Tanzania: Quotes & Our National Politics!

"The highest return to share-holders-continues to drive the market, which tends to concetrate wealth and power, which in turn influence the political process."

- Author Unknown.
 
"Democracy is a two faced phenomenon.

- One face gives an individual the right to elect and be elected,

- while the other face is the right to listen and respect the wish and the will of the majority, once the people have spoken"


- Author Uknown
 
Hope is the belief that our destiny will not be written for us, but by us, by all those men and women who are not content to settle for the world as it is, who have the courage to remake the world as it should be.
By Barack Obama
 

"...natembea na vitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha."
-Mwl Nyerere.
 
"tunataka kiongozi ambaye anachukia rushwa, na hata tukimwangalia usoni tunaamini anachukia rushwa, Sio ambaye hata ukimuangalia unajiuliza, mnh, huyuu????!"
-Mwl Nyerere
 
"Viongozi wa Chadema wamekuwa wakizunguka mikoa mbalimbali nchini na kuisema vibaya CCM na serikali yake hivyo, kama wana CCM mtakaa kimya, wananchi wataamini yote yanayosemwa na Chadema."
-Yusuf Makamba
 
"Ni fikra potofu na ni udhalilishaji kufikiri kwamba Watanzania wanapokutana usiku wanakuwa na kazi moja tu ya ‘kushughulikiana', kwa kweli hatupaswi kuendelea kufikiri hivyo,"
-Mh. Juma Kapuya
 
"Mstari wa mbele wanatuona mstari wa nyuma hamnazo, tulikataa Shirika la Ndege Tanzania (ATC) lisiuzwe kwa mwekezaji wa kutoka Afrika Kusini, hatukusikilizwa kabisa na badala yake walitumia uwezo wote wakafanikiwa,"

"Sisi wengine tunaambiwa tusubiri... tusubiri, hawa wenzetu wao walio mbele (mawaziri) wanatengeneza za kwao, hii ni sahihi?"
-Mh Lucas Selelii
 
"Namuheshimu sana Profesa Maghembe lakini kwa kuwa ameanza kunichafua na kuniita kizee kinachong'ang'ania jimbo la Moshi mjini, sasa nitaanza kumshughulikia kisiasa hadi nimng'oe ubunge 2010,"
-Mh Ndesamburo
 
"Kila siku Watanzania wanasikiliza EPA, Richomnd, mgodi wa Kiwira, Rais mstaafu Mkapa anatukanwa tena na wengine ni baadhi ya wana-CCM, Bunge linataka kugeuzwa la majungu,"

"Chenge alivunja nyumba ya nani? Na hayo mabenki yanayotoa siri za wateja wao yanapaswa kuchunguzwa."
'Oh, mara Chenge mchawi, Spika mchawi' "
-Mh Samuel Chitalilo
 
"Mwandishi huyo angekuwa karibu yangu, ningempiga kichwa, amechafua sana jina la Tanzania. Lakini kichwa cha samaki, panki ni mboga nzuri, ikiandaliwa vizuri, ni tamu sana ila serikali iyaweke mapanki katika mazingira mazuri."
-Mh John Momose Cheyo
 
"Namuheshimu sana Profesa Maghembe lakini kwa kuwa ameanza kunichafua na kuniita kizee kinachong'ang'ania jimbo la Moshi mjini, sasa nitaanza kumshughulikia kisiasa hadi nimng'oe ubunge 2010,"
-Mh Ndesamburo

Oh really.....
 
".. Waafrika ndivyo tulivyo.." - Author Nyani Ngabu (Member-JF).

Tunaridhika sana na mambo madogo madogo, hatubadiliki na hatupendi maendeleo ya kweli, matokeo yake tunaendelea kuwachagua viongozi wale wale wabovu tena sometimes kwa mpaka kura za 80%, ni kwa sababu ndivyo tulivyo, yaani akili yetu ni kama ya viongozi wetu, na ni olny in Tanzania tu!.

Ndugu Field Marshal, Natanguliza heshima, na kwa taadhima naomba kutokubaliana na wewe kuhusu hili suala, hata wenzetu wa ughaibuni huwa wanachagua kiongozi huyo huyo hata kama hana anufaaa kwa jamii. Watu wa jimbo la Illinois walimchagua Rod Blagojevic mara mbili, meya wa jiji la Chicago ndiyo usiseme anatoa mpya kila siku na watu bado wanamchagua.

Kwa hiyo kwa kuchagua viongozi tuliyowazoea nadhani ni ugonjwa wa kibinaadamu si Watanzania tu.
 
Ndugu Field Marshal, Natanguliza heshima, na kwa taadhima naomba kutokubaliana na wewe kuhusu hili suala, hata wenzetu wa ughaibuni huwa wanachagua kiongozi huyo huyo hata kama hana anufaaa kwa jamii. Watu wa jimbo la Illinois walimchagua Rod Blagojevic mara mbili, meya wa jiji la Chicago ndiyo usiseme anatoa mpya kila siku na watu bado wanamchagua.

Kwa hiyo kwa kuchagua viongozi tuliyowazoea nadhani ni ugonjwa wa kibinaadamu si Watanzania tu.

- Labda kama ungeweka makosa yao yanayofanana na ya viongozi wetu wa Tanzania, na madhara yake kwa wananchi wao, maana sidhani kama kuna tatizo kuliona hilo la matokeo ya uozo wa viongozi wetu hapa bongo?

- Mara ya mwisho nilipokuwa huko Chicago, niliona karibu barabara zote za Sate zikiwa under construction, sasa eti unasema hao viongozi wao wa Chicago hawana manufaa kwa wananchi wao? wakati bara bara zote zilikuwa zinapigwa msasa? au?
 
"CCM ya watu wenye hekima zao na busara za hali ya juu ilishindwa kuniondoa miaka yote, itakuwa CCM hii ya Makamba ya kununua wapinzani kwa bei ya biskuti"
-Mh W Slaa.
 
"Uongozi hupewa mtu wenye uzoefu, mstahiki, muadilifu na mchapakazi,"
-Mstaafu, Alhaj A H Mwinyi
 
"Watu wamejenga tabia kuwa mimi siku zote ni mtu wa kupinga kila kitu. Hii si kweli... wakati fulani nipewe nafasi ya kujieleza kwanza mjue kuwa ninataka kuzungumza nini katika jambo hili ndipo mnikosoe, lakini hii ya kusimama na kuambiwa kuwa ninakwenda kinyume si sahihi."
-Mh Zitto Kabwe
 
Back
Top Bottom