Mkuu umenikumbusha habari za Mathieu Kerekou. Alishindwa na wapinzani kwenye uchaguzi wa vyama vingi wapinzani wakatawala kipindi kimoja kisha mzee akashinda uchaguzi uliofuata!! Huenda hii ndiyo unasema ilifuatia kuomba kwake msamaha.
Twende mbele turudi nyuma Lowassa ni mtendaji na akipewa nchi tutaona mabadiliko makubwa. Huyu ni miongoni mwa wale watu ambao wakisema mlima huu uondoke basi unaondoka. Nakumbuka machache tu aliyofanya wakati wa u PM wake:
- Kuna siku alimwamuru injinia wa DAWASCO kuingia kwenye bomba na suit yake. Kulitokea kukatika kwa maji Dar kutokana na kuharibika kwa bomba kubwa huko bunju basi PM akaenda kuangalia maendeleo ya matengenezo ati na injinia wa DAWASCO akaja na suit badala ya overall, PM akamuamuru azame. Ilichukua muda mfupi maji kurejea ktk hali ya kawaida. Uthubutu
- Kulikuwa na usuasuaji wa ukarabati wa barabara ya Shekilango. PM akaingia Makamba (RC) akatetemeka muds si muda barabara ikawa tayari. Uthubutu
- Kukawa na giza akaingilia kati kuhusu kununua mitambo. TANESCO na wizara wakakosea PM akajiuzulu! Uthubutu
- Wakati akiwa waziri wa maji Misri walikuwa wakikatalia maji ya Nile ati sisi hatuwezi kutumia maji ya ziwa victoria. Mzee akasema hakuna mkataba wa mwaka 1910 hapa maji ni yetu akayapeleka shinyanga na Kahama!! Uthubutu
- Nchi haikuwa na vyumba vya madarasa. Wakakubaliana kwamba kila kata na iwe na sekondari. EL akasimamia. Watu wakalazimishwa kuchanga na wengine wakachanga wa hiari yao. Wakuu wa mikoa na wilaya wakatetema. Kila kata ikapata sekondari. Uthubutu
- etc