joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Hii ni habari njema sana kwa utengemano wa EAC. Ninakumbuka siku za nyuma nchi za Uganda, Rwanda, South Sudan zikiongozwa na Kenya, zilizindua reli ya kuziunganisha kule Mombasa chini ya Umoja uliojulikana kama "Coalition of the willings"(CoW), sina uhakika kama Umoja huo bado upo.
Nchi zile zile zimeamua kutumia bandari ya Dar, kila nchi ikitoa sababu tofauti, South Sudan imekua nchi ya mwisho kuja kuomba kutumia bandari ya Dar. Hii ni baada ya kusikia kwamba, Tanzania imetoa pesa, vifaa na mafundi ambao walienda kufufua reli ya Uganda toka Port bell hadi Kampala, ili treni zinazitoka Dar, zikifika Mwanza zibebwe na meli maalumu hadi port bell na hatimaye kufika Kampala. Tafadhali tuupatie jina huu umoja wa sasa, ili tuutofautishe na" CoW".