Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,767
- 4,035
Naomba mungu akulaani wewe mleta mada kwa kusema vitu vya uongo ili wakustukie wakufukuze kazi uwe unazunguka tu mitaani na usipate kazi popote.
Siri imefichukaeace:
Naomba mungu akulaani wewe mleta mada kwa kusema vitu vya uongo ili wakustukie wakufukuze kazi uwe unazunguka tu mitaani na usipate kazi popote.
Ikitokea Ruzuku imeondolewa, chama gani kitakufa haraka?
tendwa ni tikiti maji...
Bado nangoja mwenelezo wa darasa hili!.
Wakuu tiririka zaidi ili niweze kuelewa nielimike.
I always keep asking myself why CCM walikubali siasa ya vyama vingi?? maana kila kukicha wanatumia taasisi zao kama POLISI, MSAJILI WA VYAMA,USALAMA WA TAIFA, MAHAKAMA ili Kugandamiza demokrasia na kudhibiti wapinzani hata ikibidi kuuwa, Ulaghai, kubambikia watu kesi na kila aina ya manyanyaso na ubakaji wa demokrasia.Si waseme tuu nchi ni ya chama kimoja? Baba na Mama wa Demokrasia TZ alishakufa zamani, vyama vya upinzani vimabaki yatima.
Huu sasa ni upuuzi wa hali ya juu kuwahi kufanywa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa!
Kwa watu wasiojua ukweli/uongo wanaamini kile wanachokisikia kiwe kweli au uongo.
Sasa wewe unaposema kuwa habari hii si ya ukweli, basi tunaomba utupe hizo habari ulizo nazo za ukweli.:help:
Kumbe ulikuwa hujajua siri ya TZ kukubali mfumo wa vyama vingi? Ilikuwa mbinyo mkali sana toka nchi wafadhili. Hizi propaganda wanazotoa magamba kuwa wao waliridhia mfumo wa vyama vingi, ni uongo wa hali ya juu, na ndiyo maana ingawa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, vyombo vyote vya usalama vinatakiwa visijiingize kwenye siasa, lakini hali halisi inajidhihirisha bila shaka yoyote kuwa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa, vyombo hivyo viwili vinatekeleza kwa asilimia 100, maelekezo ya kuminya vyama vya upinzani vinavyoonekana ni tishio kwa CCM, wanayopewa na watawala. Sasa na huyo Tendwa naye yumo kwenye huo mkumbo, na ndiyo maana hilo tukio haliwezi kushangaza sana, maana ni majuzi tu Tendwa alinukuliwa akisema kama Chadema wamesusa kufanya kazi na mimi, si wasuse na kuja kupokea ruzuku!!
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu
CCM 1.2billion
CHADEMA 233million
CUF 98million
Hata hivyo utaratibu wa kutoa hizi hela ofisi ya Msajili inahusika kwa sehemu ndogo sana kwa kuandika Voucher kwenda hazina ambapo hazina inahamishia fedha hizo kwenye account za vyama kwa njia ya kielectroniki wala hakuna utaratibu wa Cheque kama mtoa habari alivyosema. Pia ile Voucher huwezi kuandika chama kimoja na kuacha vyama vingine kwa SABABU YOYOTE ILE.
Pengine ingeelezwa kuwa serikali haina fedha kwa sasa ningeelewa kwakuwa ni ukweli kuwa vyama vyote havijapata ruzuku hadi jana.
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu
Huyu jamaa anapenda kubishana bila evidence. Hata kudhani kuwa Msajili siyo Mhasibu ameshindwa. Hata kukumbuka kuwa kasma ya kuendeshea nchi ambako ndiko fungu la kuendeshea Ofisi ya Msajili ni Tofauti na kasma inayotumika kulipa ruzuku zote nchini. Anajaribu kuwashawishi watu waelewe anavyotaka yeye. John Tendwa si Mhasibu na kazi yake ni kutoa Voucher ambazo zilishaandaliwa zina list ya vyama vyote.
Deus F Mallya, uwe tayari kusahihishwa katika hili ulilotamka.
Utaratibu wa Msajili wa vyama vya siasa ni kupeleka voucher za madai ya ruzuku hazina. Hazina ikishaandika hundi zinarudishwa kwa Msajili wa vyama vya siasa. Yeye ndiye mwenye kutia sahihi hundi hizo kabla ya kuwakabidhi wahusika. Bila sahihi ya msajili wa vyama vya siasa hundi hizi zikipelekwa hazina kuchota kilicho chao vyama vya siasa haitakubalika.
Kwamba Tendwa amekalia hundi hizo za vyama vya upinzani si jambo la kupinga, ila inawezekana ni mchezo wa rafu za Tendwa kuitishia nyau Chadema.
Deus F Mallya hundi zinazotoka serikalini zina utaratibu huo si vyama vya siasa tu, labda hujawahi kupata hundi za malipo toka hazina zisizohusu mishahara. Check za malipo toka Hazina hata ukiishaishika mkononi haina nguvu ya kuchukua pesa mpaka ofisa mwandamizi mwidhinishaji umpelekee amwage wino. Nakubaliana na mleta hoja. Mimi mwenyewe mwaka huu nilishikishwa adabu nilipopata hundi yangu toka hazina nikafiri pesa ninayo tayari, lakini nipoenda pale bank nikaambiwa kazi bado niende kule kwa ofisa fulani mwidhinishaji amwage wino ndipo niirudishe bank kupata kilicho changu. Nilipofuata utaratibu wao mambo yalienda shwari.
Wanajamii forums tusijenge ubishi wa kutumia akili bila kujua taratibu za mhimili wa serikali unavyofanya kazi katika idara ya pesa kuhakikisha malipo yanamfikia mhusika.
Ninavyowajua Chadema wangeyimwa cheki ya ruzuku lazima wangetoa tamko au kuitisha maandamano nchi nzima.