Tanzania ni laana au viongozi?

Yana bwana Mkombozi mi naomba uamini kitu kimoja, hawa wazee wetu walioko madarakani uwezo wao ni mdogo mno. Mimi nawafahamu sababu nimesha deal nao. 3 years ago nilipata bahati ya kusimamia investment moja ya kama $4.5 million. Nili deal na goverment institutions zote TIC, TRA, BOT, IMMIGRATION, BOT, TANAPA NA NCAA. Acheni jamani ni aibu!!! wanachojua ni kupanga safari tu ili wapata imprests
 
Yana bwana Mkombozi mi naomba uamini kitu kimoja, hawa wazee wetu walioko madarakani uwezo wao ni mdogo mno. Mimi nawafahamu sababu nimesha deal nao. 3 years ago nilipata bahati ya kusimamia investment moja ya kama $4.5 million. Nili deal na goverment institutions zote TIC, TRA, BOT, IMMIGRATION, BOT, TANAPA NA NCAA. Acheni jamani ni aibu!!! wanachojua ni kupanga safari tu ili wapata imprests

Nani anawapa hayo madaraka?
 
Viongozi wetu wanatoka miongoni mwetu sisi wenyewe na ni sisi wenyewe ndiyo tunawapa hiyo dhamana ya kutuongoza. Kwa hiyo viongozi wetu wanaakisi jamii nzima waiongozayo. Sasa kwa kufuata mantiki hiyo utaona kuwa viongozi wetu kama ni vilaza basi na sisi ni vilaza vile vile.
Nakubaliana na wewe kabisa asilimia 100 sisi wote ni vilaza tusingekubali upupu wa ujinga kiasi hiki uendelee nchini kwetu tungekataa,natungewakomalia wangeshika adabu zao kweli kabisa sisi ni vilaza wa kutupwa hakuna sababu hata moja y nchi hii kuwa maskini
 
Tukiendelea kuwachagua viongozi wapuuzi basi kaburi tunalowachimbia watoto wetu ni kubwa mno,watu wanatumia propaganda ya amani kuitafuna nchi sie tumelala tu.
 
Kama una amini mambo ya laana nadhani ingekuwa imeshawafikia viongozi wetu kwa dhuluma wanayowafanyia watanzania.
 
Libya wana petro-dollar wewe... Nyie uchumi wenu wa kuuza korosho, viazi, mchele, dhahabu na bongo fleva... Sio kwamba hatuna raslimali, lakini mafuta is a game changer... subiri uone Kampala baada ya miaka 10. Mafuta ogopa, yanaendesha uchumi wa dunia. Pamba na korosho hamna kitu..

Kwani Singapore, Israel na Taiwan nao wana mafuta?
 
Walishatuambia "nchi haina rasilimali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!" hivi waseme mara ngapi ndipo tujue:

Wamesahau wakati tunasoma walituimbisha "ili tuendelee tunahitaji mambo manne "WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA" hapo hapakuwa pakitajwa RASILIMALI kwa sababu zilikuwapo... sasa sijui zimeenda wapi baada ya miaka michache tu :embarrassed: (yaani wanatuaminisha "hakuna madini, hakuna mbuga za wanyama, hakuna samaki, ardhi yetu haina tija, bandari yetu iko kama pambo.. na.. na... na.... na.... wizi mtupu!
hapana sio laana TUMIROGWA
Rasilimali zetu zilituwasha, tukaamua kuzigawa kwa style ya kubinafusisha. Hivyo tumebaki bila rasilimali, anzania kwenye madini, mbuga za wanyama (huko kuna vitaru vya wawindaji), nenda kwenye viwanda, fika kwenye sekta ya usafiri - ATCL and TRA tembelea Ubungo bus terminal asilimia 70 ya mabasi ni malori (Fuso type), nenda kwenye vitowewo - mtanzania saizi yake ni mapanki, njoo kwenye ardhi - ranchi za taifa zimeuzwa kwa bei ya ubuyu. Hizo natumai ni salaam tu; ukisitaajabu ya Musa utaona ya Filauni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom