Hali halisi ya ajira ya Ualimu Tanzania

Makox

Senior Member
Jan 19, 2014
108
130
KUMBUKUMBU
Ni heri kukumbuka kwa kuwa tunao ubongo, mwezi march 2013 ndipo ilianza safari, ni safari ya Abunuasi ya kusubir kustaafu!

Naacha ndugu zangu, na mali zao za thamaniiii, mashamba na vinyungu nikiwa ni mwenye nguvu.

Siendi tena site kwenye kazi zangu za ujenzi kwa Santona naachana na vyombo vyangu vya ujenzi, kazi niloipenda.

Kiwandani baibai Mhindi Kishor tunaonana.

Ni safari ya Njombe, Lilondo mpaka, Songea naripoti Namtumbo Wilayani.
Nakutana na ndugu zangu wenye sura za huzuni japo ni wasomi.

Kila mtu kituo chake kupangiwa, na mikataba ya kilaghai tunajazishwa.

Daaah hata hatujui tunapelekwa kama mang'ombeee, NHIF, LAPF na wengine PSPF Wanajujazisha mikataba ya makubaliano kwa nguvu bila maelekezo ya kina! sauti zinasikika jazeni haraka tuanze safari.

Njiani kwenda Lusewa, huko karibu na Mozambique japo hakuna boder,
ni kifuku njia mbovu cruiser ya Dreva Chuma inakwama!

Vituo kadhaa tunapita kuwamwaga walimu na kuwatelekeza, hakuna kuagana funga milango tuondoke.
Sauti ya Kigugumiz cha Afisa inasikika "Endesha tuondoke achana nao"
Mkongo, Mtakuja, Ligera,Milonji kisha Lusewa.

Kazi inaendelea.

Hakuna uhamisho, hirizi kila kona na hadithi za kutisha za kulala makaburini na chooni.

Mara mtoto alipotea wachawi walimficha na kumla, Oooh mwalimu alipotea waganga wakamfichua mashamban alifichwa!

Tena Mbweha na sifa wamekuwa tishio, wazee ofisini wanaonyana kuacha tabia hiyo, na wanyama wanapote!
Ndoa zinavunjika amani hakuna, Biblia ni kwa siri Quran ni bayana.

Mtaaluma na mshauri nasaha ni majukumu yangu ya kazi, Kazi imefanywa ni miaka minne,[HAPO hakuna daraja]

Naombwa na Gabriel nikafundishe Namabengo, maneno ya kilaghai safari ya kwa Mbena.

Naripot na ukatiri unaanza hasa baada ya kujituma kufidia mapengo ya kiuchumi, Mwaka wa Sita Wema wangu unanipoza kisa haki za wanyonge wa kidato cha pili.

Watoto wenye haki wananyimwa haki zao. Wengine Shule wanaacha uraiani wanatokomea bila hata kutafutwa na shule wala viongozi wa serikali za mitaa!

Namtetea mwanangu wa kumlea, apate haki yake.

Longolongo za utawala zimeitawala ofisi, mtoto anakandamizwa, haki yake ananyomwa, na uhamisho analazimishwa.

Nageuziwa kesi ya kumtaka kimapenzi, shitaka nafunguliwa, kesi inaendeshwa kwa njia za mikato. CWT wamejificha wanajifanya TSC,barua nakabidhiwa na kazi nafukuzwa.

Miaka kumi kazini nafukuzwa bila onyo, na mwajiri hanijui Afisa elimu mjumbe mwezangu wa bodi.

Wanangu nilowafundisha pendaneni pambaneni, akili kumkichwa za kuambiwa changanya na zako.
Usisahau utofauti kati ya WORK na JOB.
Msiogope mapori mkajiajiri huko.

Afrika bara langu, Mungu bariki bara langu TANZANIA Tanzania, nchi yangu nayoipenda.

Mungu tubariki sote tutakutana Akhera panapo siku ya hukumu.
 
Mkuu umezungumzia Hali ya ualimu TZ au masaibu uliyokutana nayo kwenye ualimu?
 
Umejaribu kuzungumza na jirani yako Jobless bin Mbangaizaji AKA Hand to Mouth ? Sababu ni wengi sana kitaa kuliko hata nyie wenye Security ya angalau Bank Akaunti Kusoma.....

In short hali si hali kwa majority Watunga Sera wanakula hadi Makombo....

I cried cause I had no Shoes..., Until I saw someone with no Feet (Bongo wengi hawana miguu, ingawa wachache wenye miguu hata hawaitumii wanawatu wa kuwabeba mgongoni)
 
Daaah hata hatujui tunapelekwa kama mang'ombeee, NHIF, LAPF na wengine PSPF Wanajujazisha mikataba ya makubaliano kwa nguvu bila maelekezo ya kina! sauti zinasikika jazeni haraka tuanze safari.
aisee
 
Masaibu wanayokuta nayo walimu nchini yanafanana kwa kiasi kikubwa.
Na furaha na Masaibu ndiyo yanaleta picha ya mwalimu.
 
Pambaneni hakuna anayewaonea au atakayewaonea huruma miaka itaenda miaka itarudi.Mtabaki hapo hapo,
 
Back
Top Bottom