Tanzania yaiteka mioyo ya wawekezaji

Tanzania yaiteka mioyo ya wawekezaji

Fikra duni sana hizi kuamini wawekezaj watakuinua kiuchumi...Nchi imetushinda hii tisubri kufa tu labda vitukuu vyetu watazinduka na kuijenga nchi yao kwa namna yao wenyewe..."Tanzanian Youth can't think beyond CCM and CDM lines of interest"..
 
Wajibu wako wa kuijenga nchi yako huwezi ukawaachia wajukuu zako ndio wake wautekeleze wajibu uliokushidlnda wewe kwa uvivu wako ,maana nao watakuwa na wajibu wao kulingana na wakati wao katika ujenzi wa Taifa lao
 
Uvivu huu ndo maana tumeshindwa hadi tunawaalika wageni(Wazungu),kwani wao nchi zao waliwaalika wawekezaji wa wapi? ili wawafanyie maendeleo,walijenga nchi zao kwa mikono yao,nguvu zao na akili zao.....think beyond that line broo,
 
Uvivu huu ndo maana tumeshindwa hadi tunawaalika wageni(Wazungu),kwani wao nchi zao waliwaalika wawekezaji wa wapi?...think beyond that line broo
Hao wanakuja kuongeza na kuchochea fursa za kiuchumi na kibiashara,hata marekani yenyewe inafurahi inapoona makampuni makubwa yanakwenda nchini mwake kuwekeza na kutoa ajira kwa watu wake, ndio maana tuna kitu kinaitwa ubia kati ya secta ya umma na secta binafsi,
 
Naunga mkono hoja
P
Tuna wawekezaji wengi lakini bado tunaomba misaada na mikopo kwa Ma-Taifa Wafadhili kweli uchumi wetu unakuwa? Au Wazungu wanatupaka matope? Deni la Taifa la nchi yetu ni kiasi gani cha pesa? Deni la Taifa kila kukicha linaongezeka kwenda juu. Tutalimaliza lini hilo Deni la Taifa? Au ndio tuseme Mama anaupiga wingi?

19264436_1139708629469183_6919971067146339766_o.jpg
 
Luca umepamba sana lakini kumbuka mchele kg 4000 sembe kg 2000 na hata maharage siku hizi ni anasa mboga ni utumbo, vichwa na miguu ya kuku.
Katika toleo la hivi karibuni la nchi zenye watu wenye furaha Tanzania ipo karibu na mwisho
Soon utauzwa 2000
 
Tuna wawekezaji wengi lakini bado tunaomba misaada na mikopo kwa Ma-Taifa Wafadhili kweli uchumi wetu unakuwa? Au Wazungu wanatupaka matope? Deni la Taifa la nchi yetu ni kiasi gani cha pesa? Au ndio tuseme Mama anaupiga wingi?
Kukopa siyo dhambi,kinachoangaliwa na kuzingatiwa Ni unakopa kwa ajili ya kufanya Nini,Aina ya mkopo yaani masharti ya mkopo,riba ya mkopo, muda wa kuanza kulipa mkopo na faida ya mradi au kazi ya mradi au shughuli ambayo mkopo huo umelengwa kwenda kutumika, katika kukopa serikali yetu ya ccm imekuwa ikizingatia yote hayo na uwezo wetu wa kulipa bado Ni mzuri na pia Deni letu Ni himilivu bado,mkopo ninkwa ajili ya kuchochea maendeleo katika juhudi zako za kujenga uchumi wako,maana ukikomba hadhina yako yote utasababisha athari katika uchumi wako na kupelekea mzunguko wa fedha kuwa hafifu na hivyo kudhoofisha biashara mitaani na hata uagizaji wa bidhàa nje ya nchi kuwa wa kusua sua ,lakini pia italeta umaskini maana watu watashindwa kukopa benki kutokana na riba kubwa kunakotokana na kutukuwepo kwa pesa za kutosha benki
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania ndio Habari ya mjini katika suala Zima la Kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania imeviteka vyombo na Taasisi mbalimbali za kimataifa juu ya kufanya vizuri katika uchumi, Tanzania inatabiliwa kufanya kiuchumi vizuri kupita nchi zote za ukanda huu wa Afrika mashariki, kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara ,Sera nzuri za kiuchumi, kuimarika kwa demokrasia nchini,utawala Bora na kuheshimu misingi ya kisheria katika kuendesha nchi,Uhuru wa vyombo vya habari ,mahakama ,Sera zinazotabilika ,Miundombinu imara na Bora ,umeme wa uhakika hasa kuanzia mwakani tutakapoanza uzalishaji wa umeme wa kutosha baada ya kukamilika na kuanza Uzalishaji Wa Umeme kupitia Bwawa la mwalimu Nyerere.

Hali hii imeiteka mioyo ya wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka maeneo mbalimbali Duniani, Ikumbukwe ya kuwa wawekezaji wanapenda kuwekeza pesa zao sehemu na mahali penye amani ,usalama na utulivu,Sera nzuri za kiuchumi na zinazotabirika,utawala Bora, Demokrasia ya kutosha n.k.

Sasa Tanzania chini ya Nahodha wetu na jemedari wetu,jasusi wa kiuchumi,komandoo wa kisiasa,nguli wa Diplomasia,Jasiri muongoza njia ,shujaa wa Uchumi mama Samia suluhu Hassani ni salama Sana ,Tulivu Sana,Sera nzuri za kiuwekezaji, demokrasia na utulivu wa kisiasa , mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara imekuwa ulimbo na sumaku ya kuwanasa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.

Sasa macho,kiu ya wawekezaji ni kuleta madollar Yao kuja kuwekeza Tanzania,Ni kuja Kufungua mabiashara Yao Tanzania,ni kuja na mafursa ya kiuchumi Tanzania,maana imeonekana Tanzania kwa Sasa Ndio eneo linalolipa kiuwekezaji na kibiashara.

Hii ni kwa kuwa Hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuhatarisha fedha zake na kuwekeza mahali palipo na migogoro ya kisiasa,Sera mbovu za kiuchumi,Sheria mbaya kiuwekezaji,udikiteta,Sera zisizo tabirika,viongozi wasiozingatia utawala Bora na wenye kuzingatia misingi ya kisheria ,matamko ya kisiasa kuwa yenye nguvu na juu kuliko sheria na Sera.

Ndio maana Tanzania inaendelea kukomba na kubeba wawekezaji wote wanaotua katika Bara la Afrika,ndio maana Tanzania inaendelea kufanya vizuri Sana kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji hapa nchini,ndio maana mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ndio maana mzunguko wa fedha Ni mzuri Sana na wenye Afya mitaani,ndio maana ajira zinaendelea kuongezeka mitaani kutokana na miradi inavyoendelea kujengwa mitaani,ndio maana Hali ya kimaisha ya watanzania Ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

Ndio maana Tanzania na watanzania ni wenye furaha,amani na matumaini makubwa Sana katika mioyo Yao,ndio maana kipato na maisha ya kaya moja moja inaendelea kuwa njema na nzuri,ndio maana kwa Sasa kila mtanzania Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, ndio maana Biashara zinaendelea kushamiri mitaani na kufanya vizuri, ndio maana shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafunguliwa kwa wingi Sana mitaani.

Ndio maana watanzania wanaheshimika Sana kwa Sasa,ndio maana kwa Sasa Tanzania inaaminika Sana na Taasisi na jumuia za kimataifa,ndio maana sauti ya Tanzania inaheshimika na kusikilizwa kimataifa,ndio maana Tanzania Ni Kama ufunguo ufunguao kila kufuri,ndio maana Tanzania inapata chochote itakacho kutoka popote na kwa yeyote na ndio maana Tanzania kwa Sasa inaandikwa kwa mazuri kimataifa na kupongezwa kwa mengi mazuri,ndio maana kwa Sasa Tanzania Ni nchi inayopigiwa mfano katika ukuaji na Sera nzuri za kiuchumi.

Hii yote Ni kutokana na maono makubwa aliyo nayo Rais wetu mama Samia suluhu Hassani aliyeamua kuifungua nchi na kuleta fursa nchini,aliyeamua kuitambulisha Tanzania na fursa za kiuwekezaji zilizopo katika anga la kimataifa,aliyeamua kuifanya Tanzania kuwa sumaku ya wawekezaji wote,aliyeamua Kuiteka mioyo ya wawekezaji kwa Sera nzuri za kiuwekezaji,Ni Rais Samia na serikali yake Ndio wameleta Neema hii kwa Taifa letu, Ni Rais Samia wetu na serikali yake walioleta heshima hii kwa Taifa letu ,Ni Rais Samia na serikali yake ya CCM wanayoifanya Tanzania miaka michache ijayo kuwa DUBAI ya Afrika na nchi ya ahadi.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627

Habari hizo
Tuna wawekezaji wengi lakini bado tunaomba misaada na mikopo kwa Ma-Taifa Wafadhili kweli uchumi wetu unakuwa? Au Wazungu wanatupaka matope? Deni la Taifa la nchi yetu ni kiasi gani cha pesa? Deni la Taifa kila kukicha linaongezeka kwenda juu. Tutalimaliza lini hilo Deni la Taifa? Au ndio tuseme Mama anaupiga wingi?

PROTECTION AGAINST THE JINN AND SHAYATEEN.jpg
 
Hao wanakuja kuongeza na kuchochea fursa za kiuchumi na kibiashara,hata marekani yenyewe inafurahi inapoona makampuni makubwa yanakwenda nchini mwake kuwekeza na kutoa ajira kwa watu wake, ndio maana tuna kitu kinaitwa ubia kati ya secta ya umma na secta binafsi,
Marekani hairuhusu wawekezaji uchwara nchini kwake na wababaishaji kama wahindi na wachina kujazana nchini mwake.Ingekuwa amri yangu nisingeruhusu hao wapuuzi kujazana nchini na ningewabana ili walete tija. Wachina wengi hawalipi kodi wame capitalize kwenye ukwepaji kodi pamoja na hao wahindi na ndio maana wanaiona nchi ni rafiki sababu imejaa wajinga kuanzia serikalini hadi uraiani.

Wamarekani wakija kuwekeza wanawekeza vitu vya kueleweka. Wanakuja kweli kubadili maisha ya raia kwa maslahi mazuri, bima ya afya nzuri na benefits kibao kwa wafanyakazi. Huo ndio uwekezaji unaotakiwa ila sio upuuzi wa wanyonyaji wachina na wahindi ambao ni maskini wenzetu tu kasoro ni rangi kufanyisha watu kazi kama vibarua na mishaara yao ya laki 3
 
Tuna wawekezaji wengi lakini bado tunaomba misaada na mikopo kwa Ma-Taifa Wafadhili
Ni kweli kwasababu development demands ni kubwa kuliko local supply hivyo tutaendelea kukopa, grants na kutembeza bakuli!
kweli uchumi wetu unakuwa?
Nikweli unakuwa na soon tunakwenda kuogoza bara zima la Africa once SGR in full swing, LNG in place, JNHPP in full capacity, EACOP in full operation, Bagamoyo port is full operation, zile used cars yards za Japan na Dubai zinahamia Bagamoyo!, no any African country can compete!.
Au Wazungu wanatupaka matope?
No hawatupaki matope, wanatufadhili!.
Deni la Taifa la nchi yetu ni kiasi gani cha pesa?
Deni ni kubwa liko kwenye taarifa ya CAG ila ni himilivu!.
Au ndio tuseme Mama anaupiga wingi?
Yes indeed!.
P
 
Marekani hairuhusu wawekezaji uchwara nchini kwake na wababaishaji kama wahindi na wachina kujazana nchini mwake.Ingekuwa amri yangu nisingeruhusu hao wapuuzi kujazana nchini na ningewabana ili walete tija. Wachina wengi hawalipi kodi wame capitalize kwenye ukwepaji kodi pamoja na hao wahindi na ndio maana wanaiona nchi ni rafiki sababu imejaa wajinga kuanzia serikalini hadi uraiani.

Wamarekani wakija kuwekeza wanawekeza vitu vya kueleweka. Wanakuja kweli kubadili maisha ya raia kwa maslahi mazuri, bima ya afya nzuri na benefits kibao kwa wafanyakazi. Huo ndio uwekezaji unaotakiwa ila sio upuuzi wa wanyonyaji wachina na wahindi ambao ni maskini wenzetu tu kasoro ni rangi kufanyisha watu kazi kama vibarua na mishaara yao ya laki 3
Hapo Ni suala letu na jukumu letu kuhakikisha kuwa tunadhibiti mianya yote ya ukwepaji wa Kodi na upotevu wa mapato,lakini pia kudhibiti ubora wa bidhàa zote zinazozalishwa na kuingia nchini , kuhakikisha kuwa bidhàa ni bora na inayokidhi viwango unapokuwa inaingia na kuruhusiwa kutumika na kutumiwa na watu,kwa kufanya ukaguzi wanmara kwa Mara pamoja na kuchukua hatua Kali za kisheria kwa mtu au kampuni au Taasisi itakayoonekana na kukutwa imekiuka misingi ya kisheria ya uzalishaji wa bidhàa katika ubora unaohitajika
 
Kwa jinsi ambavyo nawatambua watawala wa CCM katika suala zima la uwekezaji na mikataba, hapo itakuwa ni umangungo mtupu.
 
Kwa jinsi ambavyo nawatambua watawala wa CCM katika suala zima la uwekezaji na mikataba, hapo itakuwa ni umangungo mtupu.
Serikali yetu ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia ni yenye uzalendo na yenye kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu,ndio maana tumekuwa tukiambiwa juu ya Mambo mengi kwa uwazi pale serikali inapopokea mkopo au kuomba mkopo,inafanya Mambo kwa uwazi kwa kutambua kuwa sisi ndio walipaji wa mikopo yote,ndio maana serikali yetu inafanya vitu kwa uaminifu na uadilifu wa Hali ya juu sana
 
Kweli kabisa mdogo wangu Lucas, kwani hata ripoti ya CAG ya mwaka huu inahakisi taswira hiyo!
 
Back
Top Bottom