Tanzania ni Nchi Nzuri Sana na Ina Watu "Wazuri!"

Aaa Jf ina watu wanaofikiri sana nimeipenda sana hii post,ngoja sasa niwagongee thanks.
 
11. Tunambiwa na JK kwamba ana mpango kabambe wa kujenga fly-overs Dar ili kupunguza foleni, wakati barabara zilizopo tu ni mbovu na finyu. Badala ya kumwambia akarabati na kupanua kwanza zilizopo, tunampigia makofi na kumpa kura tena 2010.

12. Tunajengewa shule za sekondari za Kata zilizotoa wanafunzi 65,000 wenye divisheni ZIRO kisha serikali inaripoti UNDP kwamba school enrolment imepanda, bila kuzingatia wanafunzi hao wanapata elimu gani na katika mazingira yepi....!

Mkuu umeongea halafu hizo shule zenyewe sasa zina matatizo lukuki kila kukicha ni matatizo,jumamosi nilienda kwenye kikao cha shule moja yaani nilichoka ni matatizo tu tangu hiyo shule imeanza,atakuja diwani atawaambia msijali hii ni shule yetu na itakua nzuri hizi kero zote zitaondoka.
 
13.Anatokea kiongozi mwingine anawafananisha watanzania na mbuzi eti hata wakila majani poa tu ilimradi rada inunuliwe na watanzania walivyopoa wanasema sawa baba kwani kuwa mbuzi,kondoo etc kitu gani...kesho akiomba kura watampa aendelee kuwaita mbuzi wao poa tu...
 
13.Anatokea kiongozi mwingine anawafananisha watanzania na mbuzi eti hata wakila majani poa tu ilimradi rada inunuliwe na watanzania walivyopoa wanasema sawa baba kwani kuwa mbuzi,kondoo etc kitu gani...kesho akiomba kura watampa aendelee kuwaita mbuzi wao poa tu...

14. Tumeambiwa tutarudishiwa chenji na Uingereza baada ya BAE kukiri kuwahonga wakubwa wetu, kama kawa waliohongwa wakienda majimboni watakubaliwa na watanzania "wazuri!" Who cares?
 
Chama kina ahidi kwamba wananchi wa jamii fulani watapata mahakama ya kadhi lakini wanapiga danadana wee (danganya toto) hatimaye wananchi wataambiwa mchakato unaendelea...na watatoa kura shame!
 
"Watanzania ni wazuri sana! Hata ukiwaomba mlima Kilimanjaro watakupa tu" -- Wachezaji wa timu ya taifa ya Burundi, baada ya mechi na taifa stars Uwanja wa Taifa. Wakishangaa ilikuwaje hawakufungwa, licha ya nafasi zote za wazi... circa 1995.
 
15. Bunge lina hairishwa kirahisirahisi tu eti kamati azija jiridhisha kuwa ripoti zimekamilika, walikuwa wapi miaka yote mbona kila kikao ni hivi?
Naibu spika anasema muda auta ongezwa kwahiyo hizo ripoti azina nafasi tena tusubiri kikao kijacho cha bunge
 
15. Bunge lina hairishwa kirahisirahisi tu eti kamati azija jiridhisha kuwa ripoti zimekamilika, walikuwa wapi miaka yote mbona kila kikao ni hivi?
Naibu spika anasema muda auta ongezwa kwahiyo hizo ripoti azina nafasi tena tusubiri kikao kijacho cha bunge

Hayo mambo yanawezekana mahali penye watu "wazuri" kama Tanzania!
 
Watanzania tu wema sana tunagawa tani kwa matani ya dhahabu za mabilioni kwa wageni baadaye tunaenda kwao kutembeza bakuli la dola laki tano tena za mkopo
 
Jamani tuache utani, watanzania ni watu "wazuri" na nchi yao pia ni nzuri sana! Kwa nini?
1. Mbunge akiona hajafanya chochote ndani ya kipindi cha miaka 4 anarudi mwaka wa tano na kuwaahidi kwamba atafanya makubwa, watanzania kwa jinsi walivyo "wazuri" wanampa kura.
2. Rais alitoa ahadi nyingi sana na kama angezitekeleza Tanzania ingekuwa nchi inayotiririka "asali na maziwa,"lakini mimi sina uhakika kama ametekeleza hata moja, mwaka huu mwezi Oktoba Rais akiomba kura utashangaa watanzania walivyo "wazuri" watampa kura!
3. Wageni toka nje wanakuja nchini kwetu wanachota vijisenti kupitia mikataba mibovu, watanzania walivyo "wazuri" wananung'unika siku mbili tatu, kisha mkubwa wao anawaahidi kuunda Litume la kupitia mikataba mibovu. Mkubwa akiona watanzania "wazuri" wameshatulia basi anaweka likarabrasha kwenye shelf!
4. Mkubwa akisoma hotuba Bungeni kwamba eti kuna wezi wamerudisha vijisenti walivyoiba bila kuwataja wezi wenyewe! Watanzania "wazuri" walinung'unika kichini chini lakini wakaahidiwa kwamba vijisenti hivyo vitawekwa kwenye Benki yao ya Raslimali bila hata kuridhiwa na Bunge! Watanzania "wazuri" wakaridhika na mpaka sasa haijulikani kwamba vijisenti hivyo viliwekwa huko na kama wakulima walifaidika au la! Hata kama ikitokea walifaidika, wezi wasio na majina walifanywa nini?
5. Ama kweli Tanzania ni nchi "nzuri," ndio maana hata Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya wanakomalia sana Jumuiya ya Afrika Mashariki (yaani kuwa nchi moja) kwa sababu wanajua "uzuri" wa Tanzania na Watanzania!
6...........................
7..........................
8..........................

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzania!

Ni kweli kwa sababu WaTanzania tumelala usingizi Mnono na Elimu yetu Fupi kama akili zetu zilizo fupi ama kweli waswahili husema kuwa (MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO)tuamkeni kuchaguwa viongozi wenye Elimu jamani Hatuna Maji Masafi,Hatuna umeme Uchumi tunao tunaukalia kwanini jamani Tuamkeni ndugu zangu WaTanzania
 
just an observation.

ugandans form rebel millitias to protest the govt, kenyans will take to the streets in a moments notice to protest the govt, tanzanians will peacefully protest the govt.
 
Back
Top Bottom