Tanzania ya Viwanda: Tumefikisha 49% ya lengo!

Tanzania ya Viwanda: Tumefikisha 49% ya lengo!

Ukiomba ufafanuzi unaitwa mchochezi unapinga juhudi zote za mzalendo no 1. Ndo utamaduni mpya unaojengwa kwa kutumia polisisiem.
 
Kwa kweli hivi ni vichekesho hivi viwanda viko wapi jamani maana hata hizo bidhaa zinazozalishwa huko hatuzioni hebu tuache kuonana mazwazwa .

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Hivyo viwanda vipo Tz. ipi jamani? mie Napata shida sana kuhusu hizi data. vilijengwa lini na vipo wapi tukaombe kazi? Da!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Tanzania Tanzania nchi yangu
 
Vyerehani vitatu ni kiwanda.
Tehe tehe teh..
Kwani tafsiri ya kiwanda ni ipi ndio cherehani tatu ni kiwanda,nadhani hujatembea ndugu,kiwanda sio lazima kiwe heavy duty industry,ukienda China na India wana viwanda vingi vya aina unayoiponda na ndio hutoa ajira kubwa,hata hapo kenya wana Jua Kali ni viwanda ambavyo vianatoa ajira kubwa kuliko hata hivyo vya Dangote.Usilolijua ni kama usiku wa kiza kaka,unaishia kucheka wakati unaonyesha umbumbumbu uliotukuka
 
Ni kweli kabisa. Na mie juzi nimefungua kiwanda cha kukamua juisi ya miwa hapo kwa Azizi Ali nauza na urojo.
 
Hivyo viwanda vipo Tz. ipi jamani? mie Napata shida sana kuhusu hizi data. vilijengwa lini na vipo wapi tukaombe kazi? Da!
Nadhani tatizo tunadhani viwanda ni vya aina ya kama cha Dangote,nadhani mumesahau hata lengo la kuanzishwa SIDO,hata kama una karakana ya useremala au kushona ni kiwanda,nendeni China na India huko kuna viwanda vingi kama hivi utakuta mtu ana kiwanda chumbani kwake anatengeneza sufuria za aluminium na kuzisambaza madukani,huko China na hata Thailand wana viwanda vingi vya kushona nguo ambavyo utakuta vina vyerehani hata vitano na watu hata Watanzania wengi ndio huenda kutoa oda za kushonewa nguo ambazo tunanunua huko Kinondoni , Sinza n.k
Tatizo kubwa Watanzania hatujui dhana ya viwanda,hata hapo Kenya viwanda ambavyo vinaongoza kwa kutoa ajira sio kama vya akina Dangote Cement bali ni Jua Kali.Usitegemee kuomba kazi tu tafuta mtaji ujiajiri hata kwa kuuza crips za maembe /ndizi/mihogo n.k.Tanzania ya sasa hata nyasi/majani/mawe ni pesa.
 
Kweli nimeamini viwanda ni vyrehani. Kwanza walishasema tuna viwanda elfu tatu na ngapi sijui, sasa huyu anasema 1285! Ngoja aje kutumbuliwa sasa
Na Mimi nimeshangaa kwa nini viwanda vyetu vinapungua kwa kasi kiasi hiki? Toka 3200 mwezi septemba 2017 hadi 1200 March 2018? Kuna tatizo mahali.
 
49% in two years of JPM! Haya ni mafanikio makubwa sana. Tunaweza kujua ni ajira kiasi gani na uchumi umeinuka kuanzia asilimia ngapi toka kwenda ngapi ktk kipindi hiki kifupi!
Kaulize tuone kama hatujakuokota Koko beach
 
Viwanda vya siku hizi ni kama upepo mbona havionekani ?

Hebu orodhesheni viwanda vilivyojengwa mfano Mkoa... Wilaya... Mtaa/Kijiji ili watu tupate picha halisi..

Hivyo viwanda vimetoa ajira ya watu wangapi mpaka sasa mfano skilled labour + unskilled labour wangapi wameajiriwa..
1. Kiwanda cha kununua binadamu
2. Hapa kazi tu
3. Manina industriea......endelea
 
Tarehe 26/3/2018 nazindua kiwanda cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na ulanzi mfano: mkangafu,mndindufu,togwa n.k nitatoa ajira kwa vijana zaidi ya 16 ,karibuni sana tuungane kuzindua kiwanda
 
Kwenu,

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, ametoa taarifa ya serikali kuhusu malengo ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Kwa mujibu wa waziri, mpaka sasa tumefikisha viwanda 1285,sawa na 49% ya lengo ndani ya robo ya muda. Hii ni hatua nzuri lakini hesabu zake ni ngumu.
Jambo jema ,ni la kupongezwa
 
nasikia wenye mashine za kukamulia juisi za miwa nao wametakiwa wakajisajili kama wamiliki wa viwanda..
natumai sasa exportation ya Tanzania itakua balaa..
marekani twaja huko
kuuza mitumba..
 
Kwani tafsiri ya kiwanda ni ipi ndio cherehani tatu ni kiwanda,nadhani hujatembea ndugu,kiwanda sio lazima kiwe heavy duty industry,ukienda China na India wana viwanda vingi vya aina unayoiponda na ndio hutoa ajira kubwa,hata hapo kenya wana Jua Kali ni viwanda ambavyo vianatoa ajira kubwa kuliko hata hivyo vya Dangote.Usilolijua ni kama usiku wa kiza kaka,unaishia kucheka wakati unaonyesha umbumbumbu uliotukuka
Matusi yanamtafsiri mtu mwenye kuyatoa. Pile sana mfia nchi
 
Back
Top Bottom