Tanzania tusipokuwa makini Rwanda itatuaibisha

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
346
1,301
Ndugu zangu Watanzania wakati umefika sasa tuelezane ukweli kuhusu ujinga na dhana yetu ya kuichukulia 'poa' Kigali tukijidanganya kwa mambo mengi na ya kipuuzi.

Miongoni mwetu bado tunaidharau Rwanda kwa udogo wa eneo lake na wengine tukijidanganya eti Rwanda ni sawa na mkoa hivyo si lolote si chochote kwetu. TUNAJIDANGANYA SANA!

Ukweli ni huu; Kigali ni nchi inayotaka kutupita kwa mbio za kutisha kwenye mambo mengi hususani kwenye nyanja ya uwekezaji na TEHEMA.

Kigali kwa mfano wameendelea kuwavutia wawekezaji kwa sera rafiki na huwahakikishia usalama wao na mali zao na ndiyo maana leo eneo huru la biashara pale Kigali almaarufu FREE ZONE LINAENDELEA KUJAA VIWANDA VYA KILA AINA NA VYA KISASA.

Miundombinu ya barabara hakika Rwanda wamepiga hatua kubwa mno kwa mda mchache na hii haijalishi udogo wa nchi yao. Kuanzia Rusumo, Kamembe hadi Bugarama mpakani mwa Congo kote huko ni lami. Vilevile, Rusumo hadi Gisenyi kwenye mpaka wa Goma kote barabara ni nzuri na za kisasa!

Sekta ya afya ndiyo kipaumbele namba mbili cha bwana Paul Kagame baada ya Usalama. Vituo vya afya vya kisasa vimetapakaa hadi vijijini na vyote vikiwa na rasimali hitajiki zikiwemo gari za wagonjwa.

Upande wa usalama hakika ndicho kipaumbele namba moja kwa nchi ile! Uwapo Rwanda usalama wako ni asilimia zaidi ya 90. Asilimia 100 ya maeneo yenye muingiliano wa watu yanachangizwa na ulinzi wa mifumo ya TEHEMA. Pori kubwa la Nyungwe sasa linalindwa na camera (CCTV). Barabara zote kuu zina taa pasipo kujali umbali wake! Mfano kuanzia Rusumo sasa hadi Rusizi zaidi ya kilomita 400 barabara yote hiyo ina taa za BARABARANI.

Rwanda imewekeza kwenye majeshi yake kuliko sekta nyingine yeyote. PAMOJA NA UDOGO WAKE RWANDA NDIYO NCHI MAJESHI YAKE YANAONGOZA KWA MIFUMO YA TEHEMA KATIKA UENDESHAJI WAKE HAPA AFRIKA MASHARIKI!

Shime Watanzania tuache tena kuichukulia Kigali poa kwa sababu jamaa wanakuja na mwendo wa kutisha.

CDF mustaafu Mabeyo atakuwa shahidi na muumini wa angalizo langu hili kwa sababu aliwahi kuwa mwakilishi wetu (MWAMBATA) pale Ubalozini.

Tusiendelee kujisifu kwa ukubwa wa pua ilhali tunasahau ukubwa wa pua siyo uwingi wa kamasi.

Mungu ibariki Tanzania.

NB: Nimejaribu kuandika kwa ujumla pasi na kuweka takwimu ili wasioweza kuelewa mambo ya takwimu waweze kuelewa kirahisi.
 
Rwanda ataujipe miaka 30 haiwezi kufikia Tanzania, isipo kua wapiga debe wa Rwanda ni wengi hata humu jf kwa kujiita wa Tanzania, Rwanda naijua kama navo jua Tanzania ni promotions tu za Kigali neenda nje ya kigali hali ni ngumu kwa average myarwanda nchi yenýe GDP $12bn huwezi kuilinganisha na GDP$ 57bn, watu 60m kwa watu 11m.

Ndiyo maana mpaka leo Sweden haiwezi kuipita wa Faransa wingereza au italiano kwasbb wana wazidi gdp na market base. Rwanda itampita tu Burundi Malawi Somalia ila sio Tz Ky au Ug.
 
Yes una hoja ya msingi! Mimi nimecheka kwa nguvu niliposoma " ukubwa wa pua sio wingi wa SAMAKI"
 
Haya ndio maendeleo ya Rwanda anayosema mleta mada.
 

Attachments

  • Screenshot_20230626-140322.jpg
    Screenshot_20230626-140322.jpg
    69.1 KB · Views: 15
  • Screenshot_20230626-140400.jpg
    Screenshot_20230626-140400.jpg
    72.6 KB · Views: 14
Back
Top Bottom