Ahsante saana wakuu kwa mada hii murua. Ni katika suala zima la kuongoza au kutawala. Mabadiliko yoyote katika jamii yanatokana na siasa amabayo ni safi na uongozi bora. Nataka nitoe mfano wa nchi ya china. Anayepewa contract husaini mkataba,lakini ikitokea likatokea lolote kama kula fedha kabla ya kitu alichopewa kufanya hakikuisha na hakipo kwenye kiwango knachoridhisha,serikali hutaifisha mali ya yule mtu yote na isipotosha inaingia kwa wana familia pia,hivyo mtu akionyesha wizi,hata kabla serikali haijamshtukia basi wan familia wana wajibu wa kutoa taarifa ili likitokea la kutokea awajibishwe yeye kama yeye.
Turudi nyumbani, mimi ni mtanzania halisi. Tanzania ni tajiri kuliko hata nchi za ulaya nyingi tu,umaskini wetu ni namna tunavyotumia raslimali zetu tulizonazo. Na hii ipo mikononi mwa viongozi wenye madaraka serikalini.
Tumekuwa na watawala,wanaojiangalia wao bila ya kuwa na uchungu na nchi na maisha ya watu duni kwa ujumla, Watu vijijini bado wankosa sh 100, hamuwezi kuamini lakini huo ndo ukweli,utadhani hatujapata uhuru.
Nafasi ya kiongozi ni kuleta mamabdiliko katika jamii anayoiongoza na hivyo maendeleo hupatikana.
Hatuna watu wenye uchungu na umaskini wa nchi yetu,wao wanaangalia miradi yao kama inaendeshwa vyema au la. Nasema hivi kwa sababu hawana muda wa kujua hata matatizo ya wananchi wao ni yapi na wawasaidieje? Wanasubiri uchaguzi wakawanunulie pombe,baiskeli,magodoro, na mambo mengine mengi.
Mabadiliko hayategemei historia iliyopo na iliyokuwepo,huwezi kusema kwa kuwa baba yako hakujenga nyumba ya tofali na wewe kama mtoto huwezi kuijenga hata ukiwa na fedha. Huku ni kudidimia kwa fikra,inawezekana yeye hakuona umuhimu kwa wakati ule. Ninacotaka kusema hapa ni maendeleo na mabadiliko,tuangalie tuko wapi na tunataka nini ili tufike wapi,c kuangalia waliokuwepo mwanzoni walifanyaje, na sisi ndo tufuate mtindo uleule.
Naamini tukiwa na viongozi waadilifu basi yote yanawezekana.