huu mchakato wa EAC hebu tujaribu kitu kingine maana hii ilishatushinda tangu 77.
 
Fundi et al heshima zenu

I have to confess. Ni pro Unity wa Africa. NAAMINI KABISA KWAMBA FOR AFRICA TO MOVE FORWARD WE REALLY NEED TO PUT OUR ACTS TOGETHER. HIVYO BASI KWANGU MIMI SWALA LA EAC NALISUPPORT SANA, MAANA NAAMINI WE HAVE ALOT TO GAIN THAN TO LOSE.

Lakini baada ya kufuatilia mjadala wa EAC kwa ukaribu sana baina ya baadhi ya wakenya na watanzania (humu, Michuzi nk). Utagundua mambo kadhaa ambayo yatakufanya upumue mara mbili kabla ya kuongea. What I have realized ni kwamba kuna MISTRUST KUBWA SANA baina ya WAKENYA NA WATANZANIA. Na hii mistrust haikuanza leo wala juzi ni historical something which needs its own thread. Na you cant build a federation katika mazingira kama haya. No way.

Ukweli si kwamba Tanzania inawaogopa wakenya kwamba watachukua kazi zao..Reality check ni kwamba no body trust another. Watanzania tunawaangalia wakenya kama wabinafsi, wakabila, wanaopenda umimi sana. Wakati wakenya wanatuangalia hivyo hivo na kibaya zaidi hii mentality ya kwamba wakenya wamesoma na wanajua kiingereza kuliko wengine na quest yao ya kuwa power house ya East Africa at the expense ya TZ na Uganda..Its not something appreciated by the majority. indeed no country would love that.

Fundi na Masanja ambao ni progressive tunaweza tukasema kwamba hizo ni cheap politics, tukarefer NAFTA, EU NK lakini ukweli ni kwamba Kwa sasa Kenya na TZ wako different miles apart though walking in the same direction. Hapa umoja ni kudanganyana na if you dont trust me....hata tukiungana leo...mwisho wa hiyo ndoa utakuwa mbaya kuliko wa 1977.

Kwa nini ardhi imekuwa issue? Ukifuatilia kwa makini..Kenya ardhi inamilikiwa na wenye uwezo..(mfano Familia ya Njonjo inamiliki nadhani nusu ya wilaya kule Nanyuki). NA within Kenya itself bado kuna stratification ya makabila ukianza na wakikuyu na wajaluo nk..wao kwa wao wanadharauriana na opportunities zinaenda kwa wale wanaotoka kwenye correct tribes. Tanzania on the other hand we have our tons of problems lakini bado hata mtoto wa mkulima Masanja au Fundi anaweza akahangaika akasonga mbele bila kuhujumiwa kwa kutumia kabila lake. Upo hapo?

Fundi, hizi kwako wewe kama msomi au Mbalammwezi au Kuhani ni minor issues..Lakini kumbuka kwamba hizi ndo issues ambazo zimetufanya Africa tustagnate hapa tulipo. Politics za ukabila na ubinafsi. From Chad kwa ndugu yetu Derby na wazaghawa, Kibaki na Wakikuyu, Mseveni na Wahima/Wanyankole, Rwanda na Watusi..the list is endless.

So do I endorse the approach of Tanzania? Probably Yes and No. I advocate for gradual unification wa nchi zetu na tuache hizi sensitive issues kama Ardhi na ukaazi wa kudumu pending kwanza..tuone how the union in other areas will fair. Honestly tukiingia hivi hivi tutajikuta tunaunda jumuiya ya uadui na mistrust. By the way leo sisi tuna muungano na Zanzibar..we all know the story of the "current state of our Union".

It will be erroneous kwa kaka yangu Fundi kulinganisha matatizo ya msasani ya wavuvi na matatizo ya cross boarder...Ardhi ndo silaha ya mwisho ya proletariats wetu ambao ni 80%. SANA SANA utawafanya hawa jamaa wawe wapagazi/manamba kwenye mashamba/real estate za wakubwa. Its not something simple. We need reasoning and long term plans.

Angalia nchi nyingi za kiafrika zilizowahi kuungana..SENEGAMBIA etc...Mistrust ndo tatizo kubwa..na bila kuiondoa hiyo..we cant go anywhere. So is EAC..there is a very big concern ya kutoaminiana. Na kwa hilo..twende taratibu. Fundi, I say it again, we need unity, lakini lazima tujifunze kutokana na makosa. What went wrong with our first attempts? Kwa nini Watanzania hawataki? Kwa nini wakenya wanautaka? EU tunayoisema hivi leo..imeanza miaka zaidi ya hamsini iliyopita..lakini we still see how "hobbled" it is, decision making ilivyongumu. Juzi Constitution yao imepigwa chini na wa-Irish tuu...Ni complex affair.

Na hapa ndo nadhani wasomi wetu akina Fundi, Pundit, Kuhani, Kichuguu, Mchungaji nk.. ingebidi mfanye critical thinking kuangalia hii jumuiya na matatizo yake in the future. Waswahili walisema..Chelewa ufike...Perhaps hata watanzania tunaweza tukachelewa lakini tukafika.

Masanja,
 
Mlipoaunganisha Tanganyika na Zanzibar mlitaka kufuta mpaka- ule Zanzibar channel. Na mmefanikiwa hivyo . Hongereni. Sasa na wenzenu nao wanataka kufuta mipaka kule Horo horo na kwengineko. Hee Kuweni macho wa-Tanganyika.
 
Kabla ya kuja uongozi wa Dr. Kamala inawezekana kuna mtu aliwaahidi mengi sana hawa wenzetu wa Kenya. Akatusainisha mikataba ya mahotelini bila kujali maslahi ya nchi. Saini zozote zilizowahi kupigwa na huyo mtu kwa niaba ya Jamhuri katika historia ya utumishi wake zingepitiwa upya.

Nani aliyetufikisha hapa, aliyewaahidi Wakenya ardhi na ajira kabla ya uongozi wa Dr. Kamala ?
He-hee. Hivyo nido vimbwanga vya kuungana. sasa pale Wa-zenj wanapolalamika usiwaone mafala kwani nao pia hulalamikia ardhi yao, ajira zao, kodi zao, na vikorombwezo vingi tu vinavyoambatana na hayo unayolalamikia wewe hivi sasa, na una hofu kuwa Wakenya wanayataka.
 
napenda kurudia tena matatizo mengine ni ya kwetu, eg hatufanyi juhudi za kweli kujikomboa ki-uchumi, sana sana viongozi wetu wanataka kutumia hizo opportunity, ili wawe ndio wafalme wetu kiutawala na ki-rasilimali, odinga/kibaki design,mfano mfumo wa elimu bado uko duni, hivyo, nafasi za kazi zitakwenda kwa wenzetu. solution tuwekeze kikwelikweli ili tuweze kujilinda. ardhi yetu kubwa hatuitumi, solution wekaza hata miti ya kupanda tu ili uilinde from the intruder, bila hivyo tutashindwa tu.
mfano halisi sehemu kubwa ya ardhi karibu ya kia ilikuwa reserved land kwa ajili ya wafugaji, na labda kuna sehemu zingine ambazo sizijui, lakini sababu ya kuhama hama kwa hao wamasai/wafugaji, leo hii ile ardhi si yao tena. sasa kwa hapa hawa wafugaji wange fundishwa kulima majani na kuya hifadhi leo hii ile ardhi ingekuwa yao, kwa hiyo kuwa sema wakenya/waganda na watusi licha ya ubaya wao tutakuwa tuna kimbia kivuli chetu wenyewe, nacho ni kutokuwa na viongozi wenye fikra za maendeleo, wenye ubinafsi wa kufikiria ni jinsi gani atafaidika na uamuzi atakao fanya.
 
Hapa ndipo JKN anapo hitajika sana sana maana hawa angalliwaeleza kule kule kwao Kisumu na wakabaki kucheka yeye ana malizia hotuba .EAC kama haina manufaa kwa Taifa hili basi waachie wao waendelee .
 
“Hatuwezi kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ubinafsi, unafiki tukiendekeza mambo hayo na lile la ukabila, Jumuiya itavunjika kwani mambo hayo hayajengi, tutaibomoa EAC,” ameonya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk. Diodorus Kamala.

Impressive but still this guy sounds like "educated demagogue"....

Lets wait and see

Tanzanianjema
 
Hivi hayo ambayo tunang'ang'ania yana faida gani kwa mtanzania?

i) Hiyo ardhi ambayo tunadai ni ya kwetu, mara ngapi wananchi wamenyang'anywa na kupewa wawekezaji uchwara (kwa long-term lease) kwa dhana kuwa ardhi ni mali ya umma? Mara ngapi wananchi maeneo yao yamegawiwa kwa wenye nazo, na hao wakalipwa bei ya mafenesi yaliyomo wakati wajanja wa ardhi wanavuta mamilioni?

ii) Matumizi haya ya pasi si yanawafaidia jamaa wa immigration zaidi ya wananchi wa kawaida? Tangu lini mtu mwenye nazo amaeshindwa kupata pasi ya Tanzania? Nchi zote zenye ushirikiano wa karibu zinalegeza masharti ya matumizi ya pasi. Hii ni kweli kuanzia Nafta hadi E.U. Leo tunataka tubakie na ukiritimba wa pasi halafu tunasema tunataka ushirikiano zaidi?

iii) Nchi nyingi tu zina mpango wa ukazi wa kudumu. Watanzania wengi tu wamefaidika na hiyo. Ni wangapi walio marekani wamebeba Green Card? Wangapi wako ulaya kama permanent resident? tunaona shida gani kumruhusu mganda, mrundi au mkenya kuja kuishi kwetu ili mradi havunji sheria? Mbona na sisi wengi tu wako Nairobi, Mombasa, Jinja na kwengineko?

iv) Tulikuwa kwenye Comesa ambamo hivyo vipengele vyote vya biashara viliondolewa au kulegezwa. Usafirishaji wa mizigo ulirahisishwa na mengineyo. Pamoja na faida zote hizi, tukajitoa kwa mbinde tukithamini zaidi ushirikiano wetu na nchi za kusini kwetu. Ushirikiano uliokuwa zaidi wa kisiasa na si wa kiuchumi! Tulibembelezwa tubaki, hatukuta kusikia. Sasa leo tunalalamikia nini?

Hapana, kwenye hili sisi ni kikwazo. Hatuwezi kusema sisi kwenye hizi ishu hatugeuki halafu tukajidai ati tunataka maelewano! Bora tuwaambie wenzetu kuwa huo Muungano wanaoutaka sisi hatuna mpango nao. Tutafute njia mbadala ya kushirikiana nao bila kuwa sehemu ya huo ushirika. Lakini tutakaoumia ni sisi na si wao kama tunavyojidanganya!

Mtoto akililia wembe, mpe. Kama ilivyokuwa Comesa, hivyo hivyo itakuwa kwenye EAC. Ingawa safari hii ni wenzetu watachoka kutuvumilia na kutuacha sisi tukumbatie visivyo na faida.

Amandla.....

Ngawethu!

Kaka Fundi Mchundo, ahsante kutusaidia kuangalia upande wa pili, na kuepuka kwenda na muono wa kuhisia, kusikia, kukisia, na mtima. Lakini binafsi nimeshindwa kushawishika kwamba hapa tutajutia msimamo wetu.

Swala la ardhi, kama wananchi wananyang'anywa maeneo na kupewa wawekezaji uchwara, matajiri, hilo kosa halirekebishiki kwa kuruhusu wengine, Wakenya. Hitilafu ya pili haihalalishi ya kwanza. Hililafu ya kwanza inatokana na ufisadi na pia watu kutokuwa na elimu juu ya haki zao ambazo zinaweza kutafutwa iwapo tutaimarisha misingi ya nguvu za dola. Hitilafu ya pili inaepukika, hatutaki kuwapa Wakenya ardhi kwa sababu wao hawana ya kutupa. Kosa la kuungana katika mazingira ambayo sisi ndio tunabeba mzigo wa kuauni wenzetu tumelifanya mwaka 1964 na tusingependa kulirudia. (Wanzanzibari msitaabishwe hapo, maana hata nyinyi mnazo kero za muungano zinazowasumbua kama sisi, baadhi yetu, tunavyoona kwamba nyinyi kwetu ndio mzigo mzito kama gunia la karafuu. Kama karafuu ina uzito!) Hatutaki kurudia kosa lile lile na Wakenya.

Swala la pasi ilichofanya Tanzania – na ndicho walichokubaliana wote watatu, 1999 – ndio hicho kinafanywa sehemu nyingi duniani, zikiwemo hata hizo jumuiya ulizozitaja Fundi. Kwamba vizingiti bado vipo, na walioviondoa wameenda taratibu mno, na kuna waliojitoa katika makubalioano ndani ya jumuiya. Tanzania inasema tubaki na huu mpango wa kutoa pasi ya EA (ambayo kwa kweli ni kama visa tu, manake yabidi ugongewe tena mihuri kila baada ya miezi sita, haikupi uraia, na inatumika jumuiani tu. Ni visa tu ile.)

Na ndicho wanachofanya wengine. Katika NAFTA, mfano wako, Wakanada na Wamexico wanalazimika kuomba TN (Trade NAFTA) visa status kuingia na kutoka US mpaka kesho. Tena kuipata, inabidi uthibitishe kwamba unaenda kujihushisha na – na una ujuzi na taaluma ya kufanya – moja ya kazi ya kitaalam iliyoorodheshwa katika "TN Visa List of Qualifying Occupations." Huwezi kujiingilia ingilia na kutoka kama unasafirisha magunia ya mazao ya biashara kutoka Singida kwenda Shinyanga.

Ukiondoa vikwazo vya visa, ukaruhusu kuingia na kutoka ovyo ovyo maana yake umehalalisha makazi ya kudumu kwa sababu hakutakuwa na kuulizana. Wamarekani na wengine wenye sheria za makazi ya kudumu wao walihitaji watu. Li-nchi lao kihistoria lilikuwa tupu, lilikuwa kubwa, lilikuwa na maliasili za kumwaga, lilikuwa linatoka udenda wa kutamani nguvukazi na akilikazi za watu wa dunia. Sisi hatuna baraka zote hizo. Hata maji yanatukaukia siku hizi. Ziwa Victoria linakauka, samaki wanapukutika, misitu inapukutika, vijijini wananunua kuni! Kaka Fundi Mchundo nimekwenda kijijini kwetu miaka michache iliyopita nimekuta wanasema kuna wakati wanauziana kuni! Maliasili zinakwisha. Ukihalalisha makazi ya kudumu maana yake itabidi uruhusu wageni wanunue makazi, na nyumba, na ardhi. Hilo tumesema hivi, wao hawana cha kutupa, hatutaki. Mpango wa chetu chao, chao chao hatutaki. Kwanza hawana chao!

Kwa hiyo mpango wa kuondoa vizingiti mipakani ni wa kuuendea taratibu. Hata EU, mfano mwingine ulioutoa, nao ni mwaka jana mwishoni tu ndio wamepitisha azimio la kuondoa vikwazo vya kusafiri iwapo una pasi ya mojawapo ya nchi, Schengen passport. Na bado kuna wengine wameshtuka, wamekataa mpango wa Schengen Passport, wakina Great Britain, Ireland, Romania, Cyprus na wengine. Na sisi huu mpango tuukatae!

Kingine, Comesa hatukujitoa ili tujiunge na wa kusini, sidhani. Hata mwenyewe umesema shirikisho moja ni la kisiasa zaidi ya kiuchumi. Tungeweza kuwatumikia mabwana hawa wote wawili kwa mpigo. Kikubwa kilichotufanya tujitoe Comesa ni tukio la fedheha la sabasaba ya mwaka 2000: Hakukuwa na wafanyabiashara wa kibongo! Tukaona isiwe tabu, hatuko tayari. Heri lawama, tukajitoa. (Source ) Na mpaka sasa hivi hatuna uhakika kama tuko tayari. Juzi waziri Nagu katangaza haturudi Comesa. Maana yake bado hatujaumia kutosha kujitoa. Tukiumia tutatia akili. Lakini inaonekana bado tuko poa. Comesa nayo isubiri.

Lakini pointi yako ya mwisho Fundi Mchundo, nakubaliana na wewe, na nadhani Dar-es-Salaam na Waziri Kamala wanawazugazuga Wakenya na wengine kujifanya tunataka wakati tunaogopa. Anasema EAC ilivunjika kwa unafiki halafu yeye mwenyewe analeta ajizi, dilatory schemes za kwenda kuongelea akiwa Zanzibar. Hapana, tuwe wazi. Tusileteane ajizi, tusiwayeyushe. Tuwaambie usoni:

Hatutaki mpango wa kuondoa vizingiti vya kuingia na kutoka kama kwenye shamba la bibi maana hiyo ni sawa na kuruhusu makazi ya kudumu. Hatutaki mpango wa kuruhusu makazi ya kudumu maana itabidi uwape haki ya kujipatia makazi, na ardhi, ya kudumu. Hatutaki mpango wa kugawa ardhi kama hisani kwa wale ambao hawana cha kutupa kwa sababu sisi sio baba huruma!
 
Fundi et al heshima zenu

I have to confess. Ni pro Unity wa Africa. NAAMINI KABISA KWAMBA FOR AFRICA TO MOVE FORWARD WE REALLY NEED TO PUT OUR ACTS TOGETHER. HIVYO BASI KWANGU MIMI SWALA LA EAC NALISUPPORT SANA, MAANA NAAMINI WE HAVE ALOT TO GAIN THAN TO LOSE.

Lakini baada ya kufuatilia mjadala wa EAC kwa ukaribu sana baina ya baadhi ya wakenya na watanzania (humu, Michuzi nk). Utagundua mambo kadhaa ambayo yatakufanya upumue mara mbili kabla ya kuongea. What I have realized ni kwamba kuna MISTRUST KUBWA SANA baina ya WAKENYA NA WATANZANIA. Na hii mistrust haikuanza leo wala juzi ni historical something which needs its own thread. Na you cant build a federation katika mazingira kama haya. No way.

Ukweli si kwamba Tanzania inawaogopa wakenya kwamba watachukua kazi zao..Reality check ni kwamba no body trust another. Watanzania tunawaangalia wakenya kama wabinafsi, wakabila, wanaopenda umimi sana. Wakati wakenya wanatuangalia hivyo hivo na kibaya zaidi hii mentality ya kwamba wakenya wamesoma na wanajua kiingereza kuliko wengine na quest yao ya kuwa power house ya East Africa at the expense ya TZ na Uganda..Its not something appreciated by the majority. indeed no country would love that.

Fundi na Masanja ambao ni progressive tunaweza tukasema kwamba hizo ni cheap politics, tukarefer NAFTA, EU NK lakini ukweli ni kwamba Kwa sasa Kenya na TZ wako different miles apart though walking in the same direction. Hapa umoja ni kudanganyana na if you dont trust me....hata tukiungana leo...mwisho wa hiyo ndoa utakuwa mbaya kuliko wa 1977.

Kwa nini ardhi imekuwa issue? Ukifuatilia kwa makini..Kenya ardhi inamilikiwa na wenye uwezo..(mfano Familia ya Njonjo inamiliki nadhani nusu ya wilaya kule Nanyuki). NA within Kenya itself bado kuna stratification ya makabila ukianza na wakikuyu na wajaluo nk..wao kwa wao wanadharauriana na opportunities zinaenda kwa wale wanaotoka kwenye correct tribes. Tanzania on the other hand we have our tons of problems lakini bado hata mtoto wa mkulima Masanja au Fundi anaweza akahangaika akasonga mbele bila kuhujumiwa kwa kutumia kabila lake. Upo hapo?

Fundi, hizi kwako wewe kama msomi au Mbalammwezi au Kuhani ni minor issues..Lakini kumbuka kwamba hizi ndo issues ambazo zimetufanya Africa tustagnate hapa tulipo. Politics za ukabila na ubinafsi. From Chad kwa ndugu yetu Derby na wazaghawa, Kibaki na Wakikuyu, Mseveni na Wahima/Wanyankole, Rwanda na Watusi..the list is endless.

So do I endorse the approach of Tanzania? Probably Yes and No. I advocate for gradual unification wa nchi zetu na tuache hizi sensitive issues kama Ardhi na ukaazi wa kudumu pending kwanza..tuone how the union in other areas will fair. Honestly tukiingia hivi hivi tutajikuta tunaunda jumuiya ya uadui na mistrust. By the way leo sisi tuna muungano na Zanzibar..we all know the story of the "current state of our Union".

It will be erroneous kwa kaka yangu Fundi kulinganisha matatizo ya msasani ya wavuvi na matatizo ya cross boarder...Ardhi ndo silaha ya mwisho ya proletariats wetu ambao ni 80%. SANA SANA utawafanya hawa jamaa wawe wapagazi/manamba kwenye mashamba/real estate za wakubwa. Its not something simple. We need reasoning and long term plans.

Angalia nchi nyingi za kiafrika zilizowahi kuungana..SENEGAMBIA etc...Mistrust ndo tatizo kubwa..na bila kuiondoa hiyo..we cant go anywhere. So is EAC..there is a very big concern ya kutoaminiana. Na kwa hilo..twende taratibu. Fundi, I say it again, we need unity, lakini lazima tujifunze kutokana na makosa. What went wrong with our first attempts? Kwa nini Watanzania hawataki? Kwa nini wakenya wanautaka? EU tunayoisema hivi leo..imeanza miaka zaidi ya hamsini iliyopita..lakini we still see how "hobbled" it is, decision making ilivyongumu. Juzi Constitution yao imepigwa chini na wa-Irish tuu...Ni complex affair.

Na hapa ndo nadhani wasomi wetu akina Fundi, Pundit, Kuhani, Kichuguu, Mchungaji nk.. ingebidi mfanye critical thinking kuangalia hii jumuiya na matatizo yake in the future. Waswahili walisema..Chelewa ufike...Perhaps hata watanzania tunaweza tukachelewa lakini tukafika.

Masanja,

Masanja,

Hiyo ya gradual unification nadhani itafanya kazi vyema zaidi kuliko ya kutaka kufanya mambo yote kwa pupa. Kuanza na ushirikiano wa biashara (labda na kodi) na kisha baadaye kuleta mambo mengine zaidi kwenye muungano itakuwa wazo zuri kuliko kufikiria sasa hivi ni nani atakuwa raisi wa kwanza (museveni) au nani atapata jangwa la Dodoma!!?.

Mimi binafsi ningependa sana kuona nchi za kiafrika zikiungana na kujenga taifa kubwa lenye ushirikiano mzuri kiuchumi na kisiasa ila pia hisia na historia ya wananchi wa maeneo haya vinaelekea kuwa kitu cha kuangalia kwanza kabla muungano wowote ule haujawekwa kwenye maandishi (kusainiwa?).

Kinachoumiza zaidi ni kuwa, badala ya kutafuta namna ya kuungana, naona waafrika bado tunavunja nchi zetu. Juzi nimekutana na vijana waethiopia ambao wanataka kuanzisha nchi yao ndani ya Ethiopia - Oromo. Yaani ule utengano ulioitenga jibuti na badae eritrea, unaendelea na sasa Oromo itakuwa nchi yenye bendera yake na raisi wake na kila kitu chake.

Kutoka nchi moja hadi nne ndani ya miaka michache ni muda mfupi sana. Naona watanzania tumeanza kujadili kuvunja muungano. Wakati wa uchaguzi wa Tarime kuna watu waliandika hapa kuwa Tarime itengwe toka Tanzania na kupelekwa Kenya or something like that.... sina hakika hizi hisia zitaisha lini ila naomba kuwa ziishe karibuni kabla hatujakuwa na nchi 127 ndani ya Tanzania (kuna mtu anasema kuwa Tanzania ina makabila 127).

Kazi kwelikweli .... Ninasubiria sana kwa hamu siku ambayo waafrika tutakuwa na bara lililoungana badala ya vinchi vidogovidogo ambavyo hata haviwezi kutoa chakula kwa watoto wa shule (shule ya ufundi moshi imefungwa kwa ukosefu wa chakula).
 
Masanja,Magabe,Kuhani,TZ-Njema,...

..Bakhresa amewekeza Kenya na Uganda.

..Wakenya wa Athi River Cement wanajenga kiwanda cha saruji Tanga.

..kuna Waganda walikuwa hapa wamewekeza kwenye benki.

..sielewi ni "Muungano" gani zaidi tunaoutaka.

NB:

..waliotuburuza mpaka kufikia hapa ni Ben Mkapa na Jakaya Kikwete.

..masuala ya Afrika Mashariki yalikuwa chini ya wizara ya mambo ya nje wakati Kikwete akiwa Waziri na Mkapa Raisi.

..tena Mkapa aliwahi kudai ati tuchupe mbizi tu kujiunga kwenye Jumuiya tutajifunza kuogelea tukiwa ndani ya maji[jumuiya].
 
Back
Top Bottom