Tanzania na uvunjaji wa haki za binadamu uliokithiri: Kwanini umweke mtuhumiwa rumande na hata kumnyima dhamana wakati upelelezi haujakamilika?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,128
18,733
Huwa najiuliza kama wanadamu tunatumia angalau ule uwezo mdogo wa kufikiri ambao tumejaliwa na Mwenyezi Mungu katika kufanya maamuzi, ukizingatia kwamba wanaotunga sheria za nchi ni wanadamu wanaopaswa kuwa na akili timamu.

Hebu fikiria hili; polisi wanakukamata na kukupeleka mahabusu. Ukiwa na ngekewa utafikishwa mahakamani kabla ya masaa 48 kupita kama inavyotaka sheria. Sasa kioja ni pale unafikishwa mahakamani na polisi wanamwambia hakimu tunaomba kesi iahirishwe kwa kuwa upelelezi haujakamilika. Na hakimu katika mwisho wa busara zake, anawakubalia polisi na kuruhusu urudishwe rumande wakati polisi wanaendelea kufanya upelelezi.

Tujiulize maswali haya;
  1. Kama upelelezi haujakamilika, kwa nini mmemkamata mtuhumiwa?
  2. Kwa nini hakimu aruhusu urudishwe rumande wakati ameshaelezwa wazi na polisi au mwendesha mashtaka kwamba hadi wakati huo unafikishwa mahakamani hawana ushahidi wa kukutia hatiani na ni kama wanahisi tu kwamba una kosa?
  3. Na kama upelelezi bado unaendelea, polisi na hakimu wanajuaje huo upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa ataonekana alihusika na tukio alilokamatiwa? (upelelezi haujakamilika)
  4. Je bado hatuelwi kwamba kumweka mtu mahabusu ni tayari tunampa adhabu kabla hata hajatiwa hatiani?
Tanzania ifikie mahali ambapo tukiri kwamba tumekuwa mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa katika awamu hii ya tano. Ifikie hatua suala la kumkamata mtu "akaisadie polisi" wakati upelelezi unaendelea iwe ni kutendea kinyume cha maumbile haki za binadamu au unyanyasaji wa Watanzania. Natoa wito kwa wadau wa sheria kuliangalia hili suala kwa mapana yanayostahili kwa sababu suala la polisi kuweka watu ndani "ili waaidie polisi" wakati upelelezi unakamilishwa ni mojawapo ya mianya mikubwa inayotumika nchini kukomoa watu.

Na nyie mahakimu nchini, ni wapi mlipoisoma sheria inayosema kama upelelezi haujakamilika mtu anyimwe dhamana na arudishwe rumande? Jaji Mkuu, tuambieni kama kuna hiyo sheria. Au hauoni kwamba mtu kukaa rumande tayari anatumikia adhabu kabla hajatiwa hatiani? Mnakuwaje so blind kwa unayanyasi huu wa raia na kushirikiana na polisi kuuendeleza?

Kama kweli raisi Magufuli ana uchungu na watu walio gerezani au mahabusu bila hatia, basi aanze na hao wanaowekwa ndani wakati "upelelezi haujakamilika" kwa sababu hawa wako ndani bila kuwa wamekutwa na hatia na kuhukumiwa. La sivyo tunafanya unafiki na propaganda za kisiasa tu. Kama upelelezi haujakamilika basi mtuhumiwa asikamatwe au akikamatwa aruhusiwe dhamana wakati upelelezi unaendelea. Madai ya polisi kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana ataingilia upelelezi ni uropokaji ambao haupaswi kuvumiliwa katika nchi inayotaka kufuata utawala wa haki na sheria.

=====

UPDATES:

=====

Miaka mitatu iliyopita, August 2019, niliandika hii thread.

Nashukuru sana kuona kwamba leo hii serikali imechukua hatua stahiki. Hii ni kuthibitisha kwamba JF inafikisha ujumbe kwa wanaohusika. Tuendeleze kuweka mambo wazi

Hii ni nchi ya Wakolomije. Hamna mwenye haki zaidi ya hao wazawa wa kolomije
Na wabunge wamekaa tu wana mu-admire speaker pale mbele, huku wanasubiri wamalize muda wao wapewe maslahi yao. Yaani hili hawalioni kabisa kwamba ni tatizo. Hao walioko CCM ambao ndio wengi hata kufungua midomo kulikemea hili hawathubutu, kwa sababu hawapo pale kwa ajili ya wananchi bali wako pale kwa ajili yao wenyewe na kuitukuza serikali ya chama chao, wakiwa na upofu wa kutoona sheria hizi kandamizi zinaweza kuwaathiri wao wenyewe, watoto wao na ndugu zao. Pathetic.
 
Na wabunge wamakaa tu tu wana mu-admire speaker pale mbele, huku wanasubiri wamalize muda wao wapewe viinua maslahi yao. Yaani hili hawalioni kabisa kwamba ni tatizo. Hao walioko CCM ambao ndio wengi hata kufungua midomo kulikemea hili hawathubutu, kwa sababu hawapo pale kwa ajili ya wananchi bali wako pale kwa ajili yao wenyewe na kuitukuza serikali ya chama chao, wakiwa na upofu wa kutoona sheria hizi kandamizi zinaweza kuwaathiri wao wenyewe, watoto wao na ndugu zao. Pathetic.
Nchi ovyo sana hii
Viongozi at all levels ni self centred
 
Nchi hii watoa maamuzi hawakuandaliwa kwa kazi hii,imagine nchi ina kiongozi kama bashite,..seriously daud albert bashite

Mkuu huyo daud albert bashite ana cheo gani kwani?

Mimi naamini iwapo itatokea siku ccm ikatuachia nchi yetu, basi huenda tukaishi maisha ya furaha na amani sana badala ya haya maisha yaliyojaa stress.
 
u
Tza unakamatwa kwanza ndipo ushahidi unaanza kutafutwa,nchi zingine unatafutwa ushahidi kwanza uliokamilika ndipo unakamatwa.
nawajua wabongo wewe ? mpaka uje upate ushahidi kishajibadirisha mpaka jinsia htakaa umpate milelee
 
Tuna sheria mbovu na za hovyo kabisa. Ukiwa na sheria za hovyo halafu ukawapata wasimamizi wa hovyo, madhara ni makubwa sana kwa raia.
 
Huwa najiuliza kama wanadamu tunatumia angalau ule uwezo mdogo wa kufikiri ambao tumejaliwa na Mwenyezi Mungu katika kufanya maamuzi, ukizingatia kwamba wanaotunga sheria za nchi ni wanadamu wanaopaswa kuwa na akili timamu.

Hebu fikiria hili; polisi wanakukamata na kukupeleka mahabusu. Ukiwa na ngekewa utafikishwa mahakamani kabla ya masaa 48 kupita kama inavyotaka sheria. Sasa kioja ni pale unafikishwa mahakamani na polisi wanamwambia hakimu tunaomba kesi iahirishwe kwa kuwa upelelezi haujakamilika. Na hakimu katika mwisho wa busara zake, anawakubalia polisi na kuruhusu urudishwe rumande wakati polisi wanaendelea kufanya upelelezi.

Tujiulize maswali haya;
  1. Kama upelelezi haujakamilika, kwa nini mmemkamata mtuhumiwa?
  2. Kwa nini hakimu aruhusu urudishwe rumande wakati ameshaelezwa wazi na polisi au mwendesha mashtaka kwamba hadi wakati huo unafikishwa mahakamani hawana ushahidi wa kukutia hatiani na ni kama wanahisi tu kwamba una kosa?
  3. Na kama upelelezi bado unaendelea, polisi na hakimu wanajuaje huo upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa ataonekana alihusika na tukio alilokamatiwa? (upelelezi haujakamilika)
  4. Je bado hatuelwi kwamba kumweka mtu mahabusu ni tayari tunampa adhabu kabla hata hajatiwa hatiani?
Tanzania ifikie mahali ambapo tukiri kwamba tumekuwa mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa katika awamu hii ya tano. Ifikie hatua suala la kumkamata mtu "akaisadie polisi" wakati upelelezi unaendelea iwe ni kutendea kinyume cha maumbile haki za binadamu au unyanyasaji wa Watanzania. Natoa wito kwa wadau wa sheria kuliangalia hili suala kwa mapana yanayostahili kwa sababu suala la polisi kuweka watu ndani "ili waaidie polisi" wakati upelelezi unakamilishwa ni mojawapo ya mianya mikubwa inayotumika nchini kukomoa watu.

Na nyie mahakimu nchini, ni wapi mlipoisoma sheria inayosema kama upelelezi haujakamilika mtu anyimwe dhamana na arudishwe rumande? Jaji Mkuu, tuambieni kama kuna hiyo sheria. Au hauoni kwamba mtu kukaa rumande tayari anatumikia adhabu kabla hajatiwa hatiani? Mnakuwaje so blind kwa unayanyasi huu wa raia na kushirikiana na polisi kuuendeleza?

Kama kweli raisi Magufuli ana uchungu na watu walio gerezani au mahabusu bila hatia, basi aanze na hao wanaowekwa ndani wakati "upelelezi haujakamilika" kwa sababu hawa wako ndani bila kuwa wamekutwa na hatia na kuhukumiwa. La sivyo tunafanya unafiki na propaganda za kisiasa tu. Kama upelelezi haujakamilika basi mtuhumiwa asikamatwe au akikamatwa aruhusiwe dhamana wakati upelelezi unaendelea. Madai ya polisi kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana ataingilia upelelezi ni uropokaji ambao haupaswi kuvumiliwa katika nchi inayotaka kufuata utawala wa haki na sheria.
.
 
Back
Top Bottom