Tanzania Yangu Inavyo umizwa

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
NCHI YANGU TANZANIA UNAUMIZWA

Tanzania ni nchi pekee duniani katika Karne ya 21 ambapo kiongozi anaweza kuwahutubia wasomi chuoni akisema "someni kwa bidii Ila mkimaliza mjue mtajiajiri wapi, serikali Haina mpango wa ajira kwa ajili yenu" na akapigiwa makofi hadi maprofesa walioajiriwa wakanyanyuka kwenye viti vyao pwa pwa pwa👏👏👏 makwasa wakiyanyuka kwamba bosi katoa bonge la pointi Yani
Tanzania ya Karne ya 21 ni jamii pekee ambapo kiongozi anayelipwa mshahara mamilioni na kuishi kifahari jijini anaweza kubuni mchango kwa raia na akawaambia atakayeona ni kero ahamie nchi atakayojua yeye na akapigiwa chapuo na baadhi ya wasela wakiona kuwa jamaa ametoa bonge la pointi kinoma.

Chanzo Cha matatizo ya nchi zetu si ukosefu wa fedha Bali ni jinsi tu wanavyofikiri na kutenda
Je, serikali haiwezi kupambana na ukosefu wa ajira ikaachana na dhana potofu ya kuwashauri wanafunzi kutotegemea ajira wakiwa wao tayari wameajiriwa?

Basi inawezekana serikali ipitie hili >>>>> Story of Change - Serikali inavyoweza kupambana na Ukosefu wa Ajira
TAFAKURI JENZI.
 
Back
Top Bottom