Tanzania tuna tatizo la msingi sana la ujinga na upumbavu

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Tuna tatizo la kusoma na kutoelimika, Tuna tatizo la upumbavu ambalo unakuta mtu ana mpaka degree lakini bado ni mpumbavu. Tuna Tatizo la kutokuwa na elimu ya uraia, Tuna tatizo la kuamini CCM CHADEMA au ACT watatuletea maendele. hakuna mwanasiasa ambaye anaweza kuwaletea maendeleo sababu yupo chama fulani.

Miaka 58 ya uhuru bado nchi haina barabara nzuri, maji, umeme, madawati, madarasa ya kutosha sisi tunashangilia siasa na wanasiasa wanakimbia vyama. watanzania wengi bado ni wapumbavu na wajinga na inawezekana hata viongozi wengi wanaotawala ni wajinga na wapumbavu ndio maana hatuna chochote cha kujivunia zaidi ujinga maradhi(ukimwi) na umaskini.
 
So maendeleo huletwa na nani?Katika moja ya vitu ambavyo Baba wa taifa alisisitiza ili tupate maendeleo,alitaja vinne;
-Watu
-Ardhi
-Utawala bora
-Siasa safi

Hapo moja kwa moja utawala bora na siasa safi vinaungana kupinga uzi wako hapa!Unless unamuona mwalimu naye alikuwa kama hivyo ulivyotaja!
 
Umeongea jambo la muhimu na la ukweli sana. Mungu akubariki. Watanzania tunaona siasa ni kama oxygen ya nchi kumbe ndo tunapotea.
Inabidi tuache kuawaamini wanasiasa wote wa chama tawala na upinzani kwa kuwa wote wanapigania matumbo yao.






Tatizo ni elimu yetu ya mkoloni na ya kukariri madude inatufanya tuwe na akilindogosana inabidi angalau tusome kwa kiswahili kuanzia vidudu mpaka phd.
 
Nikajua mwisho utaweka suluhisho. Mawazo yako wewe kama wewe umechukua hatua gani. Au na wewe umekubali kuwa mmoja wa wapumbavu.
 
Mtu anashangilia mbunge kuhongwa na kununuliwa na ccm kisa yeye ni ccm

Kesho mtoto wake anakosa mkopo wa chuo kikuu kwa kukosa mfumo mzuri wa kumtetea mwanae

Au ndugu yake anafia hospital na maiti inazuiwa kwa kukosa kumaliza deni wakati anaumwana yeye anashangaa tena kama sio ujinga na upumbavu ni nini?
 
Au Kiingereza kuanzia vidudu pia..lol
Kingereza tusikitumie kabisa, huoni wakenya wanatumia kingereza ila na wao ni maboya tu.

Inatakiwa kitu ili ukielewe unapaswa usome kwa lugha yako ya asili unayoitumia kila siku za maisha yako. Nchi zote zilizoendelea wanasoma kwa lugha zao toka vidudu mpaka phd.
Mchina anasoma kwa kichina
Muingereza anasoma kwa kiingereza
Mfaransa anasoma kwa kifaransa
Mjerumani anasoma kwa kijerumani
Mrusi anasoma kwa kirusi
Mjapan anasoma kwa kijapan
Mkorea anasoma kwa kikorea
Sasa kwanini Mswahili asisome kwa kiswahili?
Kwa nini mjerumani muda wa ukoloni alifundisha kwa kiswahili?alitaka watu wake waelewe, ila muingereza alifundisha kwa kingereza ili tuwe wajinga.
Kwa nini biblia wameitafsiri kwa kiswahili?ili tuielewe biblia kwelikweli.
Fungukeni akili chanzo cha matatizo ya Tanzania ni kusoma kwa kingereza.
 
Mtu anashangilia mbunge kuhongwa na kununuliwa na ccm kisa yeye ni ccm

Kesho mtoto wake anakosa mkopo wa chuo kikuu kwa kukosa mfumo mzuri wa kumtetea mwanae

Au ndugu yake anafia hospital na maiti inazuiwa kwa kukosa kumaliza deni wakati anaumwana yeye anashangaa tena kama sio ujinga na upumbavu ni nini?
Pumbavu tu na wewe. Huna hoja yoyote ya maana.
 
Kuna ukweli mkubwa. Tatizo ni makuzi yetu na elimu yetu.
Mtu anapata elimu kubwa lakini kufikiri kiduchu hata ku construnct a complete and useful idea ni tatizo kwa wengi.
Mashuleni siku hizi hakuna utungaji/composition writing. Wanafunzi wana copy na pest. Vijana wengi wanajihangaisha zaidi na mipira na mambo ya vijiweni. Smart phones nazo zinazidi kutuharibu
Ukweli lipo tatizo mkuu. technically,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma kingereza kwanzia vidudu..hakutakua na shida kuelewa ukiingia levels nyingine...ni lugha ya kimataifa,au unadhania ukiingia hizo nchi ulizozitaja utaongea lugha gani kama sio Kingereza??..au kisambaa?? lol
Kwani barabara zinaongea kiingereza? Wachina wanajenga kila siku
Kwani umeme unaongea kingereza?
Kwani viwanda vinaongea kingereza?
Kwani madini yanaongea kingereza?
Kwani gesi inaongea kingereza?
Mito inazungumza kingereza?
Maziwa yananazungumza kingereza?
Madini ya chuma yanazungumza kingereza?

Unatakiwa uwaze kwa marefu na mapana juu ya athari ya lugha katika maendeleo ya nchi. Kiingereza ni kizaramo cha london, ukitaka utajifunza tu.
Taifa letu watu wamekariri madude toka 1961 na sio kuelewa ndio maana maendeleo yanakuja taratibu mno. Wakandarasi woooooote wanatoka nje ya nchi tena hawazungumzi kingereza je hujashtukia hilo?
 
Kuna ukweli mkubwa. Tatizo ni makuzi yetu na elimu yetu.
Mtu anapata elimu kubwa lakini kufikiri kiduchu hata ku construnct a complete and useful idea ni tatizo kwa wengi.
Mashuleni siku hizi hakuna utungaji/composition writing. Wanafunzi wana copy na pest. Vijana wengi wanajihangaisha zaidi na mipira na mambo ya vijiweni. Smart phones nazo zinazidi kutuharibu
Ukweli lipo tatizo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni lugha ya kufundishia. Mimi ninaamini kama 1961 tungesoma kwa kiswahili toka vidudu mpaka chuo kikuu tungekuwa mbali kimaendeleo. Kizazi cha waliosoma enzi hizo ndio wametia hasara taifa letu na kufilisi viwanda na maamuzi ya ovyo kabisa kutokana athari ya kusoma elimu ya kukariri pekee na sio kuelewa.
 
Back
Top Bottom