Poulsen: hana jipya kwa Starz, tangu akabiziwe timu kiwango kinazidi kushuka, kuna haja ya kuachia ngazi si mpaka aundiwe tume.
Binafsi pia sijaona lolote la muhimu lililoletwa na Poulsen....
Ni kwa nini kamuweka bench Victor Costa?,
Ni kwa nini hakumuanzisha Mrisho Ngassa?.....
Ni kwa nini amemtoa Shaban Nditti ambaye alionesha kuelewana vizuri sana na Henry Joseph kiasi cha kuleta uhai pale kati?...
Mechi ya leo ilikuwa ni rahisi sana kwa Stars,tungeweza kushinda hata kwa magoli matatu kama sio manne....Victor Costa ni beki ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa lakini kocha kamuweka benchi na kuwaanzisha Nyosso na Aggrey na sote tumeona uzembe wa Nyosso na Nsajigwa ndio umepelekea Algeria wasawazishe goli,Nyosso kachelewa kuruka hivyo kumpa nafasi mchezaji wa Algeria kufunga goli....Ifikie kipindi Shadrack Nsajigwa apumzike sasa,awaachie vijana wacheze mpira....kawa mzito sana...
Pale katikati kulikuwa na maelewano amzuri sana kati ya Henry Joseph na Shaban Nditi na walikuwa wanapeleka mipira sana mbele kiasi cha kufanya Mbwana Samatta ang'are pale mbele lakini cha kushangaza kocha anamtoa Nditti na kumuingiza Machupa ambaye hajafanya lolote...Kutolewa kwa Nditti kumepelekea Abdi Kassim arudi kwenye kiungo cha kushambulia na Henry Joseph kucheza kiungo cha kukaba hivyo kupooza mchezo/kupunguza kasi ya mchezo.....Baada ya kutoka Nditti mipira mingi haijaenda mbele hivyo kumfanya Samtta asing'are tena kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza.....
Kule mbele Abdi Kassim na Danny Mrwanda walikuwa ni mzigo......Walitakiwa kutolewa mapema sana....Sijui ni kwa nini kocha alimuweka mchezaji kama Ngassa benchi....Sote tunamjua Ngassa kwamba ni mchezaji ambaye daima hutengeneza ushindi kwa timu ama kwa kufunga ama kutengeneza magoli..........Inaumiza sana.....
Namkumbuka sana Marcio Maximo.....Sijaona jipya lolote lililoletwa na Jan Poulsena wala Kim Poulsen tangu waje nchini......
Je kuna haja ya kurudi nyuma na kufikiri kwamba sasa ni wakati wa kuwapa timu aifa ya Taifa makocha wazalendo(akina Jamhuri Kihwelo,Dkt.Mshindo Msolla,Juma Mwambusi na wengine) badala ya kupoteza fedha za walipa kodi kwa makocha wageni ambao hakuna jipya lolote wanalolileta kwa Taifa letu????
Tafakari.....................Chukua hatua