Tanzania tunaweza tukalisha Robo ya Dunia kama yatafanyika Mapinduzi kwenye Kilimo

Tatizo ni hilo hilo la siasa uchwara. Kilimo hapa kwetu kimekuwa kinabadili tu kauli mbiu, mara kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni UTI wa mgongo, sijui kilimo kwanza na utapeli wa aina hiyo. Lakini ni rahisi zaidi kuwa masikini kwa kujiingiza kwenye kilimo kuliko pengine popote. Na wakulima wengi ndio masikini hapa nchini.

Kama huamini, nenda bank kakope hela ya kwenda kwenye kilimo, na mwingine akope anataka kufungua bar, uone nani atapewa mkopo haraka.
Ni kweli inahitajika mabadiliko makubwa kuanzia kwenye mtazamo, Sera na Mkazo wa uwekezaji. Amini tunaelekea huko, bank nyingi zilikuwa hazitaki kopesha wakulima, lakini leo kuna kila aina ya mikopo ya Wakulima
 
NAFCO...nakumbuka mashamba haya pia kule Mbeya maeneno ya Chimala, Rujewa, Igurusi ilikuwa chanzo cha ajira kikubwa, Serikali inaweza fufua mashamba haya. Bashe anaweza simamia hili
Hakuna suala la mashamba ya serikali hapa,
Watu binafi wapewe kivutio ili wawekeze kwenye kilimo kama akina Bakhresa, Mo na mabepari wengine ili wazalishe chakula kwa wingi wauze ndani na nje ya nchi.

Usisikie Marekani au Ukraini wanalima na kulisha dunia ujuwe si mashamba ya Umma bali watu Binafsi zaid .

Suala la Mashamba ya Umma ni kurudisha ushumi wa kijamaa uliokwisha kufeli.

Watu kikawaida huwa hawawajibiki vilivyo kwenye projects za Serikali, lakini za mtu binafsi hakuna cha mchezo.

Naunga nkono hoja endapo serikali itatilia mkazo Andishi hili

Kuwaunga mkono wakulima wakubwa na wale wa kati .Waachane na wakulima wadogo kabisaa ,Haiwezekani kila mtu akawa mkulima.

Hawa wakulima wadogo wanatia wingi tuu huku hawana mitaji ya kuendeleza kilimo wala ujuzi wala vifaa,

Wacha wakulima wadogo wafanyekazi chini ya Mabepari na wakulima wa kati.
Hii ndiyo maana ya kutengeneza Ajira na kukuza uzalishaji nchini.
 
Mkuu..ukiacha utani, Uchaguzi ukifanyika leo, CCM saa nne asubuhi wanachukua nchi. Achana na mambo ya mitandao nenda vijiji uone Shule, Vituo vya Afya, Zahanati, Barabara etc zilivyojengwa. Watanzania wanahitaji huduma za Jamii na zinatolewa
kwani wangalikuwa wapinzani wasingelifanya hayo?
Au CCM wanatumia pesa za chama chao kujenga miundo mbinu?
wacheni upoyoyo.
Maisha ya kipato cha mtu binafsi mitaani ndiyo muamuzi wa kura.
Watu wana njaa, hawana kazi, maisha yamepanda na kila siku vitu vinapanda bei ikiwemo mafuta na sukari.
Tunahitaji kula kwanza kabla kuumwa.
 
kabisa,hajabu serikali inawekeza pesa ndefu kwenye miradi ambayo kupata return ni zaidi ya miaka 50 au zaidi.

wakati pesa hizo zingeelekezwa kwenye kilimo&mifugo ndani ya miaka mitano tu uchumi wa kweli ungestawi.sio huu uchumi wa janjajanja wa kwenye makablasha.
Usijisahaulishe kuhusu BBT
 
Mnaongozwa na vilema wa akili na majitu yasiyo na maadili wala weledi wa uongozi halafu mnatarajia maendeleo
Hii nchi ni takataka na imejaa maiti wanaotembea na kuongea
Mna matatizo ya akili

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Ruvuma ,Mbeya , Morogoro ,Rukwa , Singida, Bukoba , Kilimanjaro sehemu hizo zinaweza kuweka mazao ya kimkakati watu wakafika mbali.

Unfortunately ,tunajenga makao makuu ya nchi kule Dodoma ,pesa zinaenda huko.
 
Tanzania ni moja ya Nchi Duniani ambayo imebarikiwa na kila kitu.

Tanzania imebarikiwa Madini ya kila aina, pongezi kubwa kwa Serikali na Wizara ya Madini kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi kwenye utafiti na sasa Madini adimu kabisa ya Lithium yamegunduliwa na utafiti unaendelea.

Tanzania tumebarikiwa ardhi ya kutosha, tumebarikiwa mito ya kutosha, maziwa, Chemchem za kutosha na bahari pia.

Kama yakifanyika mapinduzi ya Kilimo, zao gani ambalo halistawi Tanzania? . Mipango mikubwa ya Kilimo ipelekwe Njombe, Mbeya, Rukwa, Kigoma, etc, ili Kilimo cha kisasa chenye uhakika cha kutokutegemea mvua kikafanyike..

Pengine ni muda sahihi wa kuanza Mipango ya baada ya miaka 20 ijayo kutumia bahari yetu kwa Kilimo. Yes inawezekana, maji ya bahari ikawa chanzo cha maji ya kutumia majumbani, viwandani na mashambani. Kama imewezekana kufanya miradi mikubwa ya SGR, inawezekana kutoa maji ya Bahari kutoka Tanga kwenda Kigoma.

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Mtaala umejaa Arabic na Islamic na Divinity - Kilimo kitaishia kwa babu zetu.
 
NAFCO...nakumbuka mashamba haya pia kule Mbeya maeneno ya Chimala, Rujewa, Igurusi ilikuwa chanzo cha ajira kikubwa, Serikali inaweza fufua mashamba haya. Bashe anaweza simamia hili
Hapo Bashe kuweza kusimamia ondoa hilo jina ,hana uwezo huo,

Alichokifanya unakijua,

Kama ni uwezo keshaonesha , ameaanzisha mashamba!, sijui ni mashamba ama makambi ya BBI,

Akachukua vijana wako makambini huko mashamba i, wanachokifanya anajua mwenyewe na mabilioni yake,.

Nilishasema humu ,kama wana uwezo mzuri wa kufikiri,ni kuhakikisha wanaainisha maeneo yote hapa nchini , ni wapi mazao fulani yanastawi na mvua zipo , halafu kuwawezesha wakulima wetu hawahawa kwa miundombinu mizuri ya umwagiliaji,

Halafu wakulima hawahawa wapewe hayo maeneo hukohuko walipo, na serikali iwawezeshe kwa usimamizi (Mabwana shamba) wapo wengi ambao tumewasomesha na hawana kufanya, hawa hata serikali haina haja ya kuwaahili , wataajiliwa hukohuko na wakulima kwa kazi watayofanyia.

Mashamba kama ya kapunga Madibira na haya ambayo yapo karibu na Dumila , nimeyasahau majina , ndio mfano mzuri wa hiki ninachoelezea.,

Yalikuwa ni mashamba ya serikali sasa hivi wamegawana wakubwa wenyewe na kuwakodisha wakulima wadogo wadogo na hayafanyi chochote cha maana.

Mtoa mada , nataka kukuambia kuwa , kama sio makusudi kwamba serikali yetu haina mpango wa kuwainua wananchi wake , basi ujue hatuna viongozi wa kuwafikiri vizuri.
 
Hakuna suala la mashamba ya serikali hapa,
Watu binafi wapewe kivutio ili wawekeze kwenye kilimo kama akina Bakhresa, Mo na mabepari wengine ili wazalishe chakula kwa wingi wauze ndani na nje ya nchi.

Usisikie Marekani au Ukraini wanalima na kulisha dunia ujuwe si mashamba ya Umma bali watu Binafsi zaid .

Suala la Mashamba ya Umma ni kurudisha ushumi wa kijamaa uliokwisha kufeli.

Watu kikawaida huwa hawawajibiki vilivyo kwenye projects za Serikali, lakini za mtu binafsi hakuna cha mchezo.

Naunga nkono hoja endapo serikali itatilia mkazo Andishi hili

Kuwaunga mkono wakulima wakubwa na wale wa kati .Waachane na wakulima wadogo kabisaa ,Haiwezekani kila mtu akawa mkulima.

Hawa wakulima wadogo wanatia wingi tuu huku hawana mitaji ya kuendeleza kilimo wala ujuzi wala vifaa,

Wacha wakulima wadogo wafanyekazi chini ya Mabepari na wakulima wa kati.
Hii ndiyo maana ya kutengeneza Ajira na kukuza uzalishaji nchini.
Bashawi, kuwaunga mkono wakulima sio kuwapa pesa ili walime, ni kuwawezesha tu, kwa sababu tayali wanalima , na ukulima wao ndio ajira yao,

Na wapo wengi (65%) ni wakulima masikini,

Na sio kwamba ni masikini sababu ni wavivu au hawana mashamba, la hasha, wana mashamba na kila siku wanaenda mashambani kwao, lakini ukulima wenyewe ndio duni,.

Hivi kwa mfano mabilioni ya pesa yanayoingizwa kujenga yale majumba ya kawe pale,, kama yangeingizwa kwenye skimu za umwagiliaji, ni eka ngapi zingejengewa miundombinu, na wakulima wangapi wangefaidika,

Hivi ile kariakoo imejengwa na serikali au watu binafsi,?

Kama watu binafsi , kwa nini serikali ihangaike na kujenga majengo ya kupangisha dunia hii, kazi ambayo ingefanywa na sekta binafsi,.

Ushauri wangu kwa serikali,

Wezesha wakulima wadogo wadogo, wasaidieni kuboresha kilimo chao na kazi ya serikali vilevile iwe ni kuwatafutia masoko huko duniani.

Uwezo wa kuilisha dunia tunao.

Kilimo tukikipa msukumo kitatutoa, na wananchi wetu watapata ajira.,

Kama ni magari wazungu wameshaunda, kama ni ndege nazo wameshaunda, sasa hata kulima tu tunashundwa? Hili ni taifa gani lisilo kuwa dira ya wapi linatupeleka.,

Matrekta, makatapila, mapampu ya maji , yote tumeshaundiwa , sasa sisi tunashindwa kutumia hiyo ya mamitambo hayo kuboresha maisha , ni nini tunachoweza.
 
Tanzania haiwezi kulisha watu bilioni mbili, tuache kujidanganya.
 
Ruvuma ,Mbeya , Morogoro ,Rukwa , Singida, Bukoba , Kilimanjaro sehemu

hizo zinaweza kuweka mazao ya kimkakati watu wakafika mbali.

Unfortunately ,tunajenga makao makuu ya nchi kule Dodoma ,pesa zinaenda huko.
Ruvuma , Rukwa - mahindi
2- Mbeya, morogoro-
Mpunga
3-Singida,
Alizeti
4- Bukoba na kilimanjaro, kahawa na ndizi,
5- Kigoma
Michikichi
6-Kanda ya Ziwa yote
Mtama , Uwele,mifugo na Samaki,
7- mikoa ya kusini,
Ufuta, mbaazi dengu, kunde na samaki, na korosho,
8-Mikoa ya pwani yote - Matunda mbalimbali,

Tunashindwa nini?
 
Ile white elephant project ya Bashe iitwayo BBT vijana 100 leo wameingia mitini .

Yani mmeshindwa kusimamia kile ki mini project mtaweza mega project za kulisha robo ya dunia?

Lazima utakuwa unaota wewe.
 
Back
Top Bottom