Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi

Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi

Umeona eeh. Kutafuta sifa za kijinga, unagawa chakula chote ilhali wanao wanakufa na njaa

Kupenda tu Sifa za kijinga. Haiwezekani wanao ndani wanalia njaa alafu wewe ukajenge heshima bar na wapambe.
 
ni ajabu sana kutoa kibanzi kwa mwenzio wakati wewe una boriti. anyway labda secret agenda.
 
Heshima wanajamvi,

Tanzania yaisaidia chakula na madawa Malawi.

Msaada huo ulikabidhiwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Balozi Patrick Tsere jana Wilaya ya Songwe na Karonga mpaka baina ya Tanzania na Malawi.

Msaada wa Madawa na Chakula ulisafirishwa na magari ya JWTZ (TPDF).

Juzi baadhi ya wanajamvi walileta mabandiko JamiiForums kwamba wameona magari ya jeshi yakielekea mpaka wetu na nchi ya Malawi na kutuamini pengine vita vingeweza kuanza wakati wowote kumbe tulikuwa tumewapelekea Wamalawi chakula baada ya kukumbwa na mafuriko makubwa.

Hii ndio JF bana! imejaa michagadema kila kitu kwao ni siasa tu!
 
Hivi kulikuwa na ulazima wa kutumia magari ya jeshi na kwenda kijeshi? Si wangewapa hiyo kazi ma-transpoters? Nadhani lengo lilikuwa zaidi kwenda kijionesha kuliko kutoa msaada! Tunependa sifa, sijui tungekuwa na uwezo kama uchina sijui ingekuwaje?
 
ni jambo la kheri ila wamechelewa kuwapa msaada huo mapema
 
Hivi kulikuwa na ulazima wa kutumia magari ya jeshi na kwenda kijeshi? Si wangewapa hiyo kazi ma-transpoters? Nadhani lengo lilikuwa zaidi kwenda kijionesha kuliko kutoa msaada! Tunependa sifa, sijui tungekuwa na uwezo kama uchina sijui ingekuwaje?
magari yanayoleta tani zote za msaada hayajafika yapo njiani,. Magari ya jeshi yametangulia kufikisha ujumbe.
 
aksante Raisi wetu na amiri jeshi mkuu. Diplomasia yako kimataifa ni kubwa sana;
Siku zote nasema maraisi wenye majina ya abb JK

JAKAYA KIKWETE
JULIUS KAMBARAGE
JOHN KENNNEDY.

Ni WENYE HURUMA SAANA NA MAPENZI SANA. SIJUI RAIS GANI AJAE MWENYE JK?????????????????????
 
Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Hakuna mtu mnafiki kama wewe,tangu lini wana ccm mkaipenda Tanzania? wewe mwanamke hunaga aibu sijui umekulia makuzi gani yasiyo na heshima wewe? ndo maana ulikimbia kuishi Canada,ningeshangaa sana kama ungeendelea kuishi ktk taifa la watu wenye akili na hekima kama Canada wakati wewe ni mpumbavu kupindukia.
 
Zamani nilisikia wale jamaa wa mvua ya mawe kule wanaandama kuhusu huduma zinazotolewa, pia nilisikia kuhusu ukosefu wa madawa nchini katika hospitali zetu,,,,, Kweli sahizi tumejipanga
 
Hivi kulikuwa na ulazima wa kutumia magari ya jeshi na kwenda kijeshi? Si wangewapa hiyo kazi ma-transpoters? Nadhani lengo lilikuwa zaidi kwenda kijionesha kuliko kutoa msaada! Tunependa sifa, sijui tungekuwa na uwezo kama uchina sijui ingekuwaje?
ma Transporters wakawaida bila ulizi wangeporwa na Red Guards nilazima pawe escort ya Military hardware Kali pa moja na Makomandos ya JWTZ.
 
Huu ni ujinga,watz wanakufa kwa kukosa madawa halafu nchi inagawia mataifa mengine. Tz tumejitosheleza kiasi gani hadi kugawia nchi nyingine? Hizi ni sifa za kijinga,uonekane mwema wakati familia inakufa njaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom