Tanzania tumedhalilishwa sana nchini Kenya. Isijirudie la sivyo tutalipiza kwa Uhuru Kenyatta desemba 9/2021

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Tanzania ni nchi kubwa Afrika Mashariki. Kihistoria Tanzania ina heshima kubwa duniani.

Tumesikitika sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan na ugeni wake akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya badala ya Rais kama mwenyeji wake.

Tukumbuke Rais (mwenyeji) anapokupokea unakuwa na Ulinzi wote wa uhakika. Badala yake SSH alilindwa na walinzi wa Tanzania bila wenyeji.

Kwa nini mama yetu hakupokelewa na Uhuru Airport na badala yake baada ya sisi kulalamika ndipo Kenyatta anajibaraguza kumsindikiza Airport kurudi Dar? Hii ni dharau sana. Je, ni kwa sababu ya jinsia yake? Hatujapenda hii. Tumenyong'onyea sana kwenye ndege.

Naye mwaliko wake mama Mulamula atampokea sherehe za Uhuru iwe 50/50. Ova
#FreedomIsBack
 
Inaelekea una taarifa za kila jambo mkuu.

Inamaana haukuona alivyokuwa na mwenyeji wake ikulu Mama akipigiwa gobore 21 na kukagua manamba kwa heshima zote?

Huwezijua mwenyeji wake alikua na masahibu gani au ratiba zilikuaje.

Punguza kidogo roho mbaya inayochagiza kisasi...umeenda mbali sana kupanga adhabu bila kujipa muda ujue ukweli wa mambo.

Inamaana kweli serikali wanaweza kuusikiliza huu ushauri wako???
 
Kuna Watu ni Wapumbavu hapa duniani hadi mnaboa. Kuna Siku Rais wa Uganda alikuja Tanzania na alipokelewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo Profesa Kabudi mbona Waganda hawakusema kuwa Rais wao kadhalilishwa?

Ni vyema kama hatujui mambo ya Itifaki tukanyamaza tu. Ukienda nchi yoyote ile kama Rais kwa Official Visit utapokelewa hata na Waziri au Waandamizi wa Ikulu ila Rais akizuru nchi yoyote kwa State Visit pale ndipo Mwenyeji wake ( Rais ) wa nchi husika hulazimika kuja Kumpokea. Elimu ya Itifaki inahitajika kwa baadhi yenu.
 
Acha kulalamika vitj vya kipuuuz puuuzi wew unaijuwa snaa itifakai kuliko wengine kwahyo wee Hilo ndio Kos umeliona ukaja uku nduki kuandika Uzi ...badilika vitu vingene pokea nlin a positive way


Ala in all wakenya CYO watu wakuwaamini
 
EeeenHeeee,

Mimi nilidhani unalo la maana la kulalamikia, kumbe ni huo upuuzi?

Mbona kapigiwa mizinga 21, na kahutubia bunge, yote haya hujayataja kama ishara za kutudhalilisha!

Hii ni ishara ya kuwa na "small mind."

Unatoka jasho kwa vitu vidogovidogo unasahau mambo muhimu Rais wako aliyoyatangaza kuiuza nchi yako; ikiwa na wewe pamoja!

Kwa hali ya namna hii tutafika wapi kama taifa!
 
Nafikiri kuna mahusiano ya karibu zaidi kati samia na huyu amina, maannanhata iftar yenyewe alikula na amina na sio uhuru, na hisi kupitia huu uswahiba wa amina na samia uhuru akaona apenyeze sera zake za opportunism.

Lkn pia nalitazama hili ni kama huyu uhuru ametaka wana siasa wamama wa kenya na wao wa enjoy kumpokea mwana mama mwenzao ..najaribu kuhisi lkn sijafikiria bado ..izi ni mahisiyo tu
 
mda mwingine watanzania tubadilike, tuache nongwa za kjinga.

sawa kupokolewa alipokelewa na waziri wa mambo ya nje.

wakati wa kuondoka, uhuru kenyatta kamsindikiza mama hadi uwanja wa ndege.

hilo unazungumziaje ndg. mleta mada?.
Jambo ambalo hulijui ni kwamba linapokuja suala la usalama hasa nchini Kenya kwenye ugaidi. Jua kwamba unapopokelewa na Rais mwenzio unakuwa salama zaidi kiulinzi. Sisi hatukupokelewa na PSU ya Kenya. Tulijitegemea. Vipi lingetokea la kutokea si tiyari CDF Mabeyo angeshafunga mipaka? Naongea kama mtu wa diplomasia. Ulijua kwa nini mama alivaa rangi maruni? Au unadhani ni urembo kwake? Unataka shule?!
 
Back
Top Bottom