Tanzania tuna vyanzo vingi vinavyoweza kuzalisha nishati ya uhakika na ya kujitosheleza

AndyMJ

New Member
May 19, 2023
1
0
Hapa Tanzania tuna vyanzo vingi tunavyoweza kuvitumia vizuri ili kupata nishati ya uhakika na kutosheleza mahitaji yetu lakini kila mwaka na kila awamu ya uongozi ni kama wanaanza upya kutatua changamoto ile ile iliyokuwepo tangu miaka ya 70.

Binafsi hoja yangu ni uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo. Mikoa 2 ninayoijua hapa Tanzania (kuishi na kukulia) ina wastani mzuri sana wa upepo unaoweza kuzalisha "clean and sufficient energy". Singida na Dodoma wana wastani wa upepo unaovuma kwa kasi ya 10 -12 mile per hour kutoka April hadi November na miezi michache kasi hupungua lkn bado ni ina nguvu vile vile.

Sijajua kwanini mpaka leo serikali haijawekeza kwenye hili.
 
Back
Top Bottom