Tanzania Tanzania mbona unateketezwa?

Kyakya

JF-Expert Member
Apr 24, 2009
398
23
Nimeandika shairi la ubeti mmoja naomba kama tunaweza kuuendeleza!


Hodi hodi naingia, Foramuni kuwajuza,
Wageni wamevamia, Nchi kuiteketeza,
Wenyeji baadhi pia, Hasa tuliowakweza,
Tanzania Tanzania, mbona unateketezwa.
 
Kyakya waniacha hoi,
Na hilo wazo lako,
Nimejaribu kuwaza,
Hasira zikanipanda,
Wageni uliowataja,
Wamekaribishwa na mjombako,
Ndugu yake na mamayo!
Mikataba kawapelekea,
Kawafuata ughaibuni,
Kwenye hoteli za fasheni.
Kosa lao nini?
Hebu nijuze leo.


Na hao wenyeji wawasema,
Kwa kura zako umewachagua,
Tisheti ulivalishwa,
Na buku-jero ukasunda,
Sasa leo waliani,
Wanapokuteketeza,
Acha warudishe mtaji,
Na faida wajazie,
Usilie bwana Kyakya,
Wavuna ulichopanda.
 
Kyakya waniacha hoi,
Na hilo wazo lako,
Nimejaribu kuwaza,
Hasira zikanipanda,
Wageni uliowataja,
Wamekaribishwa na mjombako,
Ndugu yake na mamayo!
Mikataba kawapelekea,
Kawafuata ughaibuni,
Kwenye hoteli za fasheni.
Kosa lao nini?
Hebu nijuze leo.


Na hao wenyeji wawasema,
Kwa kura zako umewachagua,
Tisheti ulivalishwa,
Na buku-jero ukasunda,
Sasa leo waliani,
Wanapokuteketeza,
Acha warudishe mtaji,
Na faida wajazie,
Usilie bwana Kyakya,
Wavuna ulichopanda.

mnh, ongeza bidii uweke VINA na MIZANI!


 
Last edited:
hodi hodi foramuni, kwa mbwembwe naingia,
mkono keybodini, ukweli wa tanzania nawamwagia,
dar mpaka mikoani, hakika jipu leo nawapasulia,
Tanzania Tanzania, mbona unateketezwa?.

misitu mikubwa umejaaliwa, wajanja wanahujumu,
magogo mazuri wajitwalia, mafisadi wa nchini humu,
mabilioni kifisadi yakwapuliwa, maisha yetu magumu,
Tanzania Tanzania, mbona unateketezwa?.

meno ya tembo yafichwa, ughaibuni yasafirishwa,
wahusika wote wakikamatwa, tatizo litakomeshwa,
rasilimali zetu zaibwa, fedha kigeni twakoseshwa
Tanzania Tanzania, mbona unateketezwa?.


to be continued.........
 
Back
Top Bottom