Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi

Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,441
Reaction score
38,124
Heshima wanajamvi,

Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi.

Msaada huo ulikabidhiwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Balozi Patrick Tsere jana Wilaya ya Songwe na Karonga mpaka baina ya Tanzania na Malawi.

Msaada wa Madawa na Chakula ulisafirishwa na magari ya JWTZ (TPDF).

Juzi baadhi ya wanajamvi walileta mabandiko JamiiForums kwamba wameona magari ya jeshi yakielekea mpaka wetu na nchi ya Malawi na kutuamini pengine vita vingeweza kuanza wakati wowote kumbe tulikuwa tumewapelekea Wamalawi chakula baada ya kukumbwa na mafuriko makubwa.



timthumb.php.jpeg

Tanzanian on Wednesday donated 1,200 metric tons of maize and 66 tons of medicine to the government of Malawi to assist thousands of people who were affected by floods in the country.

Speaking to Nyasa Times after presenting the donation at Songwe boarder in Karonga the northern part of Malawi, the Tanzanian High commissioner Patrick Sele said the donation follows the disaster which affected 15 of the country's 28 districts, prompting President Peter Mutharika to declare a State of Disaster.

Malawi being our neighbouring country, our President Jakaya Kikwete was deeply concerned with the situation that people in Malawi found themselves in, as such he decided to donate these relief items to those flood victims to bail out the problems that the victims are encountering, said Sele.

He said the donation includes 1,200 metric tons of maize, as well as 66 tons of medicines. Tanzanian Ambassador to Malawi Patrick hailed the existing cordial relationship between the two countries.

Secretary and Commissioner for Disaster Management Affairs Paul Chiunguzeni commended the Tanzania for the assistance saying it is on the right time as floods victims in the country continues to face hunger problems.

Malawi is grateful for Tanzania's contribution as we are trying to relieve the plight of the survivors some of whom are still in camps, he said. According to Chiunguzeni, Malawian soldiers will take over the assistance from Songwe boarder to Lilongwe ware house hauled in military trucks.

He said the Malawi Defence Force (MDF) presence at the border post was a matter of courtesy to their Tanzanian military counterparts. Tanzanian on Wednesday donated 1,200 metric tons of maize and 66 tons of medicine to the government of Malawi to assist thousands of people who were affected by floods in the country.

After presenting the donation at Songwe boarder in Karonga the northern part of Malawi, the Tanzanian High commissioner Patrick Sele said the donation follows the disaster which affected 15 of the country's 28 districts, prompting President Peter Mutharika to declare a State of Disaster.

Malawi being our neighbouring country, our President Jakaya Kikwete was deeply concerned with the situation that people in Malawi found themselves in, as such he decided to donate these relief items to those flood victims to bail out the problems that the victims are encountering, said Sele.

He said the donation includes 1,200 metric tons of maize, as well as 66 tons of medicines . Tanzanian Ambassador to Malawi Patrick hailed the existing cordial relationship between the two countries.

Secretary and Commissioner for Disaster Management Affairs Paul Chiunguzeni commended the Tanzania for the assistance saying it is on the right time as floods victims in the country continues to face hunger problems.

Malawi is grateful for Tanzania's contribution as we are trying to relieve the plight of the survivors some of whom are still in camps, he said. According to Chiunguzeni, Malawian soldiers will take over the assistance from Songwe boarder to Lilongwe ware house hauled in military trucks.

He said the Malawi Defence Force (MDF) presence at the border post was a matter of courtesy to their Tanzanian military counterparts.

Source:Nyasa Times.
 
Baadhi ya raia wa Malawi wameonyesha shaka kubwa magari ya jeshi kutumika katika misaada ya kiraia.
 
Watu wanamsema JK vibaya lakini katika swala la kutumia diplomasia kusuluhisha mikwaruzo na majirani zake yuko juu mno! Kwa hili nampa maksi kubwa sana! Sipati picha endapo rais wa nchi angekuwa .............., mpaka sasa tungekuwa tushahesabu vita mbili tayari: Against Malawi na Against Rwanda. But JK kaucheza mchezo vizuri na jana tu tulikuwa na Kagame hapa Bongo! Kila kitu almost kiko resolved and by now TZ and Rwanda speak BUSINESS only!...What an achievement!!!

Malawi tuna kasafari kidogo but am sure mambo yatakuwa sawa soon!
 
Walitakiwa watuamkiage,
Basi tu ujeuli wao.
 
Baadhi ya raia wa Malawi wameonyesha shaka kubwa magari ya jeshi kutumika katika misaada ya kiraia.

Walitaka yaende malory ya Bakharesa? Wangejua ni jinsi gani kodi ya wa tz imetumika hapo wangelia. Maana gharama za usafirishaji ni kubwa kuliko thamani ya huo msaada.
 
Serikali imefanya vizuri katika hilo. Ugomvi wetu wa ziwa Nyasa uko pale pale !
 
Wasisahau na shule zetu za serikali zimefungwa kwa kukosa chakula.Wanafunzi hawajui watarudi lini kuendelea na masomo yao.
 
Na tena sisi we dont share boder na malawi na tulidonate 91 million mbio mbio(na vile kenya hua kuna beaurocracy nyingi wakati wa kutoa pesa from the treasury)

Anyway, give credit where its due, hongereni watz kwa kuwasaidia wamalawi
hiyo habari ya wakenya kuichangia malawi fedha naifahamu,lengo langu kwenu ni kuwaonyesha kwamba hatuna ugomvi na malawi kama wakenya wengi mnavyo jidanganya.:lol:
 
Hospitali zetu mbona hazina madawa? Hiyo ni sifa, ukarimu au ujinga
 
Tanzania ina chakula cha kutosha hadi tunawauzia Kenya wasije kufa kwa utapia mloo,tunawapatia msaada Malawi wa chakula na madawa bureeeeeee.

Nakala MK254 Geza Ulole .................
 
Last edited by a moderator:
TANZANIA YAIKABIDHI MALAWI MSAADA KWA AJILI YA WAHANGA WA MAFURIKO
​

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu kwa Serikali ya Malawi ikiwa ni msaada wake kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea nchini humo mwezi Januari mwaka huu na kusababisha maafa makubwa.

attachment.php


Msaada huo umekabidhiwa hivi karibuni na Mhe. Patrick Luciano Tsere, Balozi wa Tanzania nchini Malawi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kupokelewa na Katibu Mkuu na Kamishna wa Idara ya Maafa, Bw. Paul Chiunguzeni kwa niaba ya Serikali ya Malawi. Aidha, msafara uliopeleka msaada huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), uliongozwa na Luteni Kanali B.B. Kisinda.

attachment.php


Katika hotuba yake fupi wakati wa makabidhiano, Balozi Tsere alisema kwamba msaada huo umetolewa na Tanzania ikiwa ni agizo kutoka kwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuguswa kwake na maafa hayo makubwa na pia kuitikia wito uliotolewa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Prof. Arthur Bingu Mutharika kwa Jumuiya ya Kimataifa na watu mbalimbali wenye uwezo kutoa msaada kwa wahanga hao wa mafuriko.

Aidha, Balozi Tsere alieleza kwamba, Malawi na Tanzania ni nchi jirani, marafiki na zinazoshirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo majukwaa ya kimataifa kama vile Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa.

"Hivyo, kwa kutambua mahusiano hayo ya ujirani mwema na udugu baina ya nchi hizi na watu wake, Tanzania imeona ni jambo jema kushirikiana na jirani yake katika kupunguza athari za maafa hayo kwa wahanga hao kwani siyo vyema kuona jirani yako amepatwa na matatizo na kisha unakaa kimya" alisema Balozi Tsere.

Mhe. Tsere aliongeza kwamba ingawa msaada huo hautoshelezi kutatua tatizo hilo kabisa bado utaweza kusaidia wahanga hao na kupunguza tatizo lililopo kwa kiasi Fulani.

Malawi ilikumbwa na mafuriko mwezi Januari mwaka huu. Mafuriko hayo yalisababisha maafa makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha, nyumba kuharibiwa na mazao mashambani kusombwa na maji. Kwa hivi sasa familia katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo hazina mahali pa kuishi na zinahitaji msaada wa chakula na kumekuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo hayo kama vile kipindupindu.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

27 MACHI, 2015
 

Attachments

  • malawi 1.jpg
    malawi 1.jpg
    181.9 KB · Views: 1,744
  • malawi0.jpg
    malawi0.jpg
    186.3 KB · Views: 1,536
  • malawi2.jpg
    malawi2.jpg
    179.3 KB · Views: 245
  • malawi3.jpg
    malawi3.jpg
    172.6 KB · Views: 255
  • malawi4.jpg
    malawi4.jpg
    174.3 KB · Views: 249
  • malawi5.jpg
    malawi5.jpg
    177.2 KB · Views: 251
Back
Top Bottom