Tanzania ya Viwanda: Tumefikisha 49% ya lengo!

Tanzania ya Viwanda: Tumefikisha 49% ya lengo!

Mimi naona hapa mjini kwetu kuna viwanda Vinci kwelikweli. mafundi wa kushona zaidi ya viwanda 20 wachoneaji viwanda 10 viwanda vya juice ba icecream takriban 45 washona viatu 5 wachapaji viwanda 6 wapishi nao c viwanda 50 jamani mpaja nashindwa kuhesabu. Tuache wivu. Hesabu tuu pale mtaani kwako utaona viwanda vya kutosha. je kwa nchi nzima? Hivyo 3000 ni vixhache sana. Uchumi umeimarika sana na vyuma vishalegea sana. Tusiwe na wivu tuipwnde nchi yetu. Tanzania oyeeeeeeee
 
Kweli nimeamini viwanda ni vyrehani. Kwanza walishasema tuna viwanda elfu tatu na ngapi sijui, sasa huyu anasema 1285! Ngoja aje kutumbuliwa sasa
Nilikuwa bado nashangaa hii namba 1285 wakati Rais anafungua kiwanda pale Pwani walisema zaidi ya elfu 3 sasa vimepunguaje au nini kimetokea? Au mwanzo walikosea hesabu? Rais wetu anafanywa mjinga sana.
 
Mungu wangu... 49% kati hivyo viwanda sijaona product mpya ya bidhaaa...
 
Nimejaribu kupiga hesabu nikaona kuwa kama hivi viwanda 1285 mpaka juzi vilivyokwisha jengwa tayari na kuanza uzalishaji ......

Maana yake ni kuwa kama kila kiwanda kingeweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa wastani wa 100 tu, basi ina maana ktk hii miaka miwili tu sekta ya viwanda hivi vipya pekee ingeshatoa jumla ya ajira za moja kwa moja (direct employments) zaidi ya 128,500!!

Maswali ya kijiuliza ni haya:

1. Je, huu ndiyo uhalisia kwa kulinganisha takwimu za serikali na uhalisia on the ground ??

2. Ni kwa nini takwimu za serikali yenyewe zinaonesha collection ya mapato kushuka iwapo sekta moja tu ya uchumi (viwanda) bila kutaja sekta zingine kama Kilimo, madini, utalii nk imeingiza sokoni watu walioajiriwa zaidi ya 130,000 ambao wanalipa kodi ya mapato ya mishahara achilia mbali kodi zingine za moja kwa moja zinazolipwa na viwanda hivi kama corperate tax nk??

3. Hivi kwanini isiwezekane mtu mwingine kufikiri kuwa hizi ni propaganda za kisiasa za utawala huu mchovu kabisa kuwahi kutokea Tanzania ??

Ni rahisi mno kufikiri hivi kwa sbb wakisemacho hakina uhalisia na hakiwiani na uhalisia wa akili na macho ya watanzania wenye akili wanaojitambua na wenye ufahamu....

Ndiyo maana utawala huu chini ya CCM ya Magufuli haitaki UWAZI kwa sbb inaogopa uongo kama huu kuchambuliwa na kuanikwa wazi na badala yake wao ndiyo wanasema tuuu na kuwalisha watu matango pori !!
 
Nahis kuna watu hawako serious, viwanda vinatakiwa viwe vikubwa, atleast vitoe ajira za watu 100.

Lakin kama mtu anakuja kusema vyerehani vinne ni kiwanda, this is fukin joke kabisa.
We need kiwanda kitakacho toa ajir za kutosha, na pia kuletea mapato serikali.
 
Msiwe wakali waungwana, tafsiri ya neno VIWANDA mnayoijua nyie inawezekana ni ya karne ya 19, kwakuwa ccm hutuwekea serikali sikivu madarakani na kuipa serikali ya chama ilani ya maendeleo, WAULIZENI tu kwa upole; VIWANDA kwa tafsiri ya ilani yao ni nini?
 
Yawezekana kufikia 2020 utekelezaji wa sera utakuwa 100+%¹
Na inji itakuwa uchumi wa katikati.
Andae sera nyingine, mmeonyesha uzoefu.
 
hapo jamaa anachekelea sana,lakini ikianza kuesabiwa hata hamsini avifiki,na kwa nini hivyo viwanda vyenyewe atutajiwi?ni vya kutengeneza nini na viko wapi kwa nini waandishi wa habari wanashindwa kuuliza vilipo hivyo viwanda? natamani siku moja aitwe waziri wa viwanda kwenye kipindi cha je?tutafika alafu atutajie horodha ya hivyo viwanda
 
Wasiwasi wangu mkubwa haupo kwenye viwanda vingapi tunaanzisha bali vingapi vitaweza ku survive. Kuna umuhimu wa kuwa na maono ya mbali na ya kijasiriamali kuona tuanzisha viwanda ambavyo tutaweza kuviendesha ili viendelee kuwepo kwani nakumbuka kipindi cha mwalimu aliweza kuanzisha viwanda vingi lakini baadae vilikufa. sasa ni vizuri tukajiuliza tulijifunza nini ambacho wakati huu hatutaweza kurudia makosa. Kwani kuanzisha viwanda ni jambo moja lakini kuweza kuvifanya viendelee kuwepo kwenye mazingira ya ushindani ni jambo lingine.
 
Back
Top Bottom