Tanzania tuna: Viongozi, Watawala au Mabwana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tuna: Viongozi, Watawala au Mabwana?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Mar 18, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Unapotafakari hatima ya Taifa letu na mwelekeo wake, kuna jambo ambalo linaongoza na kutawala mawazo na kauli zetu, suala la Uongozi Bora na Siasa Safi kama tulivyoapa katika Azimio la Arusha.

  Najiuliza kwa kutumia watu wafuatao katika kujenga kwangu hoja, Mkapa, Kikwete,Migiro, Seleli, Karume, Lowassa, Ole Naiko, Mattaka, Kilewo, Zitto, Nyang'anyi, Mukandara, Mrema, Cheyo, Tibaijuka, Rostam, Kawawa, Dewji, Mengi, Ulimwengu, Pengo, Mwalasusa na wengineo.

  Nimeweka mkorogo wa wanasiasa, wafanyabiashara, watu wa dini na watanzania ambao kwa ujumla huwa ni maarufu katika habari, ikiwa na maana wana nafasi fulani inayokuwa na wafuasi kama si washabiki.

  Kwa kuangalia mkorogo huu na kuangalia dhana yetu ya kujijenga kama jamii iliyokomaa na endelevu, swali langu laja; Je Tanzania tuna Viongozi, Watawala au Mabwana?

  Maana sielewi ni vipi kuwa mpaka leo tunazunguka kama pia bila mwelekeo na kuna kuwa na mvutano mkubwa ambao unatishia kumegua Taifa letu katika vipande vya tabaka la uwezo kimali kati ya walionazo na wasionacho, mvurugano wa kidini, kikabila, kielimu, kijinsia, kiumri na kiitikadi.

  Inakuwa kana kwamba Watanzania hatujui tupate wapi hamasa au mvuto wa kutuongoza. Tunakuwa kama kondoo au mbuzi waliopotea malishoni na kuendelea na safari kutafuta nyasi na maji hata pamoja na kuwa jua limechwea na ni wakati wa kurudi zizini!

  Ni nini kinachotukabili Watanzania kuwa tunakosa dira ya kujituma tuwe mahiri wenye juhudi, maarifa, uadilifu, utu, hekima na busara?

  Ikiwa tuliwapa dhamana kutuoongoza katika Serikali, Mashirika, Taasisi, Jumuiya, Mashule, Nyumba za ibada na hata mitaani na majumbani hawana mwamko au mwelekeo wa kuwa Viongozi wa mfano bali wao ni Watawala na Mabwana, je kuna salama ya huko tunakokwenda?

  Cheo hakina maana ya mtu kuwa mtemi, mnyapara, mwenye nguvu, amri au manufaa binafsi, bali ni wajibu mkubwa unaotokana na cheo, ndio unaoleta maana ya mtu kuwa na cheo.

  Sawasawa na Uongozi, uongozi ni dhamana, kama tulivyosema "cheo ni dhamana"!

  Uongozi si maneno na kauli tuu, bali ni vitendo na nidhamu ya hali ya juu inayoandamana na umakini, busara, uadilifu na wepesi wa kuwa msikivu na hata kuvumilia kubezwa na wafuasi.

  Ukiangalia na kupembua matatizo ya Watanzania na Taifa letu, utabaini kuwa kuna ukosefu mkubwa wa Uongozi ambao unajua maana ya uongozi; kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu na wenye nidhamu, kujali walio chini, kuwa wenye maono ya mbali na kutafuta njia bora za kutatua matatizo na si kukimbilia viraka.

  Kila siku ya Mungu tunapoamka, kuna habari moja kama si mbili ambayo inahusu kuyumba na kukosekana kwa uwajibikaji na Uongozi kutoka kwa wale ambao wanafikirika kuwa ndio viongozi wetu katika jamii.

  Nenda Bungeni, Serikalini, Mashirikani, Makanisani, Shuleni, Mijini, Vijijini na hata Majumbani, kuna udhaifu mkubwa sana wa Uongozi ambao ndio msingi mkuu wa Ustawi wetu kama jamii na Taifa.

  Fungua gazeti lako leo, utakutana na habari za kusikitisha, ajira hakuna, ubadhirifu, ufujaji, kukosekana maadili, ubabe, dharau, vitisho, kubeza, amri na kila aina ya Udikteta alimradi mtu anatumia misuli ya shingo na kutunisha kifua kuonyesha kuwa yeye ni Bwana Mkubwa!

  Zimekwenda wapi Busara, Hekima, Ufanisi, Uwajibikaji, Hamasa, Unyenyekevu, Usikivu na hata Upendo?

  Iweje tangu tujitawale kwa kupiga vita ukoloni na uonevu na hata siasa za Kibeberu, leo hii tunakubali kuburuzwa na Watanzania wenzetu ambao ni Watawala na Mabwana na si Viongozi?

  Tunapokwenda kwenye uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa, diwani na meya tutakayemchagua tutampa mamlaka awe Mtawala, Bwana na Mnyapara au ni ndugu yetu tunayemuamini kuwa anajituma na kujitolea kutumia hekina na busara kutuongoza na kutetea haki zetu?

  Na hata mwakani tutakapoanza kutafuta Wabunge, Wawakilishi na Marais wa Muungano na Zanzibar, tuko tayari kuanza kuwapima wanaotaka nafasi hizo kwa kuangalia kama kweli wana uwezo wa kuongoza au tutajinyong'onyea kwa unyonge na kuruhusu kutawaliwa na Mabwana Wakubwa ambao wao ni Mwanzo na Mwisho wa kila kitu na sisi hatuna hata sauti moja au kauli ila ni kusema "ndiyo mzee", "ndiyo bosi" "ndiyo mkubwa" na kuwa na nidhamu ya woga badala ya kuwa na heshima na kutembea kifua mbele tukijigamba kuwa tuna Viongozi wachapa kazi wenye kujali maslahi yetu kama Jamii na Taifa?

  Je kizazi cha mababu zetu, mababa zetu na hata chetu cha sasa, hakina hata watu kumi ambao wanaweza kuwa na mfano chanya wa maana ya uongozi na hivyo kuliondoa Taifa letu kutoka unyonge wa kuwa watumwa na kunyanyaswa na kupuuzwa?

  Hivi kweli ndani ya Bunge, hakuna watu weye Busara kumi ambao wanaweza kulonga na Bunge zima likaafiki kufanya mambo ya Busara na Hekima na si Ushabiki wa Pwagu na Pwaguzi?

  Je kwenye bodi za menejimenti, hakuna wajumbe wenye msimamo na kauli ambao wanaweza kusimama kidete an kusema "hapa tumekosea" "lile halikuwa sahihi" "matumizi haya hayana manufaa" nao wakazikilizwa na kuheshimiwa na hivyo shirika, taasisi au jumuiya ikaonelea kuwa kuna umuhimu wa kujirudi na kujisahihisha?

  Je tuende kuazima Viongozi kutoka kwa Wazungu, Warwanda na Wachina?

  Ni lini tutaanza kuzalisha uzao wa Viongozi wenye maono, wachapakazi, jasiri, wabunifu, fanisi, wanyenyekevu, waadilifu, wakweli, wasiopenda makuu na wenye kuelewa maana ya Uongozi na umuhimu wa kuhamasisha na kutetea haki za jamii zao na si kujifikiria wao kwanza?

  Mwisho, kwa walio madarakani, je wanaelewa kuwa mafanikio yanatokana na ushirikishi na kuaminika kutoka kwetu sisi Wananchi? Ikiwa Walioko juu tunaowaita Vigogo, Vibosile, Wakubwa, Pedeje, Wanene na Wenyewe hawatambui kuwa sisi tulio chini tuliowapa dhamana ya kuongoza ni muhimu na tuna thamani, kuna faida gani kuendelea kuwa na watu kama hao wanaodhani wao ni Miungu watu na kuwa Uongozi wa Taifa na Jamii yetu ni Urithi wao wa milele au hakuna mwingine zaidi yao?
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Watwana, mbona mko kimya? au ndivyo tulivyo tumesalimu amri?
   
 3. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Bado tunasoma, mchungaji maana hoja yako ni very serious.... nitarespond soon....
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Very serious!
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naweza kusema kuwa tuna watawala wanaopenda na pengine wanaolazimika kuwa viongozi ama mabwana.

  omarilyas
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,815
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Rev Kishoka:

  U need to un-learn. Siasa safi za Azimio la Arusha is a big hoax.
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Rev Kishoka, kwanza salamu!
  Mimi naamini ya kuwa hapa ni lazima turudi katika chanzo, kwani taifa ni kama binadamu kuna kipindi bado ni changa, alafu anakua na kuwa teenager then a country matures. Lakini life span ni kubwa zaidi kama tunavyofahamu.
  So mi nachukulia sisi bado ni watoto and we suffer from growing pains. Lakini tukichukulia mfano wa nchi mature ambayo pamoja na makosa mengi bado imekuwa nchi iliyoendelea na imara - Marekani - tunaweza kuona tofauti ya kipindi kile kichanga cha Marekani na Tanzania.
  Huko Marekani waliwatimua waingereza kwa vita na kwa mapigano halisi. Sisi tulipewa uhuru na waingereza baada ya Nyerere kuonekana as no real threat na pia Uingereza kutokuwa na real interest in Tanganyika as much as in Kenya.
  Hivyo basi, wamarekani ilibidi wamwage damu kupata uhuru wao, sisi tulilala tukaamka tukapewa. Naomba hapa nitoe heshima zote kwa akina Chifu MKwawa na akina Kinjekitile na wengine ambao walitoa resistance ya kweli dhidi ya ukoloni.
  Getting back to the analogy of a child, nchi yetu huru ilihitaji walezi. Wanasema ya kuwa viongozi wa awali wana nafasi kubwa sana ya ku-shape the future, lakini muhimu zaidi they set the standard for leadership. Ukiangalia marekani hawana Founding father Moja! in fact ni group of people with competing intrests ambao walijifungia chumbani na ku-debate ideas hadi walipofikia compromise. Na matokeo ya hayo ni constitution of the US which is truly a great legal document. In fact George Washington hakuwa sana part of this process hivyo hata katika group ya Founding fathers akina Hamilton wana-play a bigger part.
  What happened with Tanzania is that we subtitute the paternalistic utawala wa kikoloni with.... personality cult. We call Nyerere out founding father. We have purged out of history the others who worked with Nyerere. And who engineered that? Of course we know, Nyerere himself.
  So apart from many good personal characters, let us look at the first image of leadership that young Tanzania got from Nyerere:
  - He did not tolerate dissent
  - he dispensed his goodwill based on his personal likes and dislikes, there was no meritocracy. How can we justify a prime minister like Kawaw? There were many intelligent bright young men who could have become great prime ministers, but Nyerere did not want to be outshone. He gave postitions based on personal interest
  - He continued to influence the selection of the top leaders until his final years. He didn't allow for natural competition to occur.
  So what has this resulted in? Tanzanian leaders were used to looking for this all mighty power (sorry for the pun) who will make decisions and tell them what is right and wrong. This omnipotent force was Nyerere and that is why when we are lost we still turn back to him.
  But the truth is, he did not have good leadership skills in a democratic sense. Nyerere alikuwa mtawala wetu siyo kiongozi. Aliwahi kushindana katika multi party elections? Aliwahi kushindwa katika kura na ku-conceed defeat? When he was ready to owe up that he made a mistake he did so at his own terms and never tolerated public criticism from anyone within the country
  Naomba niweke wazi personally I have great admiration for Nyerere but objectively as a leader he failed.
  And it is in this reflection that Tanzania started its new life as an independent country.... (itaendelea)
   
 8. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  After setting the mold of leadership let us look at the next set of leaders and the present set of leaders:
  - President Mwinyi - handpicked by Nyerere - never competed in multi party elections
  - Prez Mkapa - handpicked by Nyerere over other competitiors - unfair disadvantage vis-a-vis young opposition parties
  - Prez Kikwete - started his career by being handpicked by Nyerere as junior minister and later used Nyerere as the person who basically 'baptized' him into leadership, went to get the 'blessings'of Mama Maria etc. but because he didn't have Nyerere, he and his cronies had a back up plan through corruption.
  Why did the actual corruption na ufisadi get out of hand after Nyerere's death, because it was always there. Nobody believed in Ujamaa. They just sing the praises of Nyerere because they crave for the same personality cult and following that he had as president. They want to be like their Father. Na ndo maana nasikia kichefuchefu wakati opposition party inataka kufananisha viongozi wake kuwa ni kama Nyerere. Personality cult is a dangerous thing na inawapa nguvu kubwa viongozi.
  If we look at the lower level, wengi wa viongozi walikuwa wateule wa Nyerere, at a lower or higher level. Sasa akili yetu imeshazoea that Nyerere is a saint kiasi kwamba eti mtu kama aliwahi kufanya kazi na Nyerere kama Chiligati au Pinda, basi hicho ni kigezo kikubwa na pekee kinachom-qualify. Inasikitisha kwa kweli.
  Dawa ya kupata viongozi wa kweli ni sisi watanzania kuondokana na hii cult ya kumwabudu Nyerere and talk about the huge mistakes he made, how he got us into this mess that we are in, kwa sababu kama marais wote wameingia madarakani kwa mgongo wa Nyerere basi tukubali amecheza part kubwa kutufikisha hapa.
  Hatuhitaji ujamaa au Nyerere tunahitaji kuwa free from personality cult and utopia.

  Na Viongozi wetu wanaogopana na hawako tayari kuwa wawazi na kukemea hadharani kwa sababu wajibu huo alikuwa nayo Nyerere peke yake. Nobody else could criticise.
  Mimi nimefurahi kuona kuwa JF kuna debate ya kweli na hatukubali cult or following ya Zitto au Mwakyembe au any politician.

  Na hivyo basi tupo wasomi na wananchi ambao tuna moyo na nchi yetu lakini kutokana na reflexes zetu (tumeshaanza kukomoa na si watoto wachanga tena) tunaogopa ku-criticize kwa kutumia majina yetu halisi - kwa kuwa somewhere bado tunategemea kuadhibiwa kwa kufanya hivyo. Pia kundi letu halitaki kujihusisha na siasa kwani hatuko tayari kuimba sifa za Nyerere au whoever. Siku Bunge litakapopitisha sheria ya uchaguzi ya kuruhusu wagombea binafsi mbona wengi tutachukua fomu! That is when we will see real leadership emerge and the healthy competition of ideas.
  Watanzania wana shauku ya kupata kiongozi (si mtawala) bora lakini chaguo lenyewe ni very poor. Na yote haya yamefanywa na wafuasi wa Nyerere ambao wanataka kuendelea kushikilia madaraka!
  Kwa leo nimemaliza Rev Kishoka!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nyerere has been out of power since 1985. He has been dead since 1999. In Rwanda Kagame came to power in 1994. He has done wonders to change the character of that small nation. And that is just in a matter of 15 years. So for me to blame Nyerere even now in 2009 for lack of leadership or vision in Tanzania is disingenious at best. We need a leader who will show us by action that Nyerere was wrong, that we can build a better Tanzania. Mpaka sasa hakuna. Na hilo tumlaumu Nyerere?
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  kwi kwi kwi, naona tunagombea hii konflikti ya interest na hatuna mwelekeo!
   
 11. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida ya sisi Watanzania hii ni blah.. blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
  blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
  blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah nyingine kutoka kwa Kishoka.......
  Swali.... umefanya nini kuondoka na hiyo hali????????????????? Au unalia na kulalamika tu...blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
  blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
  blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Blah blah blah Mungu akubariki blah blah blah!
   
 13. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Rev. mimi kwa sasa hivi ninadhani mtu ambaye anakosea ni Raisi Kikwete, kwa sababu yeye ndio anayeteua viongozi wengi mf wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mawaziri na wengine wengi, sasa kama yeye hachagui vizuri hatuwezi kufika popote na uzuri anajua kabisa kwamba nchi imebadilika na anatakiwa kubadilika nayo.
  Kitu kingine ni kwamba as long as chaguzi zitakuwa influenced by money hali hii itaendelea tuu. Kwa sababu kama watu wananunua uchaguzi maana yake watataka walipie gharama yao waliyotumia kwenye uchaguzi.
  Kitu kingine ni njaa, mtu mwenye njaa atakubali apewe chochote ili akuchague (Mwenye pesa akipita watu woote husimama na kila analolisema watu hulipa uzito) nimetoa kwenye wimbo na elimu piaa ni muhimu bila elimu hatuwezi kufika popote maana kama watu hawana elimu ni raisi kuwadanganya.
  Nimependa jibu la Jasusi kuhusu kumsingizia Nyerere ingawa Sisivuri ana point. Tuna safari ndefu lakini tutafika tuu. Lakini inabidi wananchi ndio wabadilike sio viongozi (Maana viongozi ni matunda yetu) Tukishabadilika tutafika tuu.
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Rev. Kishoka, kwanza kabisa nikushukuru kwa thread nzuri sana. Thread hii inaweza kusaidia kutambua tulipokosea, tunapokosea na tutakapokosea, kabla ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

  Naungana na Susuviri katika tathmini yake ndefu na nzuri aliyoitoa kama mchango wake hapa. Ninapompongeza Mkuu Susuviri katika hilo, ningependa pia kuongezea matatizo makubwa aliyoyafanya Mwl. Nyerere (katika uongozi wa nchi hii wakati wake wa utawala), ikiwa ni pamoja na kuwa alituongoza in a "One-Man-show style" ambayo inaigwa na viongozi wengi wa nchi yetu, tangu Nyerere ang'atuke. Alipong'atuka ndipo alipoanza kuona madhara ya uongozi wake kwenye maatendo ya wengine waliomrithi.

  Wakuu wangu mimi ninailaumu zaidi Katiba yetu. Katiba ambayo iliundwa katika mfumo wa utawala wa Nyerere ambao ulimpa yeye peke yake nguvu nyingi za kutawala na kuamua mambo yote ya nchi hii bila kuzingatia kuwa, yeye hakuwa mtu wa kuongoza Taifa hili milele, na pia bila kuzingatia mabadiliko ya mahitaji ya Taifa yanayobadilika kila kukicha. Ili tuweze kupiga hatua kama ulivyozielezea kwa tamaa kubwa hapo juu, ni lazima Katiba yetu iundwe upya yote. Kuiunda upya haina maana ya kufuta kila kipengele cha Katiba hiyo, bali kuiweka iwe huru na kuzingatia uhuru wa Taifa na wananchi wake, na pia kuweka misingi bora zaidi ya utawala. Inatakiwa iwe ni Katiba inayotoa mwongozo sahihi wa kila jambo linalomhusu Mtanzania na hasa uongozi wa Tanzania. Inatakiwa irekebishe vipengele vinavyopingana (ugombea binafsi n.k) na kuondoa vile vinavyotoa uhuru na nguvu kwa mtu mmoja ama taasisi ya watu wachache (Rais, Spika wa Bunge, Tume ya Uchaguzi n.k).

  Nikirudi sasa kwenye uwezekano wa kuwepo kwa viongozi wenye uwezo na wenye nia thabiti ya kuleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu, nina imani kuwa watu hao wapo wengi sana ila system imewabana na hawawezi kufurukuta hata chembe. Watawala waliopo kwenye madaraka ni wale waliojiundia kikundi cha kuhakikisha maslahi yao yanalindwa bila kujali maslahi halisi ya Taifa. Ni vigumu na wakati mwingine ni hatari sana kupambana na nguvu zao kwani ni watu wasiojiamini, wasio na dira na waoga wa challenge zitokazo kwa wale wenye uwezo wa kuongoza (si kutawala).

  Tutaendelea kujadili.

  Sasa naomba nimjibu Mkuu Jasusi.

  Ukweli ni kwamba, Nyerere ndie mbunifu wa utawala wa nchi hii. Yeye ndie aliebuni/kushinikiza Katiba ya sasa, kuanzia ya chama kimoja na hata ya vyama vingi na pia alibuni na kusimamia maazimio yote (Azimio la Arusha, Musoma n.k.). Baadhi ya mambo aliyofanya Nyerere yalikuwa na manufaa kwa Taifa. Ila mengi yalikuwa na hasara kwa Taifa, hasa kwa kuwa aliyafanya bila upinzani wowote wa kimtazamo na mawazo. Kumbuka Abdurahman Babu, Kambona na wengine walioonyesha kutokubaliana nae walivyolazimika kukimbia nchi na kuitwa wahaini.

  Utawala wa sasa haujabadilika sana na ule wa Nyerere. Itahitaji kiongozi mwenye nia njema sana na nchi hii kubadili system iliyopo ambayo wengi wanajua haifai kwa utawala wa nchi wa wakati huu. Ila inawafaa wao kuendelea kutawala kwa njia wanazotaka wao.

  Mfano wa Kagame wa Rwanda ni tofauti sana na hali tuliyonayo sisi sasa hivi. Kagame ali-suffer kama sisi kabla ya kuangushwa kwa serikali ya Juvenary Abyerimana ambae alikuwa mtawala wa nchi hiyo. Ilibidi nchi ichafuke na damu nyingi kumwagika ili kufikia walipofikia sasa. Sisi hatuhitaji kufanya hivyo, kwani thamani ya utu ni kubwa kuliko mamlaka. Ila inabidi apatikane kiongozi anaweza kutufikisha kwenye njia ya kweli. Na kiongozi huyo ni lazima aji-sacrifice yeye na hata chama chake au itikadi yake kwanza ili afanikiwe.
   
 15. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Recta mkuu, mi naona kama sina la kujibu kwa Jasusi kwa sababu umejibu vizuri sana. Na pia naweza kusema mfano wake wa Kagame is very unfortunate kwani inaweza kueleweka (si kwamba Jasusi alimaanisha hivyo bali tafsiri inaweza kuwa) Tanzania nayo lazima imwage damu. No! Rwanda au Uganda na Tanzania huwezi kufanananisha
  Lakini naomba tu niache food for thought:
  Nyerere ametawala from 1961 - 1985 how many years? 14 years just alone
  Marais wengine Mwinyi na Mkapa - 10 years each combined 20 years
  Jk - 4 years.
  Tukiangalia utawala wote wa Mwinyi, Nyerere alikuwa ni shadow, alidiriki hata kujitokeza na kumcriticize Prime Minister wa wakati ule Malecela etc. He was a manipulator na aliendeleza ile style ambayo Recta amei-define vizuri as a one man show.So in short Nyerere, until his death, was THE RULER na huu ni ukweli hata tukiipamba vipi. Na sehemu kubwa ya historia ya Tanzania ameinfluence, kwa kuwaweka viongozi wasiostahili katika nafasi zao.
  Jasusi naomba niulize, kama Nyerere asingem-handpick Kikwete kuwa junior minister, angekuwa wapi in a free and fair environment? Nowhere! Probably still in the barracks!
  I have a lot of issues on my plate when it come to JK but looking at the broader picture siwezi kumlaumu personally JK because he is playing by the rule of the game set up by Baba wa Taifa, tunayeendelea kumtukuza and the rules have been modified and manipulated to suit his loyal followers after his death. But kama Nyerere angekuwa kweli ameweka maslahi ya taifa mbele, angehakikisha kuwa ameacha system ambayo ni imara na ambayo is based on meritocracy siyo ya upendeleo na run by a one man show.


  No, my friend Jasusi, Nyerere ndo kiini cha matatizo yetu na mpaka mtakapokubali hilo tutaendelea na kitu kilekile all the time!
   
 16. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  To me Nyerere is revered.

  To the current leadership I always wonder if it is made up of "Yes Men/Women". I always wonder if in the current setup of cabinet and supporting organs are there any people who can actually "tell it as it is" to Prezidaa Kikwete? He is surrounded by "his peeps" - Kawambwa, Mwema, Membe, Cisco etc who I doubt can say jack schiit if there is a need to do so.

  How did he even select the current crop of cabinet ministers? How did 2 senior ministers and 3 junior ministers presented fake degrees and were chosen for key posts? How is it possible that they have not resigned from their posts and the Prez himself has kept mum? A supposedly space physician in Ireland had to resign once he was found out to have a questionable degree from a"prestigious" university - so why not our crop of "leaders"?

  What happened when people we deem to be our leaders are able to swindle the whole country to benefit themselves be let free to continue living with arrogance amongst us wenye nchi? How can a leader like Chenge agree to dubious mineral compensation, shafting the population with no ky, and he be let absolutely free to walk the streets while flipping his middle finger to every citizen of Tanzania? I mean, come on, even Wagosi wa Kaya sang about mtu kuvurunda na kupokelewa kishujaa jimboni kwao!

  Somewhere somehow someone messed up such that they can do such things and get scott free without anyone telling them schiit - the current "case" concerning Yona and Mramba comes to mind. These guys went kinyume cha wataalamu and washauri wa wizara zao and went on to do some things that affected the whole country! And they are left still standing! I am not too enthusiastic as to what will happen in their cases but deep down I have a feeling they are going to walk free........

  I think the prez should develop a back bone and as they say uswahilini "kaza ******" and act on these issues. Fire some people, filisi a whole lot others, acha kutetea watu simply because they assisted in campaign ya kukuweka hapo state house. Haiwezekani wewe na waziri mkuu wako mtoe muongozo miaka miwili iliyopita kwamba bandari na TRA waongeze shift za kufanya kazi and mwaka wa tatu unaenda kule mambo yaleyale na unarudiarudia tena wafanye hivyo! Hebu furumua wawili watatu uone ufanisi! Sasa hivi nikiangalia kule baharini naona meli zimepungua sana karibu kuisha, meaning that it could be done but it wasn't, and the people responsible are sipping on syrup and probably laughing their asses off!

  Namna gani hii mh. prezidaa??
   
 17. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu, naomba niulize kwa nini tunamwangalia Kikwete kama Mungu-mtu, kwa nini tusidai sheri itakayoweka wazi kwamba kiongozi kihiyo anatakiwa kutimuliwa kazini mara moja.
  Lakini pia naomba niulize kwani Nyerere aliweka wasomi tu? Hukumbuki JK alisema alipoteua mawaziri wakekwamba hata yeye aliteuliwa na Nyerere hajui chochote na Nyerere alimwambia you will learn on the job. That is what he is emulating, so why blame JK alone? Nyerere naye aliteua mabumbu kibao!
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nafikiri kinachotokea Tanzania ni ule woga wa kuharibu msemo wa "Zidumu fikra za mwenyekiti", laiti kama tungefanya mambo kwa kusema "Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti" tungeweza kuendelea mbele.

  Ukiangalia mambo mengi, viongozi wa sasa ni wagumu kubadilika au kufanya maamuzi ya kweli kuleta mabadiliko ya keli Tanzania kisa eti tumuenzi Nyerere.

  Hata kina Jefferson wa Marekani pamoja na kuabudiwa kuwa ndio baba wa Katiba ya Marekani, alikuwa ni mwenye kumiliki watumwa na hivyo anapata vyotwe tukuzo la katiba na laana ya kulea utumwa.

  Nyerere was and is not absolute.

  Tunalea kisingizio cha udhaifu wetu na mazoea na hata kunufaika kwetu kwa mfumo butu na hvyo ndio maana huoni hata mmoja katika mfano CCM anadiriki kusimama wazi kukemea mkao wa Utawala na Ubwana!

  Gonjwa hili limesambaa hata kwenye vyama vya Upinzani. Leo hii Mrema na Sefu wanashikilia vyama vyao kama mali binafsi, ukipingana nao, nao wanaingia mkao ule ule wa Ki-Nyerere kwa kupigwa exile kama walivyfanyiwa Kambona na Babu pamoja na makosa yao!

  It is time for change.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Susuviri,
  Nimetoa mfano wa Kagame si kwa sababu ya kumwaga damu. Nimetoa mfano wa Kagame Rwanda kuonyesha kuwa inawezekana kuwa na kiongozi mwenye vision tofauti na azma ya kufanikisha hiyo vision. Sisi Watanzania tukuendelea kumlaumu Nyerere kwa status quo tutakuwa kama tumeganda in a time warp. Mtoto aliyezaliwa mwaka 1985 hivi leo ni mtu mzima tu mwenye umri wa miaka 25 asiyejua ujamaa ni kitu gani. Russia, Poland na nchi nyingi tu za Eastern Europe zimeachana na ukomunisti na leo sijawasikia wanalaumu viongozi wao waliopita kuwa ndio wamewadumaza. Sasa, OK, tumlaumu Nyerere for all our current miseries at the end of the day what are doing to rid us of these miseries? Nyerere is no longer here. Ni wajibu wetu sasa kushika mpini na kuthibitisha kwa vitendo ( siyo maneno) yale aliyoyakosea Mwalimu. Mwangalie Obama, amerithi matatizo chungu mzima, lakini angalia alivyoshupalia kupambana nayo badala tu ya kusema Bush ametuachia matatizo. That is my point, my friend.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kasisi,
  Hata hizi ngonjera za kumuenzi Nyerere ni danganya toto tu. Nionyeshe mfano wa kitu kimoja tu ambacho utawala wa sasa unafanya kuonyesha uenzi wao wa Nyerere. Alikuja Mwinyi akaua Azimio la Arusha. Akaanzisha biashara Ikulu. Akaja Mkapa akauza NBC na kuwagawia makaburu karibu raslimali zetu zote. Mwalimu aliwaambia wasichimbe madini mpaka Watanzania wenyewe watakapokuwa tayari kuyachimba wakamwona hamnazo wakamkaribisha Sinclair, ndugu zangu wakahamishwa kwenye maeneo yao mzungu akapewa. Kumuenzi Nyerere hapo kuko wapi? Afadhali hata wangechukua mazuri aliyoyafanya Nyerere na kuyafanyia kazi lakini hapa ni kama they threw out the baby with the water. Kila mtu anajifanyia kivyake vyake tu.
   
Loading...