Tanzania imetajwa kuishinda Kenya kama mahali bora zaidi pa kuwekeza kwa wawekezaji wanaotafuta fursa katika eneo la Afrika Mashariki, kulingana na utafiti mpya wa KPMG.
Kwa mujibu wa KPMG, asilimia 15 ya wakuu wa kampuni katika eneo hilo walisema wangewekeza nchini Tanzania ikilinganishwa na asilimia 14 waliopendelea Kenya.
Ikumbukwe kuwa Kenya ndiyo Taifa lenye uchumi mkubwa zaidi katika eneo la Afrika Mashariki ingawa kwa miaka ya karibuni uchumi wa Tanzania umekuwa ikikua kwa kasi.
Nchi zenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, kama Afrika Kusini na Nigeria zimeyazidi mataifa haya ya Afrika Mashariki ambapo zilipata wastani wa asilimia 50 na asilimia 30 ya waliotoa majibu mtawalia.
Afrika Kusini inatarajiwa kuipita Nigeria mwaka 2024 kurudia nafasi yake kama Taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
Ghana, ambayo imepitia msukosuko wa kiuchumi katika mwaka uliopita, ilishindana na Kenya katika utafiti huo katika nafasi ya nne.
Utafiti ulibaini kuwa teknolojia za kifedha, mafuta na gesi, bidhaa za watumiaji, na uchimbaji madini utaendesha uwekezaji mwingi katika miaka miwili ijayo.
Utafiti huo ulihoji wakuu wa biashara wenye uzoefu wa kufanya mikataba kutaja nchi wanazoangalia kwa ununuzi au uwekezaji barani hasa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa miaka miwili ijayo.
"Katika nusu ya pili ya mwaka 2022, wakuu 150 wa kampuni na wakuu wengine waandamizi walifanyiwa utafiti kulingana na uzoefu wao wa kusimamia mikataba Kusini mwa Jangwa la Sahara (AKJS) katika miaka minne iliyopita," KPMG ilieleza katika ripoti yao.
Utafiti huo ulijumuisha wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.
"Kikundi cha wanaojibu kilitengwa sawasawa kati ya wawekezaji wa ndani (yaani, walioko AKJS) na wawekezaji wa kimataifa (yaani, walioko nje ya AKJS)," ripoti ilibainisha.
"Miongoni mwa wawekezaji wa ndani, asilimia 71 walikuwa wawekezaji wa mkakati na asilimia 29 walikuwa wawekezaji wa kifedha. Miongoni mwa wawekezaji wa kimataifa, asilimia 69 walikuwa wawekezaji wa mkakati na asilimia 31 walikuwa wawekezaji wa kifedha."
Disclaimer: Chanzo cha habari hii ni mtandao wa
Kenyans.co