Tanzania ni kama wameiaga demokrasia, upinzani Chadema wasusia uchaguzi huku wakilalamikia uhuni wa serikali

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,760
48,408
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku kikiwataka wagombea wake waliochezewa rafu kuacha kukata rufaa.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amatangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa ambapo amesema sababu kubwa ni wagombea wa chama hicho kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.

Mbowe amesema mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na wabunge, maazimio waliyokubaliana ni kugomea uchaguzi huo sababu majina ya wagombea wengi kukatatwa.

“Sisi kama chama tumeamua hatutashiriki zoezi hili na ninatoa amri kama Mwenyekiti wa viongozi na wagombea nchi nzima wasitishe kugombea na wasitishe kukata rufaa.

“Waachane na kuweka mapingamizi hatupo tayari kubariki ubatili, huu ni uhuni, wananchi wana hasira na wana haki ya kuwa na hasira na waendelee kuwa na hasira,” amesema Mbowe.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

Chanzo: Mtanzania
 
Wapinzani nchini ni kama magaidi, sijawahi ona upinzani wa hovyo na wa kishamba kama wa Tanzania, wao kuside na watu wanaotaka kuliangamiza Taifa ni kawaida na ndio maana wapinzani Tanzania hawapendwi.
 
Wapinzani nchini ni kama magaidi, sijawahi ona upinzani wa hovyo na wa kishamba kama wa Tanzania, wao kuside na watu wanaotaka kuliangamiza Taifa ni kawaida na ndio maana wapinzani Tanzania hawapendwi.
Kama mna uhakika awapendwi si muweke chaguzi huru na haki..

Kama mna uhakika hawapendwi kwann mnatumia nguvu kubwa kuwamaliza?
 
Ambao hamko ndanî ya Tanzania, mkisoma mitandao ya kijamii ambayo upinzani wmeamua kwekeza nguvu nyìngi badala ya kuwekeza kwenye mitaa halisi unaweza sema Tanzania kuna tatizo.

Njoo field ujionee, rais ana sapoti kubwa sana ya wananchi. Ila humu JF wengi ni upinzni ambao kuihalisia hawafiki laki 5.
 
MK254 , huku 🇹🇿 tumerudi kwenye primitive age. Zama za kale za mawe Stone age. Hata flinston cartoon siku hizi wako kwenye digital era
Fanyeni uchaguzi wa chama wa mwenyekiti kwanza ndio muongee demokrasia.
Mnavunja katiba ya chadema.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Kwa hili tunaomba "RAIA WA KENYA" tuweke "BEEF" pembeni, halafu mtusaidie kupigia kelele huu ubakwaji wa demokrasia.

Pakichafuka Tanzania, mjue tutakimbilia kwenu majirani zetu. Tutabanana hapo hapo kwenu. Shauri yenu.
Yaani wewe umeshindwa, uwaombe wakenya?
Kituko.
 
Ambao hamko ndanî ya Tanzania, mkisoma mitandao ya kijamii ambayo upinzani wmeamua kwekeza nguvu nyìngi badala ya kuwekeza kwenye mitaa halisi unaweza sema tz kuna tatizo.
Njoo field ujionee, rais ana sapoti kubwa sana ya wananchi. Ila humu jf wengi ni upinzni ambao kuihalisia hawafiki laki 5.
Yeah ni kweli, upinzani wa kipindi hichi wanakwama vibaya mno. Kipindi cha JK walisema wanataka Rais awe mkali apambane na mafisadi na kunyoosha nchi, sasa hivi wameletewa Rais mkali hawamtaki tena kazi yao imebaki ni kupinga pinga kila kitu, na kuandika maujinga kwenye mitandao ya kijamii.

Mimi niko upinzani na kadi yao ya chama ninayo lakini kipindi hiki nishaachana nao kutokana na siasa zao zisizoeleweka kipindi hiki.

Wao ni kuangalia tu ni nini kipo kwenye trending ili waende nayo ili wapate kiki. Sometimes wanachukua picha za matatizo ya nchi nyingine alafu wanaanza kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii wakisema eti ni Tanzania 😂😂😂
 
Ambao hamko ndanî ya Tanzania, mkisoma mitandao ya kijamii ambayo upinzani wmeamua kwekeza nguvu nyìngi badala ya kuwekeza kwenye mitaa halisi unaweza sema tz kuna tatizo.
Njoo field ujionee, rais ana sapoti kubwa sana ya wananchi. Ila humu jf wengi ni upinzni ambao kuihalisia hawafiki laki 5.
Acha uongo, mbona figisu nyingi kwenye chaguzi.
 
Back
Top Bottom