Tanzania yaiteka mioyo ya wawekezaji

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,233
9,679
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania ndio Habari ya mjini katika suala Zima la Kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania imeviteka vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa juu ya kufanya vizuri katika uchumi, Tanzania inatabiliwa kufanya kiuchumi vizuri kupita nchi zote za ukanda huu wa Afrika mashariki, kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara ,Sera nzuri za kiuchumi, kuimarika kwa demokrasia nchini,utawala Bora na kuheshimu misingi ya kisheria katika kuendesha nchi,Uhuru wa vyombo vya habari ,mahakama ,Sera zinazotabilika ,Miundombinu imara na Bora ,umeme wa uhakika hasa kuanzia mwakani tutakapoanza uzalishaji wa umeme wa kutosha baada ya kukamilika na kuanza Uzalishaji Wa Umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere.

Hali hii imeiteka mioyo ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani, Ikumbukwe ya kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza pesa zao sehemu na mahali penye amani ,usalama na utulivu,Sera nzuri za kiuchumi na zinazotabirika,utawala Bora, Demokrasia ya kutosha n.k.

Sasa Tanzania chini ya Nahodha wetu na jemedari wetu,jasusi wa kiuchumi,komandoo wa kisiasa,nguli wa Diplomasia,Jasiri muongoza njia ,shujaa wa Uchumi mama Samia suluhu Hassani ni salama Sana ,Tulivu Sana,Sera nzuri za kiuwekezaji, demokrasia na utulivu wa kisiasa , mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara imekuwa ulimbo na sumaku ya kuwanasa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.

Sasa macho,kiu ya wawekezaji ni kuleta madollar Yao kuja kuwekeza Tanzania,Ni kuja Kufungua mabiashara Yao Tanzania,ni kuja na mafursa ya kiuchumi Tanzania,maana imeonekana Tanzania kwa Sasa Ndio eneo linalolipa kiuwekezaji na kibiashara.

Hii ni kwa kuwa Hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuhatarisha fedha zake na kuwekeza mahali palipo na migogoro ya kisiasa,Sera mbovu za kiuchumi,Sheria mbaya kiuwekezaji,udikiteta,Sera zisizo tabirika,viongozi wasiozingatia utawala Bora na wenye kuzingatia misingi ya kisheria ,matamko ya kisiasa kuwa yenye nguvu na juu kuliko sheria na Sera.

Ndio maana Tanzania inaendelea kukomba na kubeba wawekezaji wote wanaotua katika Bara la Afrika,ndio maana Tanzania inaendelea kufanya vizuri Sana kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji hapa nchini,ndio maana mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ndio maana mzunguko wa fedha Ni mzuri Sana na wenye Afya mitaani,ndio maana ajira zinaendelea kuongezeka mitaani kutokana na miradi inavyoendelea kujengwa mitaani,ndio maana Hali ya kimaisha ya watanzania Ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

Ndio maana Tanzania na watanzania ni wenye furaha,amani na matumaini makubwa Sana katika mioyo Yao,ndio maana kipato na maisha ya kaya moja moja inaendelea kuwa njema na nzuri,ndio maana kwa Sasa kila mtanzania Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, ndio maana Biashara zinaendelea kushamiri mitaani na kufanya vizuri, ndio maana shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafunguliwa kwa wingi Sana mitaani.

Ndio maana watanzania wanaheshimika Sana kwa Sasa,ndio maana kwa Sasa Tanzania inaaminika Sana na Taasisi na jumuia za kimataifa,ndio maana sauti ya Tanzania inaheshimika na kusikilizwa kimataifa,ndio maana Tanzania Ni Kama ufunguo ufunguao kila kufuri,ndio maana Tanzania inapata chochote itakacho kutoka popote na kwa yeyote na ndio maana Tanzania kwa Sasa inaandikwa kwa mazuri kimataifa na kupongezwa kwa mengi mazuri,ndio maana kwa Sasa Tanzania Ni nchi inayopigiwa mfano katika ukuaji na Sera nzuri za kiuchumi.

Hii yote Ni kutokana na maono makubwa aliyo nayo Rais wetu mama Samia suluhu Hassani aliyeamua kuifungua nchi na kuleta fursa nchini,aliyeamua kuitambulisha Tanzania na fursa za kiuwekezaji zilizopo katika anga la kimataifa,aliyeamua kuifanya Tanzania kuwa sumaku ya wawekezaji wote,aliyeamua Kuiteka mioyo ya wawekezaji kwa Sera nzuri za kiuwekezaji,Ni Rais Samia na serikali yake Ndio wameleta Neema hii kwa Taifa letu, Ni Rais Samia wetu na serikali yake walioleta heshima hii kwa Taifa letu ,Ni Rais Samia na serikali yake ya CCM wanayoifanya Tanzania miaka michache ijayo kuwa DUBAI ya Afrika na nchi ya ahadi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Habari hizo
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania ndio Habari ya mjini katika suala Zima la Kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania imeviteka vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa juu ya kufanya vizuri katika uchumi, Tanzania inatabiliwa kufanya kiuchumi vizuri kupita nchi zote za ukanda huu wa Afrika mashariki, kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara ,Sera nzuri za kiuchumi, kuimarika kwa demokrasia nchini,utawala Bora na kuheshimu na Sheria ,Sera zinazotabilika ,Miundombinu imara na Bora ,umeme wa uhakika hasa kuanzia mwakani tutakapoanza uzalishaji wa umeme wa kutosha baada ya kukamilika na kuanza Uzalishaji Wa Umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere.

Hali hii imeiteka mioyo ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani, Ikumbukwe ya kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza pesa zao sehemu na mahali penye amani ,usalama na utulivu,Sera nzuri za kiuchumi na zinazotabirika,utawala Bora na Demokrasia ya kutosha.

Sasa Tanzania chini ya Nahodha wetu na jemedari wetu,jasusi wa kiuchumi,komandoo wa kisiasa,nguli wa Diplomasia,Jasiri muongoza njia ,shujaa wa Uchumi mama Samia suluhu Hassani ni salama Sana ,Tulivu Sana,Sera nzuri za kiuwekezaji, demokrasia na utulivu wa kisiasa , mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara imekuwa ulimbo na sumaku ya kuwanasa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.

Sasa macho,kiu ya wawekezaji ni kuleta madollar Yao kuja kuwekeza Tanzania,Ni kuja Kufungua mabiashara Yao Tanzania,ni kuja na mafursa ya kiuchumi Tanzania,maana imeonekana Tanzania kwa Sasa Ndio eneo linalolipa kiuwekezaji na kibiashara.

Hii ni kwa kuwa Hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuhatarisha fedha zake na kuwekeza mahali palipo na migogoro ya kisiasa,Sera mbovu za kiuchumi,Sheria mbaya kiuwekezaji,udikiteta,Sera zisizo tabirika,viongozi wasiozingatia utawala Bora na wenye kuzingatia misingi ya kisheria ,matamko ya kisiasa kuwa yenye nguvu na juu kuliko sheria na Sera.

Ndio maana Tanzania inaendelea kukomba na kubeba wawekezaji wote wanaotua katika Bara la Afrika,ndio maana Tanzania inaendelea kufanya vizuri Sana kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji hapa nchini,ndio maana mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ndio maana mzunguko wa fedha Ni mzuri Sana na wenye Afya mitaani,ndio maana ajira zinaendelea kuongezeka mitaani kutokana na miradi inavyoendelea kujengwa mitaani,ndio maana Hali ya kimaisha ya watanzania Ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

Ndio maana Tanzania watanzania ni wenye furaha,amani na matumaini makubwa Sana katika mioyo Yao,ndio maana kipato na maisha ya kaya moja moja inaendelea kuwa njema na nzuri,ndio maana kwa Sasa kila mtanzania Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, ndio maana Biashara zinaendelea kushamiri mitaani na kufanya vizuri, ndio maana shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafunguliwa kwa wingi Sana mitaani,ndio maana watanzania wanaheshika Sana kwa Sana..

Hii yote Ni kutokana na maono makubwa aliyo nayo Rais wetu mama Samia suluhu Hassani aliyeamu kujifungua nchi na kuleta fursa nchini,aliyeamu kuitambukisha Tanzania na fursa za kiuwekezaji zilizopo katika anga la kimataifa,aliyeamua kuifanya Tanzania kuwa sumaku ya wawekezaji wote,aliyeamua Kuiteka mioyo ya wawekezaji kwa Sera nzuri za kiuwekezaji,Ni Rais Samia na serikali yake Ndio wameleta Neema hii kwa Taifa letu, Ni Rais Samia wetu na serikali yake walioleta heshima hii kwa Taifa letu ,Ni Rais Samia na serikali yake ya CCM wanayoifanya Tanzania miaka michache ijayo kuwa DUBAI ya Afrika na nchi ya ahadi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Habari hizo
Luka eti ni kweli rimoti iko msoga ?
 
Jqmani chonde chonde tupunguze au kabisa tuache mawazo ya kutegemea wawekezaji wa kutoka nje waje hapa TZ eti kutusaidia kutengeneza uchumi wa nchi yetu. Bali tutafute business partners...sio vibaya tukaenda kujifunza kwa wenzetu tuliokuwa nao pamoja kwenye group la nchi masikini tukiitwa dunia ya tatu wao sasa wamevuka huko nchi kama India na Brazil hawakutegemea wawekezaji kwenye uchumi wao. Ni muda mrefu sasa India ina export wataalamu wa IT wanaofanya kazi Germany. Nashangaa kila kukicha jamani wawekezaji waje tuache huu upuuzi toka wawekezaji wamekuja nchi hii tumefaidika nini? Mfano mdogo angalia hapo Zanzibar hao wawekezaji wa utalii wameleta kitu gani cha kujivunia?? Hata hoteli wanazojenga ni zile duni ambapo ukimkurupusha anaweza kuondoka zake na kukuachia hayo majengo bila kinyongo. Groups za watali zinakuja wakati malipo yameshafanyika nchini kwao mpaka maji ya kunywa yameshalipiwa huko huko sisi tukiona picha kwenye magazeti watalii wakitelemka kwenye ndege tunashangilia Tanzania inaongoza kupokea watalii wakati hujui lolote kuhusiana na kipato cha nchi. Sana sana mtaingiza siasa na kudai unaona kazi ya royal tour hiyo......., milango imefunguliwa sasa wageni wanakuja..... Tunapoongelea uchumi tuache kabisa mambo ya siasa....ukitaka kufilisi duka anza kukopesha alafu utaona....
 
Luca umepamba sana lakini kumbuka mchele kg 4000 sembe kg 2000 na hata maharage siku hizi ni anasa mboga ni utumbo, vichwa na miguu ya kuku.
Katika toleo la hivi karibuni la nchi zenye watu wenye furaha Tanzania ipo karibu na mwisho
 
Hakuna nchi isiyotaka wawekezaji kuja katika nchi yake, wawekezaji wakija maana yake Ni fursa ya kiuchumi na kibiashara,wakija wanakuja kuwekeza ,wanakuja na mitaji,wanakuja kuongeza wigo wa ajira na kikodi ,wanakuja kusaidia upatikanaji wa bidhàa furani kwa Bei Rahisi, wanakuja kusaidia kupunguza uagizaji wa bidhàa furani nje ya nchi,wanakuja na fedha za kigeni zitakazotumika kuagiza bidhàa tusizozalishwa nchini Kama vile baadhi ya madawa ya binadamu au vifaa Tiba,wanakuja kupunguza umaskini maana hapa wanaongeza ajira,fursa za kiuchumi ,kuongeza mzunguko wa fedha mitaani,.wanasaidia kuongeza ujuzi kwa vijana wetu,wanakuja na yeknolojia mpya na ya kisasa ,wanakuja na wataalamu n.k.

Mfano asilimia kubwa ya watanzania Ni wakulima hivyo wengi wanategemea mbolea na pembejeo zingine Kama madawa n.k,hivyo anapokuja mwekezaji kuwekeza katika kiwanda Cha mbolea atasaidia upatikanaji wa mbolea hapahapa nchini Tena kwa Bei nafuu kabisa ,Hali itakayopelekea wakulima kuongeza uzalishaji Sana, hivyo Hali hii itaongeza mavuno na hivyo kuinua maisha ya wakulima na kupelekea kupungua kwa umaskini wa kipato na kumaliza kabisa suala la njaa,lakini hali hii itachochea mapinduzi ya viwanda kutokana na uwepo wa kutosha wa malighafi viwandani, viwanda hivyo vitachochea ongezeko la ajira kwa vijana pamoja na kuongeza mapato,

Lakini pia unapokuwa na viwanda vya kutosha nchini mwako maana yake unapunguza hatari ya mfumuko wa Bei kunapokuwa kumetokea mtikisiko wa Aina yoyote Ile mahali unakochukua na kuagiza bidhàa husika,mfano Bei ya mbolea ilipanda Sana Mpaka serikali kuamua kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea baada ya kuwa Tunakotegemea kuagiza mbolea kuwa katika Vita,lakini Kama tungekuwa tunazalisha hapa nchini migogoro Yao isingetuathiri Wala kupelekea kupanda kwa Bei ya mbolea nchini.

Lakini pia unapokuwa na uwekezaji wa viwanda maana yake unapunguza kuagiza bidhàa nje ya nchi, Hali hii inapunguza matumizi ya hadhina yako ya Fedha za kigeni na pia kufanya fedha nyingi kubakia nchini na hivyo kuupa Afya mzunguko wa fedha na hivyo kuchochea biashara mitaani ,lakini pia bidhàa zinakuwa zinapatikana kwa Bei nafuu kabisa kwa kuwa zinazalishwa Nchini mwetu hivyo mfumuko wa Bei unakuwa haupo
 
Luca umepamba sana lakini kumbuka mchele kg 4000 sembe kg 2000 na hata maharage siku hizi ni anasa mboga ni utumbo, vichwa na miguu ya kuku.
Katika toleo la hivi karibuni la nchi zenye watu wenye furaha Tanzania ipo karibu na mwisho
Kilimo ni biashara ndugu yangu na hakuna anayependa kufanya biashara kichaa,acha wakulima wafaidike na jasho lao maana wameteseka na kuhangaika na kupata hasara kwa miaka mingi Sana,machozi Yao yalikuwa Kama ya samaki ziwani maana Hakuna aliyekuwa anasikia Wala kuguswa na kilio Cha mkulima mpaka alipokuja mama Samia Kama mkombozi wao,

Kumbuka ya kuwa wakulima wanatumia gharama kubwa Sana katika uzalishaji ,hivyo wanastahili kupata bei nzuri ili wasikatike mitaji na kushindwa kulima Tena na hivyo kuhatarisha uwepo wa chakula nchini,kwa miaka mingi Sana wakulima wamelibeba Taifa letu katika mabega Yao kwa kulipatia chakula Cha kutosha ,japo kwa miaka yote wakulima walikuwa wakiishi kwenye maisha ya taabu na Umaskini na kilimo kuonekana Kama kazi ya Wala hoi wa vijijini ,lakini kwa Sasa hata wasomi hasa vijana wameingia kwenye kilimo baada ya kuona kinalipa vizuri na hivyo kupunguza suala la ajira
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania ndio Habari ya mjini katika suala Zima la Kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania imeviteka vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa juu ya kufanya vizuri katika uchumi, Tanzania inatabiliwa kufanya kiuchumi vizuri kupita nchi zote za ukanda huu wa Afrika mashariki, kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara ,Sera nzuri za kiuchumi, kuimarika kwa demokrasia nchini,utawala Bora na kuheshimu misingi ya kisheria katika kuendesha nchi,Uhuru wa vyombo vya habari ,mahakama ,Sera zinazotabilika ,Miundombinu imara na Bora ,umeme wa uhakika hasa kuanzia mwakani tutakapoanza uzalishaji wa umeme wa kutosha baada ya kukamilika na kuanza Uzalishaji Wa Umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere.

Hali hii imeiteka mioyo ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani, Ikumbukwe ya kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza pesa zao sehemu na mahali penye amani ,usalama na utulivu,Sera nzuri za kiuchumi na zinazotabirika,utawala Bora, Demokrasia ya kutosha n.k.

Sasa Tanzania chini ya Nahodha wetu na jemedari wetu,jasusi wa kiuchumi,komandoo wa kisiasa,nguli wa Diplomasia,Jasiri muongoza njia ,shujaa wa Uchumi mama Samia suluhu Hassani ni salama Sana ,Tulivu Sana,Sera nzuri za kiuwekezaji, demokrasia na utulivu wa kisiasa , mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara imekuwa ulimbo na sumaku ya kuwanasa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.

Sasa macho,kiu ya wawekezaji ni kuleta madollar Yao kuja kuwekeza Tanzania,Ni kuja Kufungua mabiashara Yao Tanzania,ni kuja na mafursa ya kiuchumi Tanzania,maana imeonekana Tanzania kwa Sasa Ndio eneo linalolipa kiuwekezaji na kibiashara.

Hii ni kwa kuwa Hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuhatarisha fedha zake na kuwekeza mahali palipo na migogoro ya kisiasa,Sera mbovu za kiuchumi,Sheria mbaya kiuwekezaji,udikiteta,Sera zisizo tabirika,viongozi wasiozingatia utawala Bora na wenye kuzingatia misingi ya kisheria ,matamko ya kisiasa kuwa yenye nguvu na juu kuliko sheria na Sera.

Ndio maana Tanzania inaendelea kukomba na kubeba wawekezaji wote wanaotua katika Bara la Afrika,ndio maana Tanzania inaendelea kufanya vizuri Sana kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji hapa nchini,ndio maana mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ndio maana mzunguko wa fedha Ni mzuri Sana na wenye Afya mitaani,ndio maana ajira zinaendelea kuongezeka mitaani kutokana na miradi inavyoendelea kujengwa mitaani,ndio maana Hali ya kimaisha ya watanzania Ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

Ndio maana Tanzania na watanzania ni wenye furaha,amani na matumaini makubwa Sana katika mioyo Yao,ndio maana kipato na maisha ya kaya moja moja inaendelea kuwa njema na nzuri,ndio maana kwa Sasa kila mtanzania Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, ndio maana Biashara zinaendelea kushamiri mitaani na kufanya vizuri, ndio maana shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafunguliwa kwa wingi Sana mitaani.

Ndio maana watanzania wanaheshimika Sana kwa Sasa,ndio maana kwa Sasa Tanzania inaaminika Sana na Taasisi na jumuia za kimataifa,ndio maana sauti ya Tanzania inaheshimika na kusikilizwa kimataifa,ndio maana Tanzania Ni Kama ufunguo ufunguao kila kufuri,ndio maana Tanzania inapata chochote itakacho kutoka popote na kwa yeyote na ndio maana Tanzania kwa Sasa inaandikwa kwa mazuri kimataifa na kupongezwa kwa mengi mazuri,ndio maana kwa Sasa Tanzania Ni nchi inayopigiwa mfano katika ukuaji na Sera nzuri za kiuchumi.

Hii yote Ni kutokana na maono makubwa aliyo nayo Rais wetu mama Samia suluhu Hassani aliyeamua kuifungua nchi na kuleta fursa nchini,aliyeamua kuitambulisha Tanzania na fursa za kiuwekezaji zilizopo katika anga la kimataifa,aliyeamua kuifanya Tanzania kuwa sumaku ya wawekezaji wote,aliyeamua Kuiteka mioyo ya wawekezaji kwa Sera nzuri za kiuwekezaji,Ni Rais Samia na serikali yake Ndio wameleta Neema hii kwa Taifa letu, Ni Rais Samia wetu na serikali yake walioleta heshima hii kwa Taifa letu ,Ni Rais Samia na serikali yake ya CCM wanayoifanya Tanzania miaka michache ijayo kuwa DUBAI ya Afrika na nchi ya ahadi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Habari hizo
Tunatia aibu madini hayatunufaishi, mijitu ya CCM inaingia mikataba ya hovyo sana, hebu angalia issue ya lithium kule Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom