- Labda kama ungeweka makosa yao yanayofanana na ya viongozi wetu wa Tanzania, na madhara yake kwa wananchi wao, maana sidhani kama kuna tatizo kuliona hilo la matokeo ya uozo wa viongozi wetu hapa bongo?
- Mara ya mwisho nilipokuwa huko Chicago, niliona karibu barabara zote za Sate zikiwa under construction, sasa eti unasema hao viongozi wao wa Chicago hawana manufaa kwa wananchi wao? wakati bara bara zote zilikuwa zinapigwa msasa? au?
Utengenezaji wa barabara mara nyingi ni federal government inashughulikia.
"Umaskini ni kitu mbaya"
".. Waafrika ndivyo tulivyo.." - Author Nyani Ngabu (Member-JF).
Tunaridhika sana na mambo madogo madogo, hatubadiliki na hatupendi maendeleo ya kweli, matokeo yake tunaendelea kuwachagua viongozi wale wale wabovu tena sometimes kwa mpaka kura za 80%, ni kwa sababu ndivyo tulivyo, yaani akili yetu ni kama ya viongozi wetu, na ni olny in Tanzania tu!.
Tatizo ni kuwa nia ya kuchagua viongozi mbadala ipo. Ila inadhoofishwa na hao viongozi mbadala tunatakiwa kuwachagua. Hebu niambie, katika chaguzi zetu za Rais nani kutoka upinzani anaeelekea kuwa suitable altenative choice? Kwakweli hatujamuona. Upinzani usipokuwa makini na kutuletea chaguo thabiti, mtu anaeheshimika, anae aminika na anaefahamika kwa uwezo wake wa kuleta mabadiliko ya kweli na kuliunganisha taifa, nchi hii itaendelea kushuhudia viongozi wale wale wakichaguliwa kila siku. Wahenga wanasema, Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Kaka hapo nimeona na nakubaliana na wewe na kama wana CCM wengi wangekuwa na mawazo kama ya kwako najua Tanzania yetu ingefika mbali sana. Ila personal I RESPECT YOU IN THISMkuu Recta, heshima mbele,
- point yako ni nzito tena sana, lakini pia bado Upinzani hawajapewa nafasi ya kutuonyesha uwezo wao, binafsi ninamuamini sana Dr. Slaa kuwa akipewa nafasi anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana, hasa kwenye the respect kwa rule of law, maana ndicho hasa kinachoniweka hapa JF ni kuona siku moja taifa langu linatawaliwa kwa sheria na haki.
However:-
- Ninaisikia hoja yako ya ubovu wa vyama vyetu mbadala, I mean ni kweli kabisa kuwa some of them vinahitaji ukarabati kweli kweli, mimi nilikuwa sivijui vizuri lakini katika muda mfupi niliokaa humu forums, nimepata angalau a small picture kwamba kuna viongozi makini wachache huko Upinzani, lakini wengi ni wale wale tu kama wetu wa CCM.
- Wa-Tanzania bado tuna kazi kubwa ya kuikubali na kuielewa demokrasia, kukubali mawazo tofauti na yetu, bado tuna tatizo sana kwenye hilo kuanzia CCM mpaka Upinzani, lakini pole pole tutafika tu.
Kuna visa (hadithi) viwili ambavyo vilikuwa vikisimuliwa ama mitaani hata kwenye mashule mithili ya hadithi za jioni kuhusu Mwafrika na unyonge wake. Kwa kiwango kikubwa, visa hivi vinaelemea sana kumuonyesha kuwa kauli ya "Ndivyo Tulivyo" ina uhalali!
Kisa cha kwanza; Siku moja, Mwafrika, Mwarabu, Mwasia na Mzungu walikuwa kijiweni, Mungu akaja akawaambia nina vitu vinne inabidi niwagawie, kubalianeni nani anataka nini. Vitu hivyo vilikuwa ni Utajiri, Maarifa, Biashara na Ngoma.
Basi wale wanne wakakaa wakitafakari na kujadiliana kisha kila mtu akashika alichokitaka.
Mungu aliporudi kuwahoji chaguzi zao, akakuta kila mtu kachagua kitu kimoja na hapatakuwa na ugomvi au kufanya uamuzi kupatanisha.
Mzungu akadamka, mimi nataka Akili, Mungu akawauliza wengine, je kuna mwingine kati yenu anayetaka Akili, wakasema hakuna, Mzungu akapewa Akili (Maarifa).
Mungu akasema, nani mwingine aliye tayari Mwarabu akakurupuka "nataka Utajiri" na kama wakati wa Mzungu, hakuna aliyebisha!
Mwasia akaja haraka, "Mungu mimi nataka Biashara, ili nitembee dunia nzima na kuwauzia watu vitu. Mungu akamgeukia Mwafrika, je wakubaliana na hili? Mwafrika huku akikenua meno na tabasamu akasema ndiyo mwache achukue biashara maana wote hawa wamekosea, wameiacha Ngoma ambayo ni muziki safi na ina mdundo.
Mwafrika akakimbilia ngoma yake akaikumbatia akaanza kutumbuiza huku Mzungu akitafakari nini cha kufanya, Mwarabu akiufurahia utajiri wake na Mwasia akipanga mipango ya biashara!
Mpaka leo tumeendela kukumbatia Ngoma na ndio maana tu mahiri kwenye sanaa!
Kisa cha Pili: Hiki nilihadithiwa na Mchungaji kanisani wakati wa kwenda Mafundisho ya Kipaimara. Tulimuuliza kwa nini kama Mungu ana mapenzi na alituumba kwa mfano wake,iweje kuna Wazungu, Wachina, Waafrika au Waarabu?
Jibu lake likawa ni ile laana ya mtoto wa Nuhu (aliyejenga safina)aliyemcheka baba yake kuwa uchi baada ya kulewa. Mchungaji akatuambia kuwa uzao wa yule mtoto aliyelaaniwa ndio chimbuko la Waafrika na sisi ni watu tuliolaaniwa kuwa watumwa na watumishi wa wenzetu!
Sasa kama hadithi hizi nilisimuliwa nikiwa mtoto na tukazizungumza kijiweni tutakuwa, hamuoni kuwa tayari tulishapanda mbegu ya kujiona dhaifu na wanyonge hivyo kuhalalisha dhana ya "Ndivyo Tulivyo"?
Mkuu Recta, heshima mbele,
- point yako ni nzito tena sana, lakini pia bado Upinzani hawajapewa nafasi ya kutuonyesha uwezo wao, binafsi ninamuamini sana Dr. Slaa kuwa akipewa nafasi anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana, hasa kwenye the respect kwa rule of law, maana ndicho hasa kinachoniweka hapa JF ni kuona siku moja taifa langu linatawaliwa kwa sheria na haki.
However:-
- Ninaisikia hoja yako ya ubovu wa vyama vyetu mbadala, I mean ni kweli kabisa kuwa some of them vinahitaji ukarabati kweli kweli, mimi nilikuwa sivijui vizuri lakini katika muda mfupi niliokaa humu forums, nimepata angalau a small picture kwamba kuna viongozi makini wachache huko Upinzani, lakini wengi ni wale wale tu kama wetu wa CCM.
- Wa-Tanzania bado tuna kazi kubwa ya kuikubali na kuielewa demokrasia, kukubali mawazo tofauti na yetu, bado tuna tatizo sana kwenye hilo kuanzia CCM mpaka Upinzani, lakini pole pole tutafika tu.
Mkuu Recta, heshima mbele,
- point yako ni nzito tena sana, lakini pia bado Upinzani hawajapewa nafasi ya kutuonyesha uwezo wao, binafsi ninamuamini sana Dr. Slaa kuwa akipewa nafasi anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana, hasa kwenye the respect kwa rule of law, maana ndicho hasa kinachoniweka hapa JF ni kuona siku moja taifa langu linatawaliwa kwa sheria na haki.
However:-
- Ninaisikia hoja yako ya ubovu wa vyama vyetu mbadala, I mean ni kweli kabisa kuwa some of them vinahitaji ukarabati kweli kweli, mimi nilikuwa sivijui vizuri lakini katika muda mfupi niliokaa humu forums, nimepata angalau a small picture kwamba kuna viongozi makini wachache huko Upinzani, lakini wengi ni wale wale tu kama wetu wa CCM.
- Wa-Tanzania bado tuna kazi kubwa ya kuikubali na kuielewa demokrasia, kukubali mawazo tofauti na yetu, bado tuna tatizo sana kwenye hilo kuanzia CCM mpaka Upinzani, lakini pole pole tutafika tu.
"Aliye juu, msubiri chini" -Mhenga hapo zamani...