Tanzania one haina mkataba

Mgumu

Senior Member
Nov 3, 2006
111
11
Kwa walioangalia chanel 10 jana 01/10/07 [Jenerali on Monday} watakubaliana na mimi kuwa uwezo wa wataalam wetu unatia shaka, mahojiano hayo yalihusha kamisna wa madini na mwanasheria wa wizara ya madini wote hawa wana PHD, mada kuu ilikuwa ni kujibu hoja za mwanaharakati Tindu Lisu.

Mahojiano yaliboa kwani kamisna wa madini na mwansheria walionekana kushindwa kujieleza na kujibu mwaswali ya wasikilizaji. Kujichanganya huku kulipelekea kamishna wa madini kuutangazia uma kuwa kuna baadhi ya makampuni makubwa ya madini yanachimba madini bila kuwa na mkataba.

Mtazamaji mmoja alimuulizwa kutakaka kujua ni kampuni gaini inachimba madini bila mkataba, kamisha wa madini akatamka kuwa ni Tanzania one, hawa wana lesini lakini hawana mkataba.

Swali, Tanzania one inamilikiwa na nani, na kwanini haina mkataba?
 
Hawa wateule waliotumwa kutuliza wimbi la buzwagi wameshindwa kuifanya kazi hiyo, sana sana wamezidi kuharibu kwa jinsi walivyoshindwa kukidhi haja wa watanzania kupata taarifa ya serikali kuhusiana na suala hilo.

Kwamba suala la mkataba si jambo la lazima, mpaka waziri ajisikie ndo anaweza kuamua kama mkataba unahitajika au la, hicho ni kichekesho kilichoibuliwa na Dr. wa Jiology bwana kapfumu ambaye alikuwa afisa habari wa wizara ya nishati kabla hajaukwaa ukamishna wa madini.

Faida nchi zinazoletwa na migodi isiyo na mkataba, alishindwa kutueleza na hivyo serikali inapaswa kutoa majibu ya kina kuhusiana na hilo sakata mpya.

Kwamba mkataba uliandaliwa mapema na hivyo hapakufanyika haraka yoyote katika kuusaini, maelezo ambayo yanatofautiana na yale Karamagi aliyotoa bungeni kwamba alitumia mbinu za kampuni binafsi anazomiliki katika kuharakisha kusaini ili nchi isipoteze nafasi iliyopewa na Barrick, ni uthibitisho kwamba Karamagi ndo alilidanganya BUNGE.

Kwa mujibu wa kamishna na mwanasheria wa wizara, mkataba siyo siri. Tatizo ni wabunge wetu kuwa mbumbumbu wa taratibu kwani wangetaka wangeweza kupewa mkataba huo, maelezo haya ni fasaha kweli? Kilio cha wabunge hawakuwahi kukisikia? Hata sitta hakujua huo utaratibu?

Kwa hali hii sijui hata hao mawaziri wanaenda kuwaeleza nini wananchi.
Cha kufurahisha tu ni kwamba mkataba walionao kina Lissu imethibitika kuwa ni halisi, na kelele za serikali kuwa ni uzushi sijui zinatokana na kitu gani.

Mungu ibariki tanzania
 
ndugu zanguni wapendwa kwa waliotazama jana Jenereali On Monday ilikuwa ni aibu tupu,yaani "wasomi" wawili wa PHD walishindwa kabisa kuchambua hoja na badala yake wakaanza kupiga danadana tu za kisiasa mpaka ilifikia hatua Jenerali akawa anaboreka na kuudhika sana,nakiri sijawahi kumuona Jenerali akiloose patience kama jana.Lakini hii inathibistisha kitu kimoja,kuwa hoja zote za Slaa,Zitto na Lissu ni thabiti na zina mashiko imara...kilichokuwa wazi ni kuwa hawa jamaa "walitumwa" kuja kumitetea Karamagi lakini siku zote uwongo ni vigumu kuutetea,hili walilitambua mapema ndo sababu walikuwa wakitegeana sana kujibu.lililo dhahiri pia ni kuwa mkataba alio Tundu Lissu ndo halisi aliusign karamagi.Yaani ilikuwa kama vile baba anawahoji watoto wake walioiba shilingi 50 na kwenda kununua pipi,Kafumu na mwenzake walitia aibu.Hivyo basi huu ni mwanzo mzuri sana wa safari yetu kuelekea katika ukombozi na kuimarisha demokrasia rasilimali kama anavyosema Zitto...I wonder kama Karamagi angekuwapo sijui angeongea nini...
 
Tanzania one..... Balozi Ami nini? na vipi waziri Masha ana nini huko au tenda tu?
 
Kwa walioangalia chanel 10 jana 01/10/07 [Jenerali on Monday} watakubaliana na mimi kuwa uwezo wa wataalam wetu unatia shaka, mahojiano hayo yalihusha kamisna wa madini na mwanasheria wa wizara ya madini wote hawa wana PHD, mada kuu ilikuwa ni kujibu hoja za mwanaharakati Tindu Lisu.

Mahojiano yaliboa kwani kamisna wa madini na mwansheria walionekana kushindwa kujieleza na kujibu mwaswali ya wasikilizaji. Kujichanganya huku kulipelekea kamishna wa madini kuutangazia uma kuwa kuna baadhi ya makampuni makubwa ya madini yanachimba madini bila kuwa na mkataba.

Mtazamaji mmoja alimuulizwa kutakaka kujua ni kampuni gaini inachimba madini bila mkataba, kamisha wa madini akatamka kuwa ni Tanzania one, hawa wana lesini lakini hawana mkataba.

Swali, Tanzania one inamilikiwa na nani, na kwanini haina mkataba?


Ndugu zangu hakuna kazi kubwa kama muungwana kupewa kazi ya kutetea ufisadi. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa Mkurugenzi wetu wa Madini ni mmoja wa wale watendaji waaminifu kwa taifa letu ambao kwa sasa wamekuwa endangered spicies. Labda kuna yake machafu yaliyojificha lakini hadi sasa naamini ninachokijua.

Sasa mtu kama huyu anapotumwa kutetea uozo ambao inawezekana hata yeye hauamini ni lazima utajichanganya na kusema yasiyotakiwa kusemwa. Kwa waliokuwa wakimwangalia kwa umakini ni wazi watagundua kuwa ndugu huyu alikuwa anateseka sana moyoni alipokuwa akitekeleza utumwa wake.

Kwa kweli hali inakuwa mbaya maana naona ndugu zetu wameamua kuongeza spidi ya kuhakikisha kuwa kila mtu ana vumbi la ufisadi ili kusiwe na wakumfunga paka kengele. Huu ni mkakati maalumu ulioanza kutekelezwa na wataalamu wa ufisadi na matarishi wao katika asasi mbalimbali za dola ili kuhakikisha kuwa wote wanakuwa wachafu. Mmoja wa victims maarufu wa mkakati huu ni Mzee wetu Jaji Warioba. Wapo pia waungwana wengi katika list ambao wameingizwa mtegoni kwa kudhani kuwa wanafanya kwa maslahi ya chama na tabaka tawala.

Inasikitisha kuwa sasa mkakati huu unawatarget watendaji wetu. Kwa kweli inasikitisha na inatisha pia.

Nasubiri kuona waungwana wachache waliomo katika baraza la mawaziri wakiloweshwa tope hili la ufisadi kwa jina la kutetea serikali ya JK. Sijui ni nani atakuja kuokoa jahazi pale watanzania watakapondoa imani yao kiduchu iliyobakia kwa viongozi wote na serikali nzima na tabaka tawala lote kupoteza legitimacy....tunaelekea pabaya mno

Mungu endelea kuonyesha mapendo yako kwa waja wako watanzania...

Tanzanianjema
 
ningemshauri jk aitishe uchaguzi mpya ilikuinusuru nchi ktk janga hili,kinyumechake ni wtz kuchukua sheria mkononi ili kuwaondoa wabadhirifi wote.
 
..kila wakiibuka kukanusha au kufanya spin zao ndio vinaibuka na vingine vichafu zaidi,na wakikaa kimya sijui ndio itakuwaje maana moto wake utakuwa ni mbaya zaidi hapo JK kujiokoa inabidi afanye kweli kutetea uraisi wake ili naye wasimwite kibaka...awaambie kina Karamagi wajiuzulu tuu na full investigation ifuate..lakini naye atapona?
 
Kwanza nawashukuru wana JF kwa kutumegea kile kilichoendelea ch.10. Lakini zaidi nawaomba kama kuna uwezekano mtubandikie hiyo mahojiani kama ilivyofanyika last week.
 
Ndugu zangu hakuna kazi kubwa kama muungwana kupewa kazi ya kutetea ufisadi. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa Mkurugenzi wetu wa Madini ni mmoja wa wale watendaji waaminifu kwa taifa letu ambao kwa sasa wamekuwa endangered spicies. Labda kuna yake machafu yaliyojificha lakini hadi sasa naamini ninachokijua.

Sasa mtu kama huyu anapotumwa kutetea uozo ambao inawezekana hata yeye hauamini ni lazima utajichanganya na kusema yasiyotakiwa kusemwa. Kwa waliokuwa wakimwangalia kwa umakini ni wazi watagundua kuwa ndugu huyu alikuwa anateseka sana moyoni alipokuwa akitekeleza utumwa wake.

Naelekea kuamini usemi wako hasa kujumlisha na suti walizovaa na confo lilikuwa ziro. Inaonekana hawa mabwana waliambiwa ni lazima waende kuitetea serikalini. Ilionekana wazi kuwa walikuwa wanazungumza wasichokiamini.
 
Sio huyu Kafumu aliyesema watasakwa walioutoa huo mkataba? sasa anasemaje sio siri!?

NIMECHANGANYIKIWA!!
 
FD,
Siyo wewe uliyechanganyikiwa. Ndio maana Bomani anawashauri wasiende mahakamani. Yule ni lawyer anajua kitakachojiri kule. Lakini sanduku la pandora tayari limefunguka. Tusubiri.
 
Kwa ninavyo mfahamu Dr Kafumu, ni mtu muadilifu na anamwogopa Mungu!! Alikuwa ni mpigania ukweli tokea akiwa mwanafunzi pale VUB Belgium akifanya PhD yake ya geology. Jana amenishangaza sana na majibu yake ya kipumbavu kabisa bila hata kujali profesion yake, alikuwa muoga maswali mengi akitaka yajibiwe na mwanasheria wake ambaye naye hakuwa well informed na issue yote ya Buzwagi.
Jamani hakuna kulala mpaka kieleweke !! Ikiezekana kipindi kingine cha Jenerali awaiita akina Lisu ama Zitto na hao jamaa wa wizara ya mafisadi (madini)
 
karibu mzee wa ushirombo,
Vipitumbaku mwaka huu imepatikana ya kutosha au mavuno yalikuwa hafifu
 
Waangalieni nani ni Wakurugenzi wa Tanzania one ndio mtashika Vichwa na kujua kuwa List ya Dr Slaa ilichukua majina ya Baadhi yao tu!na wala Jaji Bomani hakuwa mjinga kusema Chonde msiende Mahakamani,kwani nae yaweza kuwa akatajwa kwa ushauri wake wa kisheria kwa Kampuni fulani!!!
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nae anamiliki Mgodi huko Arusha.

MGODI WA PROFESA KAPUYA WAPORWA.
NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
WATU wanne wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuhusika na wizi wa mashine katika mgodi wa madini ya rubi, unaomilikiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya.
Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Basilio Matei zilisema tukio hilo lilitokea usiku wa Septemba 16, mwaka huu katika mgodi huo uliopo kijiji cha Kiseriani, wilayani Longido.
Kamanda Matei aliwataja watuhumiwa wa wizi wa mashine hiyo inayotumika kwa ajili ya hewa mgodini kuwa dereva wa gari aina ya Fuso, lenye namba za usajili T 826 AJT, Nyinyila Mwambasa (31), mkazi wa Makao Mapya mjini Arusha.
Wengine ni Daniel Barnabas (28), mkazi wa Lendikinya, wilayani Monduli; Lomayani Kalea (25), mkazi wa Namanga na Jumanne Ramadhan (26), mkazi wa Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda Matei, watuhumiwa baada ya wizi wa mashine hiyo, waliisafirisha kwa kutumia gari hilo. Hata hivyo, walikamatwa wakiwa Namanga.
Alisema utekelezaji wa wizi huo ni njama zilizopangwa kwa kipindi kirefu, kati ya wezi hao na baadhi ya watumishi wa mgodi huo, kwa kuwa si rahisi kwa watu wa nje kuingia ndani ya mgodi pasipo kuwa na wenyeji.
"Waziri Kapuya anamiliki mgodi wa uchimbaji wa madini ya rubi katika eneo hilo, kwa hiyo watuhumiwa walipanga njama kwa kushirikiana na baadhi ya wachimbaji …hivi sasa tunawashikilia watuhumiwa wanne," alisema Kamanda Matei.
Imetolewa kwenye Gazeti la Uhuru.
ISSN 0876-3896
# 19114 Dt:02:10:07
 
amakweli ccm ni chukua chako mapema,hivi wanapokaa kwenye vikao vyao vya baraza la mawaziri kazi yao ni kugawana mali za wadanganyika tu,haaaaaaaaa ndio maana nchi haina hata chembe ya maendeleo.
Niwakati sasa wa viongozi kuchagua moja biashara au utumishi wa umma.
 
mimi nimeona live mpaka nikajisikia kichefuchefu maana walianza kukataa kuwa mkataba uliovuja sio original, wakaulizwa kwana huo original hakuna sehemu Kara...alifuta kwa mkono? baadae wakakubali nakudai anayohaki yakufuta kama waziri mwenye dhamana hiyo sasa sijui walikuja kufanya nini humu chan.10 inaelekea wamekuja kupoza joto. mbaya zaidi wanazidi kuchimba kabuli kwa kusema eti kuna makampuni yanafanya kazi bila leseni, inabidi tuchunguze nani anamiliki hayo makampuni kama hutakuta ni wao wenyewe.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom