Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Huwa najiuliza kama wanadamu tunatumia angalau ule uwezo mdogo wa kufikiri ambao tumejaliwa na Mwenyezi Mungu katika kufanya maamuzi, ukizingatia kwamba wanaotunga sheria za nchi ni wanadamu wanaopaswa kuwa na akili timamu.
Hebu fikiria hili; polisi wanakukamata na kukupeleka mahabusu. Ukiwa na ngekewa utafikishwa mahakamani kabla ya masaa 48 kupita kama inavyotaka sheria. Sasa kioja ni pale unafikishwa mahakamani na polisi wanamwambia hakimu tunaomba kesi iahirishwe kwa kuwa upelelezi haujakamilika. Na hakimu katika mwisho wa busara zake, anawakubalia polisi na kuruhusu urudishwe rumande wakati polisi wanaendelea kufanya upelelezi.
Tujiulize maswali haya;
Na nyie mahakimu nchini, ni wapi mlipoisoma sheria inayosema kama upelelezi haujakamilika mtu anyimwe dhamana na arudishwe rumande? Jaji Mkuu, tuambieni kama kuna hiyo sheria. Au hauoni kwamba mtu kukaa rumande tayari anatumikia adhabu kabla hajatiwa hatiani? Mnakuwaje so blind kwa unayanyasi huu wa raia na kushirikiana na polisi kuuendeleza?
Kama kweli raisi Magufuli ana uchungu na watu walio gerezani au mahabusu bila hatia, basi aanze na hao wanaowekwa ndani wakati "upelelezi haujakamilika" kwa sababu hawa wako ndani bila kuwa wamekutwa na hatia na kuhukumiwa. La sivyo tunafanya unafiki na propaganda za kisiasa tu. Kama upelelezi haujakamilika basi mtuhumiwa asikamatwe au akikamatwa aruhusiwe dhamana wakati upelelezi unaendelea. Madai ya polisi kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana ataingilia upelelezi ni uropokaji ambao haupaswi kuvumiliwa katika nchi inayotaka kufuata utawala wa haki na sheria.
=====
UPDATES:
=====
Miaka mitatu iliyopita, August 2019, niliandika hii thread.
Nashukuru sana kuona kwamba leo hii serikali imechukua hatua stahiki. Hii ni kuthibitisha kwamba JF inafikisha ujumbe kwa wanaohusika. Tuendeleze kuweka mambo wazi

- Kama upelelezi haujakamilika, kwa nini mmemkamata mtuhumiwa?
- Kwa nini hakimu aruhusu urudishwe rumande wakati ameshaelezwa wazi na polisi au mwendesha mashtaka kwamba hadi wakati huo unafikishwa mahakamani hawana ushahidi wa kukutia hatiani na ni kama wanahisi tu kwamba una kosa?
- Na kama upelelezi bado unaendelea, polisi na hakimu wanajuaje huo upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa ataonekana alihusika na tukio alilokamatiwa? (upelelezi haujakamilika)
- Je bado hatuelwi kwamba kumweka mtu mahabusu ni tayari tunampa adhabu kabla hata hajatiwa hatiani?
Na nyie mahakimu nchini, ni wapi mlipoisoma sheria inayosema kama upelelezi haujakamilika mtu anyimwe dhamana na arudishwe rumande? Jaji Mkuu, tuambieni kama kuna hiyo sheria. Au hauoni kwamba mtu kukaa rumande tayari anatumikia adhabu kabla hajatiwa hatiani? Mnakuwaje so blind kwa unayanyasi huu wa raia na kushirikiana na polisi kuuendeleza?
Kama kweli raisi Magufuli ana uchungu na watu walio gerezani au mahabusu bila hatia, basi aanze na hao wanaowekwa ndani wakati "upelelezi haujakamilika" kwa sababu hawa wako ndani bila kuwa wamekutwa na hatia na kuhukumiwa. La sivyo tunafanya unafiki na propaganda za kisiasa tu. Kama upelelezi haujakamilika basi mtuhumiwa asikamatwe au akikamatwa aruhusiwe dhamana wakati upelelezi unaendelea. Madai ya polisi kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana ataingilia upelelezi ni uropokaji ambao haupaswi kuvumiliwa katika nchi inayotaka kufuata utawala wa haki na sheria.
=====
UPDATES:
=====
Miaka mitatu iliyopita, August 2019, niliandika hii thread.
Nashukuru sana kuona kwamba leo hii serikali imechukua hatua stahiki. Hii ni kuthibitisha kwamba JF inafikisha ujumbe kwa wanaohusika. Tuendeleze kuweka mambo wazi
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), apiga marufuku watuhumiwa kushikiliwa kabla upelelezi haujakamilika
Agizo hilo limetolewa kupitia Muongozo wa Mashitaka Namba 1 wa mwaka 2022 ambao pia unaagiza upelelezi wa mashitaka kukamilika ndani ya siku 90 na zikizidi iwe kwa kibali maalumu cha DPP. Aidha muongozo huo umeongeza kifungu cha 131A kinachoweka ulazima wa kukamilisha upelelezi kabla ya...
www.jamiiforums.com