Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,878
Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa Barani Afrika ameelezea wasiwasi wake kuhusu namna Tanzania inavyokabiliana na mlipuko wa Virusi vya Corona.
Dkt. John Nkengasong aliiambia BBC hakuwa na data za kutosha za kufahamu hali ilivyo nchini Tanzania. Alisema kituo cha kudhibiti magonjwa kimeanzisha jitihada za pamoja za kupambana na virusi hivyo.
"Tunaendelea kutumaini na kuiomba Tanzania kuripoti hali ilivyo ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuondoa virusi hivi katika bara hili," alisema. Alisisitiza kuwa kuna uhitaji wa mataifa yote ya Afrika kushirikiana katika hili.
"Tunaendelea kuwasiliana na Tanzania lakini bado hatujapata majibu ambayo tunayatarajia," alisema. Rais wa Tanzania John Magufuli amesisitiza kusema kuwa taifa lake liko salama.
Tanzania inajiandaa kufanya uchaguzi mwezi Oktoba na shamrashamra za Uchaguzi zimeanza. Wananchi wengi wa taifa hilo wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuvaa barakoa na wala kuzingatia kukaa mbali.