Hongera kwa machawa. Walaumiwe waliojigeuza kondoo wa kafara

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Taifa letu soon litageuka kuwa si mahala salama pa kuishi. Uhalifu utaongezeka kama kule Haiti kwasababu watu wengi watakata tamaa ya maisha.

Hivi Sasa kila kitu kinaenda hovyo hovyo lakini waliopewa dhamana ya uongozi kwa kuwa wao wanakula na kushiba wanachukulia poa tu. Idadi kubwa ya watu wanapoteza biashara na ajira kufuatia mfumuko wa bei, ukosefu wa umeme, ukosefu wa sukari, ukosefu wa maji na siasa mbovu.

Hata hivyo wanaopaswa kulaumiwa ni watanzania walio wengi ambao wameamua kuficha mbawa zao na kutoonesha hasira zao kwa watawala. Watanzania walipaswa kuwa wakali na ikibidi kuwawajibisha watawala kwa uzembe badala ya kujigeuza kondoo wa kafara.

Ndiyo maana naona bora hata machawa walioamua kuonesha ujinga wao hadharani kwa kuwashangilia viongozi wanaolipeleka taifa shimoni.
 
Back
Top Bottom