Tanzania tunahitaji shopping malls?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kihistoria hizi shopping zilianzishwa baada ya wazungu wengi huko US kuanza kuishi nje ya mji (suburban). Hizi nazo zikawekwa maeneo ya huko.

Watu walifuata huduma hapo na magari na ndiyo kisa cha malls kuwa na parking kubwa sana. Kwa hiyi hizi malls huwa zinachukua eneo kubwa sana, eneo la jengo na parking.

Zilijengwa ili kutokana na utamaduni wa hao jamaa. Pia hawa jamaa utamaduni wao ni kununua vitu vya wiki nzima sisi ni kila siku au kila mlo tunaenda dukani/sokoni na sidhani kama wanayo masoko kama sisi huku. Temefautiana sana utamaduni.

Nilisikia mji wa Mbeya wanataka kujenga Mall katikati ya CBD! Hizi mall ni kweli tunazihitaji au tunajenga kwa kuiga bila kuangalia wenzetu walijenga kwanini!?

Nyie wakuu mnaonaje, kweli tunahitaji hizi mall au hutu tu strip mall(fremu) na masoko yanatosha?
 
Maendeleo tunayahitaji kwa namna yoyote ile, kila kitu useful kilivumbuliwa kutibu tatizo fulani katika jamii fulani. So wacha wajenge tu
 
Maendeleo tunayahitaji kwa namna yoyote ile, kila kitu useful kilivumbuliwa kutibu tatizo fulani katika jamii fulani. So wacha wajenge tu
Mdiyo maana wazungu wanaishi nje ya miji wakaona wawe na malla kama sehemu ya kufanya shopping. Sisi tunajenga kutibu shida gani?
 
Inabidi uelewe mteja mkuu wa malll ni nani?

Mteja mkuu wa Mall ni mabenki.

Mabenki mengi hayapendi kujenga jengo mradi kufungua branch tu

Na kuna wilaya nyingi Sana na hata mikoa

Ambako hakuna kabisa jengo linalofaa Kwa benki kuweka branch

Hadi imefikia bank kama Nmb inajenga majengo yake huku haipendi.

Imefikia baadhi ya benk zina branches nyingi dar na hazina branch kabisa mikoani.

Mall inaweza accomodate banks kadhaa

Na maofisi kadhaa kama TRA n.k.

Tanzania bado inahitaji sana malls hasa kila wilaya
 
Mie ntaendeleaza katabia kangu ka kukopa unga, wine, bia, mafuta ya kupikia kwa mangiii manake amekuwa akinipa mkopo adi mshahara unatoka.

Mangi hoyeee.
 
450908765.jpg
 
Kuna mtu alisema dunia ilipofikia/inapoelekea sasa hivi siyo tena muda wa kujivunia kuwa na malls nyingi maana siku hizi habari ya mjini ni online shopping
Hii nayo ni point nzuri sana. Online shopping inakuja kwa kasi. Haya ma Mall yatakuwa hayana maana tena.
 
Kwasisi tusiopenda shida tunahitaji shopping malls tukihitaji vitu twende tukanunue bila kero za kukosa parking, tukiwa tumependeza watushangae huko masoko uchwala, tukinunua sana mifuko ikajaa watushangae kumbe ni shopping ya mwezi pia usalama wa eneo, pia bidhaa zilizoongezwa thamani zitapatikana imagine Mchele uliochambuliwa, maharage yaani nikununua nakupika yaani tupate sehemu ya watu tunaopenda maisha ya kisasa.
 
Hii nayo ni point nzuri sana. Online shopping inakuja kwa kasi. Haya ma Mall yatakuwa hayana maana tena.
Hata huko kwenye mall wanaweza kuweka kitengo cha online shopping kwa kuweka bidhaa kwenye mtandao mtu akipenda anapelekewa.
 
Kihistoria hizi shopping zilianzishwa baada ya wazungu wengi huko US kuanza kuishi nje ya mji (suburban). Hizi nazo zikawekwa maeneo ya huko. Watu walifuata huduma hapo na magari na ndiyo kisa cha malls kuwa na parking kubwa sana. Kwa hiyi hizi mall huwa zinachukua eneo kubwa sana, eneo la jengo na parking.....
Kwenye mall kuna maduka ya nguo, huduma Za kibenki,migahawa,cinema,kumbi za mikutano /shughuli mbalimbali ,super/hyper markets,maduka y vito nk. ...

Sasa jiulize unahitaji mall au auhitaji
 
Kwenye mall kuna maduka ya nguo, huduma Za kibenki,migahawa,cinema,kumbi za mikutano /shughuli mbalimbali ,super/hyper markets,maduka y vito nk. ...

Sasa jiulize unahitaji mall au auhitaji
Saa hizi tunapatq wapi hivyo vitu?
 
Back
Top Bottom