Tanzania: Vyama vya upinzani vyanyimwa ruzuku Rasmi

Bado nangoja mwenelezo wa darasa hili!.
Wakuu tiririka zaidi ili niweze kuelewa nielimike.

Huyu jamaa anapenda kubishana bila evidence. Hata kudhani kuwa Msajili siyo Mhasibu ameshindwa. Hata kukumbuka kuwa kasma ya kuendeshea nchi ambako ndiko fungu la kuendeshea Ofisi ya Msajili ni Tofauti na kasma inayotumika kulipa ruzuku zote nchini. Anajaribu kuwashawishi watu waelewe anavyotaka yeye. John Tendwa si Mhasibu na kazi yake ni kutoa Voucher ambazo zilishaandaliwa zina list ya vyama vyote.
 
siku zinakuja wazee wenye element za tendwa wanataishi uhamishoni maana wanatumiwa kabla ya ktumikia wananchi na jamii kwa ujumla bila kubagua wanatoka mlango gani wa kisiasa
 
Wewe kamwe huwezi kuchangia mtu. Najua hata watoto wako muda mwingine unaweza kuwalaza na njaa!

aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu
 
Kibacha na Deus F Mallya... tunachotaka kujua Chadema wamepata ruzuku yao? arguments nyingine sio mahali pake hapa....

Siyo Chadema wala Cuf ama Nccr, ila hawo wengine ni chambo tu. Chadema haijalipwa, huyi Deus F Mallya anataka kututoa kwenye hoja na kutupeleka anapopajua yeye.
 
Last edited by a moderator:
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu

Tutaendelea kuchanga, tumaini letu la mabadiliko ni hilo, subject hapa ni ruzuku siyo mchango, kunywa uji wa mhogo unasaidia kuboresha akili na kuchanganua mambo. kama kweli ulikuwa unachanga ni kwa utashi wako hukuwekewa bastola mdomoni kwamba ni lazima uchange.
 
Huyu jamaa anapenda kubishana bila evidence. Hata kudhani kuwa Msajili siyo Mhasibu ameshindwa. Hata kukumbuka kuwa kasma ya kuendeshea nchi ambako ndiko fungu la kuendeshea Ofisi ya Msajili ni Tofauti na kasma inayotumika kulipa ruzuku zote nchini. Anajaribu kuwashawishi watu waelewe anavyotaka yeye. John Tendwa si Mhasibu na kazi yake ni kutoa Voucher ambazo zilishaandaliwa zina list ya vyama vyote.

ndugu usishangae maana kunawatu wabishi kama nini hawajui ila wanajifanya wanajua au wanabisha bila vielelezo vya kwa nini wanabisha. watu kama hao nikuachana nao maana hata tuwaeliomishe naman gani ni kazi bure
 
Nimeandika hapo juu Mkuu. Hadi jana Vyama vyote havijapata ruzuku. Pengine tuambiwe ni Ukata Serikalini.
Naomba Chepe iwe Chepe tusiite Kijiko, Tendwa ana udhaifu wake lakini kama hajafanya kosa la kuipa CCM ruzuku yake na kuwavima vyama vingine, au hana huo uwezo basi tusimzushie.
Tuwekane wazi hii kitu imetokea au ni kutafuta idadi ya Topic humu JF?.
 
Udhaifu wa Tendwa na Ubovu wa maneno na maamuzi yake havipingiki. Ila inapoletwa hoja ya kisera na kimuundo ikiwa imebetuka kiasi hiki inatutia aibu kuwa hata pengine hatujui muundo na utendaji wa kazi za serikali inayoongozwa na rais kikwete ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi.
 
Unajua Deus F Mallya usitake tukubali ama tuseme nyeusi ni nyekundu, Huu ndiyo ukweli kuwa CCM wameshachukua chao kama unabisha waulize, then nimekuambia cheki bila saini ya tendwa haitoki, mambo yote ya taarifa za vyama huchukuliwa pale, ule ni muhimili mwingine baina ya serikali na vyama vya kisiasa, acha ubishi usiyokuwa na tija mkuu, ninauzoefu na ofisi hii sasa najua kila kinachoendelea kinachotakiwa kufanyika kwaajili ya kuhujumu nguvu ya vyama vya upinzani hususani CDM, si mbebi mtu bali nimeeleza kile ninachokijua na ninachokiona kila siku.
 
Haya yote yana mwisho, wala siyo mbali. Mabadiliko hayaletwi na pesa, bali watu, hasa walioathirika na mfumu uliopo. Kumbukeni mwavuli hautumiki kukwepa athari za kimbunga.
 
Udhaifu wa Tendwa na Ubovu wa maneno na maamuzi yake havipingiki. Ila inapoletwa hoja ya kisera na kimuundo ikiwa imebetuka kiasi hiki inatutia aibu kuwa hata pengine hatujui muundo na utendaji wa kazi za serikali inayoongozwa na rais kikwete ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi.

Unajua Deus F Mallya usitake tukubali ama tuseme nyeusi ni nyekundu, Huu ndiyo ukweli kuwa CCM wameshachukua chao kama unabisha waulize, then nimekuambia cheki bila saini ya tendwa haitoki, mambo yote ya taarifa za vyama huchukuliwa pale, ule ni muhimili mwingine baina ya serikali na vyama vya kisiasa, acha ubishi usiyokuwa na tija mkuu, ninauzoefu na ofisi hii sasa najua kila kinachoendelea kinachotakiwa kufanyika kwaajili ya kuhujumu nguvu ya vyama vya upinzani hususani CDM, si mbebi mtu bali nimeeleza kile ninachokijua na ninachokiona kila siku.
Hili jambo yafaa lipate maelezo vizuri:-
1. Tendwa anaweza kuzuia ruzuku ya chama cha siasa?
2. Utaratibu wa malipo ni wa cheki au vocha?, Kwa sahii ya nani?
3. Utaratibu unafanywa kwa ujumla au ni kwa chama kimoja kimoja?
4. Je kama inatokea Tendwa anaweza fanya No. 1 Utaratibu gani unafuata kwa chama husika?
 
Back
Top Bottom