Tanzania yaiteka mioyo ya wawekezaji

Tanzania yaiteka mioyo ya wawekezaji

Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania ndio Habari ya mjini katika suala Zima la Kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania imeviteka vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa juu ya kufanya vizuri katika uchumi, Tanzania inatabiliwa kufanya kiuchumi vizuri kupita nchi zote za ukanda huu wa Afrika mashariki, kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara ,Sera nzuri za kiuchumi, kuimarika kwa demokrasia nchini,utawala Bora na kuheshimu misingi ya kisheria katika kuendesha nchi,Uhuru wa vyombo vya habari ,mahakama ,Sera zinazotabilika ,Miundombinu imara na Bora ,umeme wa uhakika hasa kuanzia mwakani tutakapoanza uzalishaji wa umeme wa kutosha baada ya kukamilika na kuanza Uzalishaji Wa Umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere.

Hali hii imeiteka mioyo ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani, Ikumbukwe ya kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza pesa zao sehemu na mahali penye amani ,usalama na utulivu,Sera nzuri za kiuchumi na zinazotabirika,utawala Bora, Demokrasia ya kutosha n.k.

Sasa Tanzania chini ya Nahodha wetu na jemedari wetu,jasusi wa kiuchumi,komandoo wa kisiasa,nguli wa Diplomasia,Jasiri muongoza njia ,shujaa wa Uchumi mama Samia suluhu Hassani ni salama Sana ,Tulivu Sana,Sera nzuri za kiuwekezaji, demokrasia na utulivu wa kisiasa , mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara imekuwa ulimbo na sumaku ya kuwanasa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.

Sasa macho,kiu ya wawekezaji ni kuleta madollar Yao kuja kuwekeza Tanzania,Ni kuja Kufungua mabiashara Yao Tanzania,ni kuja na mafursa ya kiuchumi Tanzania,maana imeonekana Tanzania kwa Sasa Ndio eneo linalolipa kiuwekezaji na kibiashara.

Hii ni kwa kuwa Hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuhatarisha fedha zake na kuwekeza mahali palipo na migogoro ya kisiasa,Sera mbovu za kiuchumi,Sheria mbaya kiuwekezaji,udikiteta,Sera zisizo tabirika,viongozi wasiozingatia utawala Bora na wenye kuzingatia misingi ya kisheria ,matamko ya kisiasa kuwa yenye nguvu na juu kuliko sheria na Sera.

Ndio maana Tanzania inaendelea kukomba na kubeba wawekezaji wote wanaotua katika Bara la Afrika,ndio maana Tanzania inaendelea kufanya vizuri Sana kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji hapa nchini,ndio maana mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ndio maana mzunguko wa fedha Ni mzuri Sana na wenye Afya mitaani,ndio maana ajira zinaendelea kuongezeka mitaani kutokana na miradi inavyoendelea kujengwa mitaani,ndio maana Hali ya kimaisha ya watanzania Ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

Ndio maana Tanzania na watanzania ni wenye furaha,amani na matumaini makubwa Sana katika mioyo Yao,ndio maana kipato na maisha ya kaya moja moja inaendelea kuwa njema na nzuri,ndio maana kwa Sasa kila mtanzania Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, ndio maana Biashara zinaendelea kushamiri mitaani na kufanya vizuri, ndio maana shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafunguliwa kwa wingi Sana mitaani.

Ndio maana watanzania wanaheshimika Sana kwa Sasa,ndio maana kwa Sasa Tanzania inaaminika Sana na Taasisi na jumuia za kimataifa,ndio maana sauti ya Tanzania inaheshimika na kusikilizwa kimataifa,ndio maana Tanzania Ni Kama ufunguo ufunguao kila kufuri,ndio maana Tanzania inapata chochote itakacho kutoka popote na kwa yeyote na ndio maana Tanzania kwa Sasa inaandikwa kwa mazuri kimataifa na kupongezwa kwa mengi mazuri,ndio maana kwa Sasa Tanzania Ni nchi inayopigiwa mfano katika ukuaji na Sera nzuri za kiuchumi.

Hii yote Ni kutokana na maono makubwa aliyo nayo Rais wetu mama Samia suluhu Hassani aliyeamua kuifungua nchi na kuleta fursa nchini,aliyeamua kuitambulisha Tanzania na fursa za kiuwekezaji zilizopo katika anga la kimataifa,aliyeamua kuifanya Tanzania kuwa sumaku ya wawekezaji wote,aliyeamua Kuiteka mioyo ya wawekezaji kwa Sera nzuri za kiuwekezaji,Ni Rais Samia na serikali yake Ndio wameleta Neema hii kwa Taifa letu, Ni Rais Samia wetu na serikali yake walioleta heshima hii kwa Taifa letu ,Ni Rais Samia na serikali yake ya CCM wanayoifanya Tanzania miaka michache ijayo kuwa DUBAI ya Afrika na nchi ya ahadi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Habari hizo
Vijana mnatumika vibaya sana
 
Kukopa siyo dhambi,kinachoangaliwa na kuzingatiwa Ni unakopa kwa ajili ya kufanya Nini,Aina ya mkopo yaani masharti ya mkopo,riba ya mkopo, muda wa kuanza kulipa mkopo na faida ya mradi au kazi ya mradi au shughuli ambayo mkopo huo umelengwa kwenda kutumika, katika kukopa serikali yetu ya ccm imekuwa ikizingatia yote hayo na uwezo wetu wa kulipa bado Ni mzuri na pia Deni letu Ni himilivu bado,mkopo ninkwa ajili ya kuchochea maendeleo katika juhudi zako za kujenga uchumi wako,maana ukikomba hadhina yako yote utasababisha athari katika uchumi wako na kupelekea mzunguko wa fedha kuwa hafifu na hivyo kudhoofisha biashara mitaani na hata uagizaji wa bidhàa nje ya nchi kuwa wa kusua sua ,lakini pia italeta umaskini maana watu watashindwa kukopa benki kutokana na riba kubwa kunakotokana na kutukuwepo kwa pesa za kutosha benki
Tuna kazi sana kuvuka mstari huu mwekundu Kwa mentality ya uchawa, haujui soon utapokea adhabu kutokana na matendo yake
 
Hakuna muwekezaji mwenye manufaa hata mmoja , wezi tu hao.

Mtu anakuja na dola milioni 400 hela ambayo watanzania wenyewe wanazo halafu unampa rasilimali muhimu Bure Bure tu kwa masazo ya Kodi na ajira za kuhesabu.
Watanzania wangapi wana 400 milioni dollari?? Hata serikali ingewakopa na Magufuli angewapora alafu unasema anapewa raslimali?? Kwa nini apewe si ananunua kinachouzwa?? Willing buyer and willing seller alafu baadae unamletea ushenzi baada ya kuwekeza dollari 400 milioni wewe una akili timamu au punguani??
 
Jqmani chonde chonde tupunguze au kabisa tuache mawazo ya kutegemea wawekezaji wa kutoka nje waje hapa TZ eti kutusaidia kutengeneza uchumi wa nchi yetu. Bali tutafute business partners...sio vibaya tukaenda kujifunza kwa wenzetu tuliokuwa nao pamoja kwenye group la nchi masikini tukiitwa dunia ya tatu wao sasa wamevuka huko nchi kama India na Brazil hawakutegemea wawekezaji kwenye uchumi wao. Ni muda mrefu sasa India ina export wataalamu wa IT wanaofanya kazi Germany. Nashangaa kila kukicha jamani wawekezaji waje tuache huu upuuzi toka wawekezaji wamekuja nchi hii tumefaidika nini? Mfano mdogo angalia hapo Zanzibar hao wawekezaji wa utalii wameleta kitu gani cha kujivunia?? Hata hoteli wanazojenga ni zile duni ambapo ukimkurupusha anaweza kuondoka zake na kukuachia hayo majengo bila kinyongo. Groups za watali zinakuja wakati malipo yameshafanyika nchini kwao mpaka maji ya kunywa yameshalipiwa huko huko sisi tukiona picha kwenye magazeti watalii wakitelemka kwenye ndege tunashangilia Tanzania inaongoza kupokea watalii wakati hujui lolote kuhusiana na kipato cha nchi. Sana sana mtaingiza siasa na kudai unaona kazi ya royal tour hiyo......., milango imefunguliwa sasa wageni wanakuja..... Tunapoongelea uchumi tuache kabisa mambo ya siasa....ukitaka kufilisi duka anza kukopesha alafu utaona....
Nampa 2 years from now wanaotegemea chochote kwenye uwekezaji huu ambao mikataba yake yenyewe hatujui majina ya kampuni.
 
Nampa 2 years from now wanaotegemea chochote kwenye uwekezaji huu ambao mikataba yake yenyewe hatujui majina ya kampuni.
Utasubiri Sanaa na utaumia moyo wako bure tu maana Tanzania inaendelea kupaa kiuchumi na kufanya vizuri Sana kutokana na ubora wa Sera zake kiuchumi na kiuwekezaji
 
Utasubiri Sanaa na utaumia moyo wako bure tu maana Tanzania inaendelea kupaa kiuchumi na kufanya vizuri Sana kutokana na ubora wa Sera zake kiuchumi na kiuwekezaji
Ok tusubiri 2 years to come, kiufupi siumij ikiwa mambo haya yatatoa Faida Kwa nchi hii ila yakienda ndivyo sivyo, patashika nguo kuchanika pale NEC ya CCM na utakuja mwenyewe hapa kufukunua Uzi huu.
 
Watanzania wangapi wana 400 milioni dollari?? Hata serikali ingewakopa na Magufuli angewapora alafu unasema anapewa raslimali?? Kwa nini apewe si ananunua kinachouzwa?? Willing buyer and willing seller alafu baadae unamletea ushenzi baada ya kuwekeza dollari 400 milioni wewe una akili timamu au punguani??
Wewe mjinga huwezi elewa nachoandika akili zako ndogo unaiona hiyo pesa hapa Tanzania hakuna??

Sasa investment ya dola milioni 400 ndio ya kukaza mishipa ya shingo na Kumtoa Rais ikulu??

Mambo mengine ni kujidhalilisha tu kuyatetea.

Kama watu wamepiga 1.7 trilioni kwenye Reli tu tukisimamia vyema mapato yetu tutashindwa kufanya wenyewe mambo kama hayo mpaka tutegemee watu wengine kuja kuufanya??

Mmekalia wizi tu ndio uwezo wenu ulipoishia ila sio kufikiri rationally.
 
Wewe mjinga huwezi elewa nachoandika akili zako ndogo unaiona hiyo pesa hapa Tanzania hakuna??

Sasa investment ya dola milioni 400 ndio ya kukaza mishipa ya shingo na Kumtoa Rais ikulu??

Mambo mengine ni kujidhalilisha tu kuyatetea.

Kama watu wamepiga 1.7 trilioni kwenye Reli tu tukisimamia vyema mapato yetu tutashindwa kufanya wenyewe mambo kama hayo mpaka tutegemee watu wengine kuja kuufanya??

Mmekalia wizi tu ndio uwezo wenu ulipoishia ila sio kufikiri rationally.
Acha chuki binafsi na kumshambulia watu bila uthibitisho
 
Tuna wawekezaji wengi lakini bado tunaomba misaada na mikopo kwa Ma-Taifa Wafadhili kweli uchumi wetu unakuwa? Au Wazungu wanatupaka matope? Deni la Taifa la nchi yetu ni kiasi gani cha pesa? Deni la Taifa kila kukicha linaongezeka kwenda juu. Tutalimaliza lini hilo Deni la Taifa? Au ndio tuseme Mama anaupiga wingi?

View attachment 2599878
Deni letu bado Ni himilivu,pia mikopo tunayochukua ni mikopo ya masharti nafuu na inayochukua muda mrefu katika kuanza kuilipa,mikopo inatusaidia kuchochea maendeleo yetu kwa kutusaidia kukamilisha miradi yetu ya kimkakati kwa wakati
 
Wewe mjinga huwezi elewa nachoandika akili zako ndogo unaiona hiyo pesa hapa Tanzania hakuna??

Sasa investment ya dola milioni 400 ndio ya kukaza mishipa ya shingo na Kumtoa Rais ikulu??

Mambo mengine ni kujidhalilisha tu kuyatetea.

Kama watu wamepiga 1.7 trilioni kwenye Reli tu tukisimamia vyema mapato yetu tutashindwa kufanya wenyewe mambo kama hayo mpaka tutegemee watu wengine kuja kuufanya??

Mmekalia wizi tu ndio uwezo wenu ulipoishia ila sio kufikiri rationally.
Kukuelewesha wewe ni kazi ngumu sana na utabaki na ujinga kwa kizazi chako chote na wajinga ndio waliwao
 
Kukuelewesha wewe ni kazi ngumu sana na utabaki na ujinga kwa kizazi chako chote na wajinga ndio waliwao
Ndio maana sikutaka kukuandikia mambo magumu sana maana uwezo wako wa kudigest mambo ni mdogo.
 
Uzi Wako umesifu sana mvuto wa Tz kwa wawekezaji wa nje (FDI) na hata kulinganisha na nchi nyingine za Afrk Mashrki.
Lakini hukuweka data zozote au chanzo cha kuaminika. Mpaka hivi karibuni Rwanda na Kenya zilikuwa mbele ya Tanzania kwa kuvutia wawekezaji (FDI). Kenya pia ni mojawapo ya wawekezaji wakubwa hapa TZ. TAFAKARI kidogo kuhusu hilo.
Ni kweli kuna ongezeko la imani ya wawekezaji kwa TZ, lakini bado tatizo la rushwa, urasimu, kukiuka mikataba na kutolipa wawekezaji walioshinda kesi lukuki katika mahakama za migogoro ya kibiashara za kimataifa.
Kama tunajisifu, lakini pia tujikosoe na kujisahihisha KIUKWELI.
 
Back
Top Bottom