Tanzania ni Nchi Nzuri Sana na Ina Watu "Wazuri!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni Nchi Nzuri Sana na Ina Watu "Wazuri!"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Feb 9, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  Jamani tuache utani, watanzania ni watu "wazuri" na nchi yao pia ni nzuri sana! Kwa nini?
  1. Mbunge akiona hajafanya chochote ndani ya kipindi cha miaka 4 anarudi mwaka wa tano na kuwaahidi kwamba atafanya makubwa, watanzania kwa jinsi walivyo "wazuri" wanampa kura.
  2. Rais alitoa ahadi nyingi sana na kama angezitekeleza Tanzania ingekuwa nchi inayotiririka "asali na maziwa,"lakini mimi sina uhakika kama ametekeleza hata moja, mwaka huu mwezi Oktoba Rais akiomba kura utashangaa watanzania walivyo "wazuri" watampa kura!
  3. Wageni toka nje wanakuja nchini kwetu wanachota vijisenti kupitia mikataba mibovu, watanzania walivyo "wazuri" wananung'unika siku mbili tatu, kisha mkubwa wao anawaahidi kuunda Litume la kupitia mikataba mibovu. Mkubwa akiona watanzania "wazuri" wameshatulia basi anaweka likarabrasha kwenye shelf!
  4. Mkubwa akisoma hotuba Bungeni kwamba eti kuna wezi wamerudisha vijisenti walivyoiba bila kuwataja wezi wenyewe! Watanzania "wazuri" walinung'unika kichini chini lakini wakaahidiwa kwamba vijisenti hivyo vitawekwa kwenye Benki yao ya Raslimali bila hata kuridhiwa na Bunge! Watanzania "wazuri" wakaridhika na mpaka sasa haijulikani kwamba vijisenti hivyo viliwekwa huko na kama wakulima walifaidika au la! Hata kama ikitokea walifaidika, wezi wasio na majina walifanywa nini?
  5. Ama kweli Tanzania ni nchi "nzuri," ndio maana hata Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya wanakomalia sana Jumuiya ya Afrika Mashariki (yaani kuwa nchi moja) kwa sababu wanajua "uzuri" wa Tanzania na Watanzania!
  6...........................
  7..........................
  8..........................

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzania!
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,795
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  6. kiongozu mmoja anaweza kuamua kuwaita raia wa tanzania waishio pembezoni mwa mbuga za wanyama kwa zaidi ya miaka 100, kuwa wao ni "wamasai" tena wamasai wa kenya!! wnatimuliwa kwa mabavu, sisi tunasikia, tunachukizwa kidogo, halafu tunasahau, mwezi wa kumi wanatuambia nani kama kijani na njano, tunawapa kura.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  7. Mafisadi wanaendelea kutamba hakuna anayechukuliwa hatua yoyote na mafisadi hao hao wakirudi majimboni kwao mwezi Oktoba, mwaka huu utashangaa mwenyewe! Sisi kweli roho zetu "nzuri" sana, ya nini kumnyima mtu kula, sorry kura?
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,795
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  8. Mhasibu wa wilaya anatafuna mihela weeeeee! anajenga mahekalu na misururu ya magesti housi kila mahali, mshahara wake unajulikana, marupurupu na posho zinajulikana, haziwezi kujenga msururu wa magesti. watu wanajua, then wanakaa kimya, anatokea primier anasema nakusimamisha kazi uchunguzi ufanywe! sisi tunaona sawa tu! maisha yanaendelea......TAKUKURU na uasalama wanafanya vikao na kulala kwenye magesti hayo hayo! wala hawaulizi. sisi tunaona poa tu, ani kama kijani na njano, wakati wananitoa na tshirt an kofia vitakavyonifaa kwa miezi kadhaa ya jua la kijijini?!! sasa bana.
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  8. Tunawaondoa wananchi kwenye ardhi yao waliyoishi zaid ya miaka 30 tunakwenda kuwakatia mapori halafu tunampatia mwekezaji sehemu iliyokwisha tengenezwa na walalahoi. Nani mwenye uwezo wa kuondoa pori, mwekezaji au mwananchi maskini?
   
 6. N

  Nanu JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  9. Tunagawa ardhi yenye rutuba ifaayo kwa chakula kulima mazao kusema tutapata mafuta, chakula tunaagiza kutoka nje, ipi ghali kuagiza chakula nje ambayo kila mwenye pumzi anakula au mafuta ambayo yanatumiwa na magari yasiyozidi hata mil.1?
  Tanzania zaidi ya uijuavyo!
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,795
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  10. tunafunga viwanda vya kutengeneza vipuri kama machine tools, viwanda ambavyo vilikuwa vinatengeneza aina yeyote ya kipuri, hata kiwe cha gari moshi, then tunafungua soko la takataka - scraper za magari, vifaa vya magari vilivyokwisha kutumika na kuharibika (used), alafu tunaingiza na fake za taiwani. sisi tunaona tu! hakuna kiongozi anayesema au kuweka mipango ya udhibiti wa uingizaji wa vifaa wala ufufuaji wa viwanda vinavyoweza kuleta tija......tunadanganjwa wachina wataleta tvii za kisasa pale TBC, tunasema yeees! halafu tunawapa kura.
   
 8. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,469
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  11. Tunambiwa na JK kwamba ana mpango kabambe wa kujenga fly-overs Dar ili kupunguza foleni, wakati barabara zilizopo tu ni mbovu na finyu. Badala ya kumwambia akarabati na kupanua kwanza zilizopo, tunampigia makofi na kumpa kura tena 2010.

  12. Tunajengewa shule za sekondari za Kata zilizotoa wanafunzi 65,000 wenye divisheni ZIRO kisha serikali inaripoti UNDP kwamba school enrolment imepanda, bila kuzingatia wanafunzi hao wanapata elimu gani na katika mazingira yepi....!
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,795
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  12. Tunaambiwa nchi inafuata uongozi wa sheria, lakini kila kukicha polisi wanajigamba kwamba wameua majambazi 3, 4 6, tunachukulia poa tu! tumeshasahau kuua ni kuua tu, hasa ukiwa hujui aliye uwawa na kama yale ya kamanda Zombe au la!! sisi haooo, kwenye mistari ya kupiga kura na tunachagua rangi ya kijani na njano
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,188
  Likes Received: 33,453
  Trophy Points: 280
  Watanzania ni mazuzu magic
   
 11. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  13.Mkulu anatuambia kuwa tukitaka kula lazima tuliwe kidogo,watanzania wazuri tunakenua na kusifu kuwa hilo nalo neno!!!
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  14:Miundombinu yetu mibovu ndio inayoteketeza maisha ya watanzania kila siku kwa ajali za kila aina,kisha mkulu anatangaza vita dhidi ya ukimwi na malaria,ishu ambazo zinashibisha mitumbo ya wajanja wachache,kama kawa watanzania wazuri tunakubali nakufurahia kupigania vita ya kunenepesha mitumbo ya mijitu michache!!
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,188
  Likes Received: 33,453
  Trophy Points: 280

  umenena vyema sana mpwa..
  ukweli mtupu.
   
 14. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 2,020
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  15. Muungwana akisema asilima 70 tunaangalia upepo unakoelekea tunashangilia na kukenua bila kujiuliza sie tupo kundi lipi.
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,188
  Likes Received: 33,453
  Trophy Points: 280
  hapa umelonga ukweli mno kaka.
   
 16. B

  BUBBA Member

  #16
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  13. Tanzania ni Nchi nzuri, hata asiyefanya kazi anataka aishi maisha ya juu akishindwa anatafuta pa kupeleka lawama zake bila kuangalia nini amekosea kwa maisha anayoishi.
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 40,188
  Likes Received: 33,453
  Trophy Points: 280
  hapa umelonga ukweli mno kaka.
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Feb 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  Ukishindwa kutawala Tanzania basi wewe huwezi kutawala inji yoyote duniani!
   
 19. M

  Mukubwa Senior Member

  #19
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 125
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  14/ Wantania wamesoma lakini kwa kutokujiamini wanaletewa mdosi ambaye wanamzidi elimu kuwa mkubwa wao wa kazi na anapata mshara maradufu ya wao, kwa uzuri wao watamtengenezea working permit fake na kuishia kujipendekeza kwake
   
 20. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dah! hapa umenikuna kweli!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...